Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

[emoji23][emoji23]so,mlikuwa mnaimbiwa masongi kama the gambler bila nyie kupenda?..haka kajamaa kalikuwa kashenzi kweli kweli.
 
Watu wanatenguliwa sababu ya utendaji wao na sio sababu mbowe ni mtoto wa mjini🤣🤣🤣
Siku utakapoguswa wewe mama D huo upepo wa bendera utaupunga vinginevyo. Hapo hujatambua tu ndani serikali iliyopita ndani kwa ndani walikuwa hawapatani na chokochoko zilikuwa nyingi. Walishughulikiana kimya wenyewe kwa wenyewe nyie huku nje mkikenue kumwaga sifa.

Sikiliza mama, ni hivi mama anaadabisha vifaranga vyake kwa hasira kwa kuwa vilikuwa vinamdharau enzi hizo, kwa yakini atawasambaratisha kweli, vifaranga pamoja na udogo wao wataondoka kwenye himaya kwenda kujitafutia bila kuogopa hatari mwewe nje. Vifaranga watapambana kimya kimya kulinda uhai wao hatimaye watakuwa wazima hata hivyo hatarejea kumsalimia mama. Baada ya kumaliza zoezi la kushughulikia vifaranga vyake na vikatoweka kwenye mbele yake na usumbufu kupungua, Mama atabaki mpweke, watu wazima walikuwa wakishangilia mama kuwashughulikia vifaranga vyake hawatamfariji kwa kuwa na wao wanahitaji kukaa kwenye kiota hicho.

Msimu wa mvua utawadia, mama atakimibilia kwenye kiota akidhani atwakuta vifaranga wamerejea nyumbani ili awapashe joto, lakini wapi

Kiangazi hicho kinafika kwa msimu wa mavuno, kwenda shambani anakuta mazao yote wametafuna wale walioukuwa wakimshangilia, yeye hana akiba ya chakula, kisha anaanza safari za kuingia msituni kujitafutia chakula na ahitaji mengine

Wawindaji wanaingia msituni na kuchioma moto ili kuwaibua wanyama waliwao wawawinde, kiota cha mama kiko katikati ya mstu huo na yeye yuko mbali anahea kwa ajili ya familia. Kwa mbali anaona moto unaotoa moshi, anabeba furushi dogo ili awahi kwenye kiota kuzuia kisiungue moto, lakini inashindikana................ndipo anajitokeza mama mmoja jamii ya mbuni ambaye na yeye ana mayai yake kwenye ardhi ndani ya huo msitu anakimbia kwa ksai ya kilomita 70 kuelekea mtoni anafika anjiloweka kwenye maji kisha kwa kasi ile ile anarejea kwenye tawa la mayai yake na kuzima moto ambao tayari ulikuwa umefika eneo hilo. Mama anayehea msituni naye anafika kwenye kiota chake huku akimtizama mbuni anavyoyalinda mayai yake kwa upendo, wakati kiota chake kisicho na vifaranga wala mayai kikiteketea kwa moto bila msaada wa jeshi kubwa lililoonekana kumpa moyo mama. Kisha mama anajawa na mawazo na kufanya maamuzi ya kuhama huku akiwa amepata hasara isiyoelezeka.
 
Kumbe sabaya ndo alikuwa firauni kiasi hicho, mungu ni muweza
 
Tanzania kama huna PHD ya kupika MAJUNGU na FITINA huwezi KUDUMU kazini au kwenye siasa.
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan hawa pichani ni waliokuwa walinzi wa Freeman Mbowe. Kuna Khalifa Hassan, Adam Kasekwa (ADAMO) na Mohamed Lingwenya.. Freeman Mbowe aliongeza ulinzi wa kutembea nao baada ya kuvamiwa Dodoma na kuvunjwa mguu wake wa kulia.

Wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu (aliyekuwa DC wa HAI) Lengai Ole Sabaya na genge lake walivamia hotel ya Freeman Mbowe inaitwa 'Protea Hotel Aishi Machame', huko Hai, wakawakamata hawa watu, wakapewa kesi ya UGAIDI. Pia wakabebeshwa mzigo wa nguo na sare za JWTZ na wakaambiwa wamekutwa nazo, wakapewa na vilipuzi.

Mashtaka mengine ni kukutwa na silaha pamoja na dawa za kulevya aina ya Heroin.. Waliteswa sana. Walipigwa sana. Waliumizwa sana. Tazama makovu yao. Waone walivyokondeana. Hawa wanaishi Tundu la choo hapa, pua zao hapa. Wapo gereza la Segerea.

Wanafungiwa private cell. Kila mmoja room yake. Hawatoki nje isipokuwa saa 11 alfajiri wakati wa kufunguliwa, kuhesabiwa na kupewa uji, saa 3 asubuhi kupewa ugali maharage, na saa 9 mchana wanafungiwa. Muda wote wamefungwa pingu kwenye miguu na mikono yao. Upelelezi haujawahi kukamilika.

Mahakamani hawapelekwi na hata usikilizwaji wa kesi kwa njia za video hawafanyiwi. Mahakama ni kama imewasahau. Sio sawa kabisa hii. Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kuna watu wanateseka sana kwa sababu ya amri za SABAYA. Wapo wengi, hawa ni baadhi.

Tunamtaka DPP aharakishe upelelezi wa kesi ya hawa ndugu zetu wenye familia zao au vinginevyo, awaachie huru watu hawa wanateseka bila hatia.. Hizi ni roho chafu na hila za shetani. Nchi yetu sio ya kidikteta.. SABAYA amewaumiza sana watu HAI. Ushahidi upo. @ MMM

 
Mkuu huyu sabaya alikuwa kaa la moto, kwa waTz wote .
Alikuwa ni kjana hatari kwa maslai mapana ya Taifa
Kama kweli alinda haya basi kifungo kinamfaa kwa asilimia kubwa
 
Malisa usisahau kuandaa makala nzuri kama hii uanike uovu wa aliekua DPP bw Bwisalo ambaye leo kapewa ujaji ilihali alipaswa kuwa gerezani.
 
inabidi sasa nianze kutumia "Iron Dome"
kujikinga na MAJUNGU na FITINA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…