Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Wanasiasa..
1. Hapi (Iringa
2. Mmiliki wa Gwambina na Mbungwe Misungwi (Nimesahau Jina lake)
3.Mkuu wa Mkoa wa Iringa


Voingozi wa Taasisi

1. Mkurungezi wa Benki ya Kilimo (Tadb) anaitwa Japhet
2.Mkurugenzi wa TPA (Tayari huyu ushamuondoa)


List ni ndefu mama ngoja watu wengine waongeze majina..... kwa ufupi hawa ni wanawanyanyasa saana watanzania katika nafasi zao na mbaya saana walikuwa wanakudharau saana wewe kwa nafasi yako ya Umakamu enzi za mwenda zake
 
ili afanye kazi kwa uhuru,na tupate sababu za msingi kumlalamikia akiharibu.

inabidi atoe watu wote anaohisi walikuwa wa mwendazake watamkwamisha.
 
Wakiondolewa hao utakuwa na maisha Bora sana.
 
Jafetii ana shida gani?
Huyu ni Dictator mwingine kama alivyokuwa mwendazake...Kawaariba maisha waliokuwa wafanyakazi wa benki hiyo kwa kufukuza bila sababu za msingi na wengine kuwabambikia kesi Takukuru walipogoma kujiuzuru pale alipokuwa hataki kufanya nao kazi....Yeye na Mkurugenzi wa TIB (iliyoungana na TPB sasa) ndio wakurugenzi pekee ambao mpaka leo hawajapata Vetting ya BoT lakini wanakalia viti vyao (hutakiwi kuwa mkurugenzi wa Benki kama huna vetting ya BoT)
 
Kuna mdau alishauri Amuondoe na makonda, hata kama hana cheo amuondoe tuu.
 
Angalia Majungu mengine haya ukiuliza toa sababu huna zaidi ya kumsikia Kigogo,Jaruo, na Karume mtoto wamesema πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 


Walitenguliwa Kina Kitwanga na Lugola sembuse huyu SabayaπŸ™„πŸ™„πŸ™„ Kama kuteuliwa kupo kutenguliwa nako kupo vilevile

Kazi iendelee
 
Ole Sabaya ni mhuni, kibaka na jambazi kama majambzi wengine. Hapa lazima SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE ili Viongozi wanopenda kujimwambafy wajue kwa hakika CHEO NI DHAMANA.....!!!
 
Amemsimamisha kupisha uchunguzi, hajamfukuza kazi. Kuna ubaya kuchunguza tuhuma za kiongozi wa umma? Unadhani Rais hana vyanzo vyake vya taarifa?
Boma ng'ombe hatujalala kuhusu kupisha uchunguzi sasa atakapopanda Karandinga huyo Ole sabaya itakuwa sherehe Nchi nzima au akaungane na mwenda zake tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…