Rais Samia amtembelea Mzee Warioba. Je, Katiba Mpya kupata kiki?

Mama kaenda kumpiga Mkwara kiutu uzima
 
Kaenda kuweka handbrake wazee wasipige kelele kuhusu katiba mpya.

Kwenye swala la katiba mpya mh nadhani alikuwapo bungeni na alishiriki mijadala mbali mbali na anafahamu nini warioba ali address toka kwa wananchi
 
Hao wazee wasipokuwa wanafiki wakamwambia ukweli, wazo la katiba mpya litamsaidia aonekane shujaa kwataifa. Hilo litamfanya atengwe na inzi wa kijani. Akikataliwa ccm aende upinzani akagombee huko, na atapokelewa japo kwa masharti.
Nawajua wote hao wako straight kama rula na wanazeeka na misimamo yao. Muongeze hapo na Mzee Msekwa.
 
Katiba mpya hawezi kubali sababu itakuwa mwisho wake maana wananchi huku hawataki hata kumsikia kabisa
😁😁😁😁 jf bwana!

kila mmoja akijishibia kande na kujisikia tu kuongea basi huyo anafika na kubwabwaja
 
Anaenda kuwajulia hali si kupata maoni yao. Huwezi kumtembelea mtu lisaa limoja ukapata mawazo yake. Angekuwa serious kupata maoni angewaita ikulu na kufanya nao mikutano siku nzima.
Kwa mtu aliyejipanga maoni ya msingi unayapata ndani ya nusu saa. Ikizidi hapo ni kujirudirudia tu.
 
Hao wazee wasipokuwa wanafiki wakamwambia ukweli, wazo la katiba mpya litamsaidia aonekane shujaa kwataifa. Hilo litamfanya atengwe na inzi wa kijani. Akikataliwa ccm aende upinzani akagombee huko, na atapokelewa japo kwa masharti.
Atuachie kwanza nchi yetu halafu la katiba mpya lifuate. Hana huruma na wananchi. Bidhaa muhimu zote zimepanda bei!!

1 sukari
2. Mafuta ya kula
3. Vifurushi
4. Nondo
5. Cement
6. Mabati
7. Misumali
8. Rangi za nyumba
9. Chakula
10. Ugolo/ Tumbaku

Halafu wala hazumgumzii tatizo hili la mfumuko wa bei.
 
Lini sasa aichie nchi wakati kwanza ndio miezi 9 tu tangu aichukue. Labda muujiza utokee tena. Usiniulize muujiza gani nitakunasa kofi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…