Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Safi sana
Na upinzani tumkatae.
Yaani kotekote akataliwe.
Dr. Slaa alipinga suala la BANDARI si kwasababu ya uzalendo bali kwa kutafuta kiki za kisiasa, aluamini huenda 2025 atapewa nafasi ya kuwania Urais.
Angekuwa mzalendo angepinga ukatili wa Magufuli
Peleka ujinga wako huko ww nguruwe maji
 
Tujifunze kuheshimu maamuzi ya watu.
Nafikiri Slaa alifanya maamuzi sahihi kuliko hata Mbowe.

Angewezaje kukaa meza moja na Lowasa ambaye yeye alimtaja kuwa ni fisadi na eti anapewa ridhaa ya kugombea uraisi kupitia Chadema?

Slaa pekee ndiye alisimamia maneno yake aliyoyatamka
Kama ndivyo unavyoamini ilikuaje basi kupewa zawadi ya Ubalozi na aliyekuwa M/Kiti wa CCM Taifa wa wakati huo??? Watz siyo Wajinga.
 
Kumbe Rais Samia wa hovyo hivi? Kweli bado kuongoza nchi kwa nchi zetu hizi za kishenzi!
Kwa kosa lipi kafanya mpaka umvue ubalozi?

All in all ubalozi wenyewe ulikuwa wa shukrani baada ya usaliti kwa wapigania haki!
Nadhani msali ni yule aliyehongwa vipande vya fedha akaruhusu fisadi kugombea urais kupitia chama chao
 
Kama ndivyo unavyoamini ilikuaje basi kupewa zawadi ya Ubalozi na aliyekuwa M/Kiti wa CCM Taifa wa wakati huo??? Watz siyo Wajinga.
Unafahamu rais aliyepita alivyokuwa....angeweza kufanya hivyo kuwakomoa chadema
 
Adhabu hii haina nguvu yoyote sana sana imemu expose Sa100 kwa watu wenye akili timamu!
Mwanamke hata awe na mamlaka vp hawezi acha kisirani, pia ni mnafki alijinasibu yeye ni mcha Mungu na mpenda maridhiano kumbe sivyo alivyo moyoni.
Angempotezea Slaa kwa watu makini angeonekana ana ngozi ngumu kweli kwa yeye kama mwanasiasa ila kumbe ni mpenda kusifiwa na kwamba hata haya maujinga ya chawa wa mama huwa yanamfurahisha sana moyo.
Jinga kabisa!
Nimekupa like yangu , saa100 ni wa hovyo lakoni kwa kuwa media zetu zinaenjoy maisha na matajir wanaelea kwenye utsjiri ,wao hutasikia baya lolote kwa huyu kibwengo mkuu
 
DKt Wilbroad Slaa amevuliwa hadhi ya ubalozi kuanzia leo Septemba 1, 2023. Taarifa imetolewa hivi punde na Ikulu katika mtandao wa kijamii wa X ama Twitter.

Hayati Rais John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Willibroad Slaa ambaya ni Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Upinzani, CHADEMA kuwa Balozi mnamo Novemba 23, 2017

Julai 22, Dkt. Slaa alizungumza na Wananchi kupitia vyombo vya habari akisema ni kwa ajili ya kuelimisha wananchi kuhusu kasoro zilizopo kwenye mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.

Aliweka wazi kuwa hapingi uwekezaji katika bandari hiyo ya Dar es Salaam bali anapinga mkataba wa uwekezaji kwa kueleza kuwa hauna maslahi kwa Taifa.

Aidha, siku hiyo alisema “Najua maneno hayo ni makali… nimepokea vitisho na mimi pia sio tu Mawakili, wengine wakasema ubalozi wako tutachukua, nawaambia chukueni sasa hivi, siishi kwa ajili ya ubalozi. Nimesema sina chama najiamini najau ninachosimamia“

View attachment 2735983

=====
WILLIBROD PETER SLAA NI NANI?
View attachment 2735984
Dk Slaa alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1948 wilayani Karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965.

Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Ni kiongozi mwenye stashahada tatu pamoja na shahada ya Uzamivu (PhD). Anayo Shahada ya Uzamivu (PhD ) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo Kikuu cha St. Urban, Rome. Pia anastashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari, Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari, Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho.

Amewahi kuwa padri wa Kanisa Katoliki kuanzia mwaka 1977 hadi 1991, akishika nafasi za kiutawala katika kanisa pia. Amepata kuandika vitabu vitatu ambavyo ni Utimilifu wa Msichana (1977), Utimilifu wa Mvulana (1977) na Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981).

Ni mzungumzaji wa Lugha nane kwa ufasaha; ambazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.
Siku ya Alhamisi, Novemba 23, 2017 Aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alimteua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa balozi. Alikuwa Balozi wa Sweden, pia ailiidhinishwa kwa Nchi za Denmark, Finland, Norway, Iceland, Estonia, Latvia, Ukraine na Lithuania.

Kipindi Dk Slaa anateuliwa kuwa Balozi, alikuwa anaishi Canada, alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kumpitisha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa vyama vya siasa wa Ukawa.

Pia, soma: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa kuvuliwa ubalozi na kukamatwa!
Bora ili mafuta yashuke bei,nfumuko wa bei na dola ziongezeke mtaani, pia kuvuliwa ubalozi ccm wamejibu hoja za kugawa bandari zetu kwa mwarabu wa Dubai.
 
Kwa hiyo tunakubaliana kwamba huyu naye ana visasi kama yule mwingine maana yule mwingine mada ingekuwa hiyo.😁.

Balozi Ali Karume yeye atavuliwa lini hiyo hadhi?
 
Tujifunze kuheshimu maamuzi ya watu.
Nafikiri Slaa alifanya maamuzi sahihi kuliko hata Mbowe.

Angewezaje kukaa meza moja na Lowasa ambaye yeye alimtaja kuwa ni fisadi na eti anapewa ridhaa ya kugombea uraisi kupitia Chadema?

Slaa pekee ndiye alisimamia maneno yake aliyoyatamka
Mbowe ni mjesiriamali na mwenye uchu wa fedha kuliko ,aliamua liwalo na liwe ,slaa aliyesimamia msimamo wake eti ndo anaonekana msaliti watu wakiwaita wafuasi wa mbowe kuwa ni nyumbu wanakuwa wakali kama pilipili
 
Mvuaji akumbuke wapo waliovuliwa na mwendazake ,alipokuja yeye akawavalisha ,Yeye akiondoka Dr Slaa atavalishwa na mrithi wake.
 
Hii ni kawaida tu. Hata Alphayo Kidata kamishna wa sasa wa TRA aliwahi kuvuliwa hadi ya ubalozi na Rais aliyepita Mwendazake Magufuli. Sioni cha ajabu hapo.
 
Mbowe ni mjesiriamali na mwenye uchu wa fedha kuliko ,aliamua liwalo na liwe ,slaa aliyesimamia msimamo wake eti ndo anaonekana msaliti watu wakiwaita wafuasi wa mbowe kuwa ni nyumbu wanakuwa wakali kama pilipili
Niliwahi kusema kuwa ipo siku Slaa ataonekana ni shujaa kwa maamuzi ya kusimamia maneno yake
 
Mbowe ni mjesiriamali na mwenye uchu wa fedha kuliko ,aliamua liwalo na liwe ,slaa aliyesimamia msimamo wake eti ndo anaonekana msaliti watu wakiwaita wafuasi wa mbowe kuwa ni nyumbu wanakuwa wakali kama pilipili
Hayo ni mawazo yako. Lakini kwa upande mwingine ukweli unaujua.
 
Wewe akili yako hua inawaza upumbavu wa mambo ya kishirikina tu,chakusikitisha kuna wapuuzi hua wanakuona wa maana kwa kujaza issue za mambo yakusadikika humu,Dunia inaenda kwa kasi sana kwenye teknolojia ila wewe akili yako iliishia kuwaza upuuzi wa ushirikina tu.
umemtus bure.hiko alichoweka ndio walichosema hao wazee wanywa gahawa wa huko unguja mbele ya rais na waziri mkuu. tuanze kwanza kumsema rais wako na serikali yake na watu wa itifaki kwa kukenua na kuacha matamko ya kipumbavu kama hayo.
 
Back
Top Bottom