Rais Samia amwagiwa sifa kwenye Bunge la Ulaya

Nchi yetu ni taifa huru

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote
Taifa huru wakti hamuwezi kujitegemea wenyewe,budget ya kuendesha serikali mnategemea msaada...labda kujitegemea kwa porojo
 
Wewe upo Tz kweli au kuzimu?
Kama upo Tz umeandika uongo mtupu ILA kama upo kuzimu tena kwa miaka mingi upo sawa!
 
David McAllister akamamatwe mara moja na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi
 
Vipi kutembeza bakuli
 
Tatizo kubwa, wengi wenu hata hicho Kiingereza hamkijui vizuri, mnaenda mnaokota neno moja moja.

Hakuna mahali ambapo Samia amesifiwa, zaidi ya kueleza kuwa kwa baadhi ya mambo aliyoyafanya, yanaleta matumaini, japo bado kuna concern kubwa kwenye masuala ya haki na demokrasia.

Lakini pia ni uwongo wako binafsinkusema kwamba hakuna watu ambai wamewekwa ndani, na bado wapo ndani kwa sababu za kisiasa. Vuongozi na baadhi ya wapenzi wa CHADEMA, moaka sasa waliopo kwenye mahabusu za magereza, kwa nchi nzima, ni zaidi ya 100.

Taarifa ya Rita, hiyo ya kusema uongozi wa Samia umeketa matumanini, bado imepingwa kutokana na ushahidu mbalimbali, na wameambiwa watoe majibu ya uhkakika kuhusiana na matujio mbalimbali ambayo yameshuhudiwa na kuthibitishwa na balozi mbalimbali. Ufahamu kuwa McAllister siyo mbunge kama alivyo Rita. McAllister ni Mwenyekiti wa Foreign Affairs wa Bunge la Ulaya, na Rita na team yake walitumwa na McAllister. Ndiyo maana Rita ameagizwa na McAllister kutoa majibu kwa masuala mbalimbali ambayo inaonekana hawakuyafanyia kazi kikamilifu. Ja wameambiwa watoe mapendekezo kwa Bunge juu ya hatua za kuchukua dhidi ya utawala wa Samia, na sia business as usual.

Tusiwe wajinga wa kusifia mafanikio madogo au utendaji wa kinafiki wa Serikali ili kuwaridhisha critics wa kimataifa.
 
Nchi yetu ni taifa huru

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote
Utakuwa mpumba.vu, umemchoma moto mikono mtoto wako, wakija majirani kukuhoji, unajitetea kuwa mimi ni familia huru. Utakuwa mwendawazimu hasa.

Uhuru wa Taifa, kama ilivyo wa mtu mmoja mmoja, una mipaka yake. Ukienda nje ya mipaka, Dunia itakuhoji na inaweza kukuadhibu. Mpumb.avu pekee ndiye akihojiwa kwa uovu, atajibu kuwa sisi ni Taifa huru. Uhuru wa Taifa unaishia katika kuwatendea haki watu wako, na siyo uhuru wa kutenda uovu.
 
Mzungu akusifie kweliii?? Mungu wanguu
 

Mpumbavu atakua yule anayeita wengine wapumbavu ilihali hana analosaidia katika kuondoa tatizo analoliona zaidi ya kulalama na kutukana

Ningeuona mwerevu kama wewe ungekua chanzo cha kufanya mabadiliko kwenye kile unachoona kinahitaji kubadilishwa. Vinginevyo wewe ni wa kulialia na blahblah tuuuuuu

Wacha nikupe cheo cha mpumbavumkuu
 
KUTOKA MAKTABA
November 20, 2020

Balozi Nyamanga : Bunge la Umoja wa Ulaya Halijatoa Azimio lolote Kuhusu Tanzania​

Udaku SpecialNovember 20, 2020



Na Immaculate Makilika- MAELEZO
Serikali kupitia Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya imesema kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya halijatoa azimio lolote kuhusu Tanzania kupitia kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Bunge hilo.

Akizungumza mapema leo kupitia televisheni ya Taifa (TBC), Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya Jestus Nyamanga alisema kuwa kuna taarifa za upotoshaji na zisizo na ukweli wowote zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zikidai kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya jana Novemba 19 limeazimia kusitisha misaada na mikopo kutoka umoja huo na mashirika yake, kwa nchi ya Tanzania sambamba na kuiwekea vikwazo.


Halikadhalika taarifa hizo za upotoshaji zinadai kwamba Bunge hilo la Umoja wa Ulaya limeazimia kuiwekeza vikwazo Tanzania na kuzuia kuuza bidhaa zake katika nchi za Umoja wa Ulaya.


“Novemba 19 asubuhi hapa Ubeligiji, Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya ilikutana katika kikao chake cha kawaida, moja ya masuala yaliyojadiliwa ilihusu Tanzania na hali ilivyo baada ya Uchaguzi Mkuu kukamilika, huu ni utaratibu wa kawaida kabisa wa Kamati hiyo kuijadili nchi ambayo ni mdau wao mkubwa wa maendeleo mara tu baada ya Uchaguzi Mkuu kukamilika”, alisema Balozi Nyamanga


Balozi Nyamanga alifafanua kuwa kikao hicho ni kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na si Bunge lote na hata hivyo kikao hicho kilitoa nafasi kwa wabunge kutoa mawazo yao na kujadili kuhusu hali ya Tanzania baada ya Uchaguzi Mkuu ambapo ni wabunge watano tu ndio walitoa mawazo yao kati ya wabunge 71 wa Kamati hiyo. Ambapo hilo lina idadi ya wabunge 705 na hivyo halijatoa azimio lolote kuhusu Tanzania.


Alibainisha kuwa pia kuna taarifa ambazo si za kweli zinazoenezwa na watu wenye nia mbaya na Tanzania zikidai kwamba Bunge hilo la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania msaada wa euro milioni 626 ambazo Tanzania inapewa na Umoja wa Ulaya kila mwaka, si kweli kwamba Umoja huo unaipa Tanzania fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi. Aidha Serikali inaendelea kutekeleza miradi yake mbalimbali.


“Hakuna mjadala wala majadiliano yanayoendelea katika Umoja wa Ulaya wala hakuna azimio lililowekwa na Kamati hiyo ya Bunge, wala kuizuia Tanzania kuuza bidhaa zake katika nchi hizo za Umoja wa Ulaya, hata hivyo naomba niwahakikishie watanzania wenzangu kwamba uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya ni mzuri sana kwa zaidi ya miaka 45 sasa na tunaendelea kushirikiana katika masula mbalimbali yanayohusu maendeleo kwa pande zote mbili”, alisema Balozi Nyamanga.
Mwisho

N.B
 
Ukiona mizungu inakusifia jua ......
 
Toka maktaba :

21 November 2020

KUMEKUCHA.!. PROFESA KABUDI AWAJIBU MABEBERU,TANZANIA HAIJAWAHI KUPIGA MAGOTI



Source : millard ayo

Zaidi Toka maktaba miaka 3 iliyopita

Hatuwezi kupiga magoti kuomba misaada- Prof. Kabudi​

3 years ago Hatuwezi kupiga magoti kuomba misaada- Prof. Kabudi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa Tanzania haikupiga magoti katika kipindi cha utawala wa awamu ya pili ilipokuwa na hali ngumu, hivyo haiwezi kufanya hivyo wakati huu ikiwa na hali nzuri zaidi.

Amesema kuwa licha ya nchi kutokuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni wakati huo wa awamu ya pili (1985-1995), Tanzania haikupiga magoti kuomba msaada, lakini sasa Taifa lina akiba ya fedha za kigeni za miezi mitano
“Kama tuliweza kwa wakati huo hatuwezi kushindwa katika awamu hii ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, tumeamua kujitegemea na hili tunalitekeleza kikamilifu kwamba hatuwezi kupiga magoti kwaajili ya kuomba misaada.”amesema Prof. Kabudi
Profesa Kabudi aliyasema hayo Bunge jijini Dodoma alipokuwa akijibu hoja za Wabunge waliochangia mjadala wa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020
 
Rita Laranjinha sio mbunge wa EU
 
Weka speech yote acha kuhadaa watu hapa.. Ameanza kusifu lakini kazungumzia demokrasia inavyo banwa.
 
Mungu wabariki Wazungu
 
03 December 2021

Wananchi wavutiwa na msimamo wa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Ulaya


Wananchi watoa maoni kufuatia Kamati ya Bunge la Ulaya ya Masuala ya Nje, kudai hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya serikali ya Tanzania baada ya njia za majadiliano na ushawishi kugonga mwamba na kushindwa kuifanya serikali ya CCM kujisahihisha makosa yake ya utawala bora, kuminya demokrasia na kuumiza utu wa raia wake.


Source : BONGOTIMES TV
 
Nimesikiliza na kutizama Video, nimegundua mtoa thread hapo juu ni Mnafiki wa kiwango Cha Rami, ni sawa na muuaji!
 
Nimesikiliza na kutizama Video, nimegundua mtoa thread hapo juu ni Mnafiki wa kiwango Cha Rami, ni sawa na muuaji!

Kweli kabisa kuna nia ovu ya kupotosha umma mpana wa raia wa Tanzania kwa makusudi kabisa.

Si bure wazalendo uchwara wa CCM kufanya makusudi waTanzania wasielewe au kufundishwa lugha ya kigeni ili tubaki tusifahamu ukweli, kujifunza au kupata maarifa.

Hii kampeni ya kuenzi lugha ya Kiswahili kusudio lake kubwa ni kuacha ombwe la ufahamu ili waendelee kututawala na pia kujaribu kuwazuia wadau wa maendeleo kutofahamu kinachoendelea nchini.


Tujiulize kwanini nchi ya Tanzania inayotambua lugha rasmi mbili yaani ya Kiswahili na Kiingereza, vipi hatuna idhaa yoyote ya serikali au binafsi inayorusha matangazo, mijadala, midahalo, entertainment, michezo kwa lugha ya Kiingereza ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…