Rais Samia amwalika Rais Kenyatta kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 60 za Uhuru wa Tanzania

Katika kasoro zote za muungano hili la Tanganyika kutokuwa na kiongozi tumebugi,inakuwaje Mzanzibari awaongoze Watanganyika katika sherehe za uhuru wao wakati yeye sio Mtanganyika?
Hata Hivyo Huyu Kafika Hapo Kwa Emergency Tu Wala Hakutarajia Kabisa. Najiuliza Hivi Uwaga Wakikutana Rais Wa JMT na Rais Wa BMZ Uwaga wanaongea Nn?
 
Katika kasoro zote za muungano hili la Tanganyika kutokuwa na kiongozi tumebugi,inakuwaje Mzanzibari awaongoze Watanganyika katika sherehe za uhuru wao wakati yeye sio Mtanganyika?
Unaambiwa anakuja Uhuru Kenyatta
 
Rais Samia amesema amemuomba Rais Uhuru Kenyata wa Kenya kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania hapi tarehe 09/12/2021.

Rais Kenyatta amekubali ombi hilo.

===

Rais Samia Suluhu: Mwisho ni kwa taarifa yenu waandishi wa habari, mwaka huu ifikapo mwezi December, Tanzania tunatimiza miaka 60 ya uhuru wetu na hivyo nimetoa mwaliko rasmi kwa Rais Uhuru Kenyatta awe mgeni rasmi katika maadhimisho yale ya miaka 60 ya uhuru wetu.

Kazi Iendelee!
Hatuna rais.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Yani kamwalika Rais wa Kenya awe mgeni rasmi (the most important guest at an occasion) kwenye Sherehe ya Uhuru wa Tanganyika?? Hii protokali imeanza lini ndugu zangu😳😳😳
Imeanza leo,
kwani shida Nini? Kila Jambo Lina mwanzo usihofu anzisha mwendo wengine watafuata..
 
Wakati Wajumbe Wa CCM Wanataka Hayati Magufuli aongezewe mda ulihoji Kama Hatafika Huo Mwaka.
kwa sababu walitaka Magufuli aongezewe muda, ushaelewa?

Huyo rais Hassan asipokuwapo December, mualiko kwa rais Kenyatta haukomi kwa sababu yeye hayupo.
Mualiko umetolewa kitaasisi, haujatolewa kibinafsi.

Ila ugombea urais wa Magufuli ulikuwa wake Magufuli, hakuna John Pombe Magufuli yuleyule mwingine wa kugombea urais baada ya John Pombe Magufuli kufariki.

Hapo utaona, kuhoji habari za kumuongezea mtu muhula wa urais miaka mitano ijayo ni jambo linaloweza kuhojiwa kwa msingi wa "mna uhakika gani atakuwepo?"

Lakini mualiko wa rais Hassan kwa rais Kenyatta December hauwezi kuhojiwa kwa msingi wa "mna uhakika rais Hassan atakuwepo?".

Kwa sababu hata asipokuwepo, kutakuwa na rais mwingine.

Umelinganisha mambo ambayo hayana muunganiko wa moja kwa moja kimantiki.
 
Mkuu naomba maoni yako kuhusu rais wa nchi A kuwa mgeni rasmi wa nchi B ilhali rais wa nchi B yupo. Imekaaje sawa hii kiitifaki?
 
Tuache makelele, kiprotocall huwezi toa kila kitu mlichozungumza hadharani. Hicho cha kumwalika kilikuwa cha kutoa hadharani period. Huu ni mwanzoa mzuri.
 
kwa sababu walitaka Magufuli aongezewe muda, ushaelewa?

Huyo rais Hassan asipokuwapo December, mualiko kwa rais Kenyatta haukomi kwa sababu yeye hayupo.
Mualiko umetolewa kitaasisi, haujatolewa kibinafsi.

Ila ugombea urais wa Magufuli ulikuwa wake Magufuli, hakuna John Pombe Magufuli yuleyule mwingine wa kugombea urais baada ya John Pombe Magufuli kufariki.

Hapo utaona, kuhoji habari za kumuongezea mtu muhula wa urais miaka mitano ijayo ni jambo linaloweza kuhojiwa kwa msingi wa "mna uhakika gani atakuwepo?"

Lakini mualiko wa rais Hassan kwa rais Kenyatta December hauwezi kuhojiwa kwa msingi wa "mna uhakika rais Hassan atakuwepo?".

Kwa sababu hata asipokuwepo, kutakuwa na rais mwingine.

Umelinganisha mambo ambayo hayana muunganiko wa moja kwa moja kimantiki.
Hatusimami kuplan kwa sababu eti tutakufa, watu waache woga. Mwendazake kaenda kwa style yake wengine Mola anajua siku ya kufa.
 
Mkuu naomba maoni yako kuhusu rais wa nchi A kuwa mgeni rasmi wa nchi B ilhali rais wa nchi B yupo. Imekaaje sawa hii kiitifaki?
Si lazima rais awe mgeni rasmi katika kila hafla, na si tu rais wa nchi A anaweza kuwa mgeni rasmi katika hafla ya nchi B wakati rais wa nchi B yupo, katika scenario nyingine unaweza kukuta rais wa nchi A na wa nchi B wapo katika hafla ambayo mgeni rasmi ni mtu mwingine tu, pengine raia tu, wa nchi A, B au hata C.

Mimi napenda kujadii kw amifano.

Wakati wa vita vikuu vya pili, Princess Martha wa Norway alikimbilia USA kuwa mkimbizi. Akakaa karibu sana na rais Roosevelt.

Katika moja ya jitihada zake za ku mobilize Marekani iisaidie Norway, Princess Martha aliitisha kikao maalum. Kabla ya kikao, akamuomba radhi rais Roosevelt kwamba katika kikao hicho rais hatakuwa mgeni rasmi, ila mgeni rasmi atakuwa baharia wa jeshi la majini la Norway aliyepata kilema kutokana na kuipigania nchi yake. Baharia yule akasema kwa uchungu sana kuiomba Marekani iisaidie Norway kupata silaha kupigana na Hitler.

Hapo utaona Princess Martha wa Norway hakuwa mgeni rasmi, rais Roosevelt wa Marekani hakuwa mgeni rasmi.

Mgeni rasmi alikuwa baharia kilema wa Norway.
 
Hatusimami kuplan kwa sababu eti tutakufa, watu waache woga. Mwendazake kaenda kwa style yake wengine Mola anajua siku ya kufa.
Ku plan tulishaplan tukaweka ukomo wa urais wa miaka 10.

Zaidi ya hapo ni kujimwambafy tu.
 
Back
Top Bottom