Rais Samia amwalika Rais Kenyatta kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 60 za Uhuru wa Tanzania

Rais Samia amwalika Rais Kenyatta kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 60 za Uhuru wa Tanzania

Yani kamwalika Rais wa Kenya awe mgeni rasmi (the most important guest at an occasion) kwenye Sherehe ya Uhuru wa Tanganyika?? Hii protokali imeanza lini ndugu zangu😳😳😳😳
Ndiyo inaanza sasa elewa hivyo. Diplomasia haiko static bali ni dynamic
 
Tanzania haijawahi kupata uhuru kwa kuwa haijawahi kutawaliwa. Kuna uhuru wa Tanganyika tu wakati Tanzania ina muungano peke yake.

Kwa upande mwingine, Zanzibar ilipata uhuru Desemba 10, 1963 ila SMZ haisherehekei isipokuwa siku ya mapinduzi ya Januari 12, 1964
Rais Samia amesema amemuomba Rais Uhuru Kenyata wa Kenya kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania hapi tarehe 09/12/2021.

Rais Kenyatta amekubali ombi hilo.

===

Rais Samia Suluhu: Mwisho ni kwa taarifa yenu waandishi wa habari, mwaka huu ifikapo mwezi December, Tanzania tunatimiza miaka 60 ya uhuru wetu na hivyo nimetoa mwaliko rasmi kwa Rais Uhuru Kenyatta awe mgeni rasmi katika maadhimisho yale ya miaka 60 ya uhuru wetu.

Kazi Iendelee!
 
Hata Hivyo Huyu Kafika Hapo Kwa Emergency Tu Wala Hakutarajia Kabisa. Najiuliza Hivi Uwaga Wakikutana Rais Wa JMT na Rais Wa BMZ Uwaga wanaongea Nn?
Sio kwa dharura,kwa mipango ya mungu
 
Hatuna rais.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Kosa la uhaini Kama ukijulikana,ilitakiwa useme hivyo wakati magufuli kafariki na Samia hajaapishwa.
Uwe Makini katika kuandika,hii sentesi yako yaweza kukufikisha mahali pabaya usipotarajia Kama wakiamua kukufuatilia,huwezi jificha Kama unatumia mtandao.
Hata melo mwenyewe kwa comment Kama hii hawezi kukuficha Kama wenye mamlaka wakitaka mawasiliano yako.
 
Yani kamwalika Rais wa Kenya awe mgeni rasmi (the most important guest at an occasion) kwenye Sherehe ya Uhuru wa Tanganyika?? Hii protokali imeanza lini ndugu zangu[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
Dah...hata Nani nimeshtuka Sana,[emoji2960]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanzo mzuri wa kukua kwa diplomasia ya Tanzania iliyokuwa imefikia kwango cha chini kabisa (2015-20) kuliko wakati wowote tangu uhuru! Liberata Mulamula kazini!
Mmmh watu wengine sijui huwa mna matatizo gani?!? Una umri gani wewe? Diplomasia yetu imekuwa nzuri kabisa...ungekuwepo 1977 Hadi 1985 pengine usingeandika haya...hovyo kabisa...
 
Kosa la uhaini Kama ukijulikana,ilitakiwa useme hivyo wakati magufuli kafariki na Samia hajaapishwa.
Uwe Makini katika kuandika,hii sentesi yako yaweza kukufikisha mahali pabaya usipotarajia Kama wakiamua kukufuatilia,huwezi jificha Kama unatumia mtandao.
Hata melo mwenyewe kwa comment Kama hii hawezi kukuficha Kama wenye mamlaka wakitaka mawasiliano yako.
Labda yupo nje ya nchi Kama Lema na Tundu
 
Mwanzo mzuri wa kukua kwa diplomasia ya Tanzania iliyokuwa imefikia kwango cha chini kabisa (2015-20) kuliko wakati wowote tangu uhuru! Liberata Mulamula kazini!
mlikuwa mnaipimaje kama imeshuka!!!??
 
mlikuwa mnaipimaje kama imeshuka!!!??
... huwezi kusimama hadharani kutukana wengine ukasema kuna mahusiano mazuri! Fuatilia kipindi chote cha Rais Samia kama utasikia tusi lolote kwa nchi au mwananchi yeyote wa kigeni. Kama kutakuwa na kuhitilafiana (which is normal) mambo yatamalizwa diplomatically.
 
diplomasia sio unafiki bali ni ushirikiano wa kweli baina yenu.

tz haijawahi kuwa na kinyongo na nchi yoyote,shida ni pale tulipoanza kupangiana mambo binafsi.mama mwenyewe tayari kashaanza kuonyesha jeuri,tofauti yake na mwendazake yeye ana kifua tu.
 
... "... ana kifua .." sifa muhimu sana ya diplomat! Kutukanatukana mataifa na raia wa kigeni sio diplomasia ni ushamba na ukosefu wa weledi wa kidiplomasia. By the way, unaonekana mwehu tu!
 
Back
Top Bottom