Rais Samia anafanya kweli. Mashirika ya Umma kuwa ya Umma kiukweli

Ukiua shirika ukienda kwake naye anakuua
Duh kumbe hivo
 
Kwa hili nipo pamoja na mama, na hatajutia kumtumia Mchechu kwa nafasi aliyempa. Alifanya vizuri kule NHC japo Magu alimtungua kwa sababu hakupeleka miradi ya NHC Chatu bali alikomaa na mijengo ya town. Ila atakae koroga anyongwe kweli na mapema, sio kusubiri mpaka shirika lifa nae
 
Tulijua tu ni mbinu ya kuachia uchumi wa nchi mikononi kwa wahuni. Hivi shirika kama TPDC ni kampuni ya biashara au ni shirika la serikali la usimamizi na kuendeleza mambo ya mafuta. Serikali inaliachia ili iweje. Mali za umma chini ya shirika inakuaje? Vyuo vya umma vinaachiwa ili iweje. Je navyo ni makampuni ya biashara. Hivi hii serikali inayotaka kugawa kila kitu tutaweza kuiacha hadi uchaguzi 2025?..Siwatakua wamegawana mali zote za nchi hii?
Yaani mama kwa uhakika ni janga . Bila shaka maadui wanafanya kazi kwa spidi kali kuitwaa nchi kipindi hiki cha mama.
 
Mnapenda sana porojo
 
Bandari zetu zitaendelea kuwa za umma au za DPw bila kikomo kwa kadri ya IGA?Tuanzie hapo kwanza manake naona tunachanganyana sasa!
 
Duuuuh kweli waraka wa TEC ni balaa .
Leo FaizaFoxy kadata Hadi anaandika kikongo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mleta Uzi hicho ulichoandika ndo mlivyofundishwa huko shuleni kwenu πŸ§‘β€πŸ¦½πŸ§‘β€πŸ¦½
Anajiitaga pedagogist at heart kumbe tapeli kweli kweli
 
Watanzania wauziwe hisa na wawe na kauli nayo.
Huu utakuwa ni wizi mwingine mchana kweupe!! "watanzania " mabepari wanaenda kupewa ulaji!! hayatakuwa ya umma tena bali yatamilikiwa na "watanzania mabepari" na hao watakuwa na sauti nayo!! Msechu ni mtanzania bepari!! huu ukweli lazima osemwe. Lakini pia mabepari wa nje watawatumia watanzania vibaraka kama mawakala wa kumiliki mashirika ya umma kupitia hisa zao!! TUKATAE watu binafsi kumiliki hisa kwenye mashirika ya umma yanayofanya vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…