Tanzania sasa inapata Uwekezaji kila kukicha na kutoka kila Taifa na ndio maana kwa uhodari na utaalamu wake mkubwa wa kuzifanya Siasa za Kimataifa, Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EC) imeamua kuipa Tanzania Fedha za Msaada kabisa na za bure Takribani Trilioni 1.15 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa namna Rais Samia alivyo hodari na anavyojua kushawishi Mataifa kuja nchini kuwekeza na namna Uwekezaji mkubwa unavyozidi kuingia nchini, Nchi hii itapata mafanikio makubwa sana kimaendeleo, uchumi na uwekezaji. Mpaka sasa kwa muda mfupi wa Miezi 11, Tanzania imeshuhudia Uwekezaji mkubwa kuingia nchini ambao haukuwahi kutokea. Zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 3.5 zimeingia nchini kuwekeza kwenye miradi zaidi ya 90 kwa muda huu tu mfupi wa uongozi wake. Eneo la Diplomasia ya Uchumi ni eneo muhimu sana kwa maendeleo ya Nchi yetu na Rais Samia amelipa nguvu kubwa sana kupitia mashirikiano haya na Mataifa mengine. Linalipa.
Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com