Pre GE2025 Rais Samia anamtengeneza Mrema wake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Enzi za utawala wa Mzee Ruksa bila kujua athari zake alimwachie Late Mrema madaraka makubwa kupitiliza.

Awamu ya Sita namwona Mama akirejea makosa yale yale ya kumwachia maradaka makubwa Bashite.

Nimekaa pale nawaangalia taratibu.Anachofanya Bashite ni kujijenga yeye binafsi na si chama.Ipo siku watajua hawajua kumrejesha Joka kwenye chupa itakuwa vigumu sana.
 
Enzi za utawala wa Mzee Ruksa bila kujua athari zake alimwachie Late Mrema madaraka makubwa kupitiliza...
Kuna siku Mrema alivunja itifaki akaingia uwanja wa taifa kwenye sherehe wakati Mwinyi tayari yuko uwanjani.

Mlipuko wa umma kumshangilia Mrema ulimshitua Mwinyi akaamua kumpeleka wizara ya kazi.

Yaliyofuata baada ya hapo ni somo zuri la historia.

Bashite na Mrema wanashabihishwa na elimu zao.
 
Nadhani wanasiasa kutokea Zanzibar wanatabia za mfanano.
 
Chama changu hebu Katibu mkuu ukae chini na wenzio mjiulize haya yote anayoyafanya na kuyaibua si ni aibu kwa Chama kinachojinasibu kimeshughulikia wananchi wake?

Mbona Sasa kila anaconda Kuna matatizo matupu na dhuluma na ufisadi mtupu Serikali iko wapi na hizo wanasema Imani za Chama iko wapi.

Ni malalamiko kila kona ya nchi. Hivi Hawa Mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa Mikoa na wa Wilaya wapo hawayaoni haya yanavyotokelezea.

CCM shame shame shameful!
Xxxxx
 
 
Kaamua kumuacha Meneja wa Mkoa,maana ukweli anaujua,UMEME hautoshi..

Makonda acha janja janja..kiini cha TATIZO unakifahamu
 
Pitia hapo Mkuu, hicho unachokisema na mimi pia nilishakiona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…