Rais Samia anamuakisi Mzee Jakaya Kikwete kiuongozi na kiutendaji

Rais Samia anamuakisi Mzee Jakaya Kikwete kiuongozi na kiutendaji

Ila na nyinyi wafuasi wa magufuri munataka kuzidi gubu kila saa magufuri sasa hata kama mtamkumbuka kwa mema itasaidia nn? ya kwamba atafufuka aje kufanya haya unayo lalamikia?

Yaani sasa hivi akija mgeni kutoka nje ya nchi akasoma maoni ya wafuasi wa magufuri ndani ya jf anaweza kudhani labda kipindi cha uongozi wake Tz ilikuwa zaidi ya Qatar au Marekani.


Huyu mama anaweza kuwa ana matatizo lakini msitumie mapungufu yake kumpa JPM sifa ambazo saa nyingine hasitaili, Magufuri katuharibia mfumo wa uchumi wetu.

Kati ya maraisi bora kuwahi kulitawala taifa hili basi ni Mkapa na Kikwete maana wao walijenga mfumo imara wa kiuchumi na unao jiendesha lakini alipo kuja huyo shijaa wenu akauvuruga kwa kudhani uchumi unaendeshwa kwa bunduki na vitisho.

Baada ya kuuvuruga huo mfumo wa kiuchumi ulio anzishwa na Mkapa na Kikwete ,serikali ilianza kukosa kodi mpaka akanza kupora pesa kwenye akaunti za watu ili apate pesa za kuendeshea serikali yake.
Na baada ya kubaini amelikoroga ndipo alianza kiwakumbatia tena wafanya biashara ambao mwanzo alikuwa anawaita mafisadi mfano ni Rostam Azizi, na matajiri wa GSM.

JPM alitembelea kwenye nyota ya kikwete maana hata uwo umeme unao sema ulikuwa haukatiki vyanzo vya uwo umeme vime jegwa na Kikwete.

Hata mapato makubwa mlio kuwa mnamsifu kuyakusanya alikuwa anayakusanya kwenye uchumi uliojegwa na Kikwete.

Una zidhihaka safari za nje za Jk lakini hizo safari za nje ndo ziliwezesha kupata fedha ambazo zilianzisha mradi wa REA ambao umekusambazia umeme mpaka kijiji chenu.

Tuje kwenye bidhaa maana hapo ndo kichaka chenu.

JPM kaingia madarakani sukari ili ni sh1800 mpaka anaondoka bei ya sukari ilikuwa ni sh300.

Kakuta bei ya siment ni sh1200 kaondoka ikwa na sh19500 mpaka sh20000

Kakuta mafuta ya kula yakiwa bei chini lakini mpaka anaondoka bei ya mafuta ikuwa imepanda mara mbili ya alivyo yakuta.

Huyu mama ana matatizo yake tena makubwa tu lakini tumkosoe yeye kama yeye, mambo ya sijui angekuwepo magufuri lingefanyika hili na lile kuyaache maana ni kuendekeza upumbavu ndani ya vichwa vyetu.

Wtz tupambane kutatua matatizo yetu hili neno Magufuri tuliache maana kwa sasa hana tena msaada wowote kwetu kwa maana kesha kufa, hata ikitokea akafufuka bado hata kuwa na msaada kwetu kwa sababu amesha poteza mamlaka yake.

Mwisho kabisa Tz kwa sasa haihitaji raisi aina ya Magufuri ,bali Tz inahitaji raisi muwajibikaji na anaye tumia akili kuendesha nchi na sio kutumia nguvu na vitisho.
 
Nimenukuu

Hebu litazameni, nenden mkalitazame. HUYU SIO KIONGOZI!

JPM atakumbukwa daima.
 
Ni mfumo asilia; kila baada ya uongozi wa conservatives hufuatia liberals.

Maisha ya aina moja huchosha na kukinai, hivyo kubadilibadili huko kunaifanya CCM iendelee kutawala kwa muda mrefu.

Baada ya hawa liberals na mafisadi atatokea Rais mzalendo na conservative.

Tuupe muda nafasi.
 
TAIFA halina muelekeo kama ilivyokua wakati wa JK.

Umeme ,Maji imekua shidaaaa kama ilivyokua wakati wa JK.

Ufisadi umerudi Kwa Kasi kama ilivyokua wakati wa JK .

Mfumuko mkubwa wa gharama za Maisha kama ilivyokua Kwa JK .

Ajira zimerudi kua za Unandugu ? Kama ilivyokua Kwa JK.
Kwa sasa ni kama mzee wa msoga ndie yupo madarakani!
Kama ilivyokuwa kwa awamu yake na awamu hii ndio kabisaa tunaelekea kaburini!
Mikataba michafu ya kiwizi, upigaji wa kutisha wa "seniors officers", utapeli na udalali
 
Kumhitaji shetani akuongoze au kuwa na hamu ya kuongozwa na mtu mwenye tabia kama za shetani, ni lazima na wewe uwe shetani mdogo.

Yawezekana Rais Samia na Kikwete wakawa na mapungufu kiuongozi lakini kwa vyovyote ni bora maradufu kumzidi dikteta Magufuli.

Hivi kweli unaweza kutamani kuongozwa na muuaji kama wewe
mwenyewe siyo muuaji?

Hivi kweli unaweza kutamani kuongozwa na mumiani anayewapoteza watu wanahoji ushetani wake, kama na wewe si miongoni mwa hao wapotezaji?

Utatamani vipi kuongozwa na kiongozi mwizi wa fedha za umma 2.4 trilioni, mporaji wa fedha za aliowabambikia kesi za ubujumu uchumi, kama wewe si miongoni mwa wanufaika wa huo wizi?

Utatamani vipi uongozwe na mtu aliyeharibu ukuaji wa uwekezaji toka 28% mpaka 4%; utalii toka 15% mpaka 3.6%, thamani ya mauzo akayaporomosha kwa 50%.

Lazima uwe kichaa, punguani au mfuasi wa shetani kuweza kuutamani utawala wa Magufuli.

Sisemi Rais Samia na Kikwete have been the best presidents, lakini kwa ujumla kuwalinganisha naMagufuli, wataonekana ni malaika.

Magufuli was the worst president the country had ever got. Hakuwa na quality yoyote ya uongozi. Upole wa Watanzania ulisaidia sana, vinginevyo maafa makubwa yangeweza kutokea kama ingekuwa ni nchi ambayo haiwezi kuvumilia kuwa na kiongozi mwovu. Alikuwa shetani; muuaji, mporaji wa fesha za watu na haki za watu, mbaguzi ambaye hakujua hata maana ya tunu za Taifa letu, aliyeongoza kwa hadaa na uwongo, akiwapofusha akili waliokuwa wajinga, ambao wengi wao mpaka leo wanamsifia.

Athari za uongozi mbaya wa Magufuli zitaendelea kuonekana kwa miaka kadhaa, hasa katika kujenga jamii ya watu wenye haki sawa.

Ingawa hata tawala zilizotangulia zilishindwa kujenga Taifa lenye demokrasia, haki na uhuru wa maoni wenye utimilifu wa 100%, lakini kulikuwa na uafadhali. Magufuli akaja akaharibu kabisa.

Tunamwomba, na maombi yetu tunashukuru Mungu anayasikia daima, kamwe isitokee tena katika Taifa letu kuwa na mtawala mbaya kama Magufuli. Kuja kwa Magufuli katika uongozi kumetusaidia kujua kiongozi mbaya anakuwaje, na anaweza kulirudisha nyuma Taifa na kupoteza ndoto za walio wengi kwa kiasi gani.
 
Wameanza kukiri wenyewe bila shuruti kuwa nchi inaongozwa na mbumbumbu
 
Back
Top Bottom