Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
RAIS SAMIA ANAONYESHA UTAWALA BORA KWA VITENDO.
Na Elius Ndabila
0768239284
Moderator ninakumbuka kuna mtu hapa jamii forum aliwahi kuuliza, nani anajua anakotupeleka Rais Samia? Ninaomba mtag andiko hili kwa kuwa Rais Samia anatupeleka sehemu yenye mwanga mkubwa wa Umoja wa Kitaifa.
Rais Samia katika safari yake ya Urais hataki mtu yeyote abaki nyuma. Anatamani Watanzania wote waende pamoja.
Hataki kuwabagua watu kwa itikadi za vyama wanavyotoka. Anataka kila mtu ashiriki katika kuliletea taifa maendeleo.
Kwa ujumla hapendi manung'uniko kutoka Kwa mtu yeyote. Anajitahidi kwa kila namna kusimamia misingi ya utawala bora.
Hataki kuparuana na kuonyesha ukubwa wa Cheo chake, bali anajitahidi kwa kila namna cheo chake cha Urais kuwa silaha ya kuwaunganisha Watanzania.
Kitendo anachofanya Cha kukutana na kuzungumza na viongozi wa vyama vya siasa ni jambo kubwa na la mfano. Maendeleo yoyote duniani yanaletwa na Watu ambao wako pamoja na wanazungumza lugha moja. Kazi ya kuleta maendeleo kwenye Taifa ambalo watu hawawezi kuzungumza pamoja lugha moja ni ngumu zaidi ya ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
Mhe Samia anatumia kila namna kuhakikisha Watanzania tunaenda pamoja na manung'uniko ya kila mtu anayasikiliza. Mwendelezo wa jana kuendelea kukutana viongozi wa vyama vya siasa ni kuendelea kulithibitishia Taifa na Dunia juu ya dhamira yake njema kwa Taifa.
Ninatambua wapo wanaoishi Kwa kutengeneza migogoro. Wapo ambao hawapendi mshikamano na ushirikiano, maana wao wanaishi Kwa matusi na migogoro. Hawa wachache hawawezi kufurahishwa na hiki anachofanya Mhe Rais.
Ushauri wangu, Wakati Rais anaendelea kuliunganisha Taifa juu, basi viongozi wengine ngazi za mikoa na Wilaya nao waendelee kuzungumza na makundi ya chini kwa yale yaliyochini ya uwezo wao. Tusisubirie kila jambo Rais aseme. Kwa kuwa tumeshaona nia basi hiyo ndiyo iwe njia ya wengine kufanya.
Hongera Mhe Rais. Taifa imara linategemea sana umoja na ushirikiano. Safari yako ya uongozi imeanza vizuri ndio maana kila mahali watu wamepona mioyo Yao. Changamoto ndogo zilizopo tunaamini zitaendelea kupungua siku hadi siku Kwa kuwa hata Mungu hakujenga Dunia siku Moja. Maendeleo ni hatua. Na kila hatua ina changamoto zake....