Rais Samia anashauriwa kutengua uteuzi wa Hassan Bomboko Haraka iwezekanavyo

Sioni tofauti yako na huyo DC unaemtuhumu..maelezo mengi bila kusema amefanya nini, unadhani wasomaji wako wote wanafahamu huyu bwana DC amefanya nini?
 
Pole kwa DC kukuharibia soko la dada powa. Naona umeguswa mnooo aisee!
 
Dunia inabadilika, sasaivi watu sio wajinga wajinga kama zamani..
 

Attachments

  • Screenshot_20240621-085601_Instagram.jpg
    451.4 KB · Views: 2
Msitake kutetea ujinga ukahaba mwisho ubungo
Hakuna mtu anaetetea ukahaba. Lakini huwezi kumaliza ukahaba kwa kuzunguka na maaskari na makamera mitaani eti unakamata makahaba. That is cheap popularity..

Serikali imeshindwa kutengeneza fursa za vijana kujiajiri au kuajiriwa, matokeo yake vijana wanaona rasilimali pekee waliyo nayo ni miili yao. Hata ukiwakamata unawapeleka wapi? Utawafunga? Halafu? Wakitoka wanarudi kwenye biashara yao maana hawana kingine cha kufanya!!
Leo ukikamata 50 kesho wanaingia wapya 100 kuziba hilo ombwe. Je wanaojiuza mitandaoni nao utawakamataje? Nonsense
 
Lakini Chalamila alipofanys upuuzi kama huu na kugharimu maisha ya mtu, mlikaa kimya.

Tatizo ni CCM
 
mdau na wewe mnunuzi nini mbona wa kinondoni naye anawadaka kila siku hamsemi aondolewe, ama kwa kuwa wa huko amegusa maslahi yenu? uklahaba na umalaya sio kazi watafute kazi za kufanya shenzi taipu
 
Kujiuza
Kuwa mchipuko
Kuuza pombe bar

Hizi sio kazi za MTU kufanya huyo DC Approach anayotumia haifai Ila anachofanya ni sahihi

Angewakamata kimya kimya na kuwajengea bweni au hosteli nje ya mji malaya wore ili wapewe counseling na therapy ya akili

Malaya Kama hao Jela au police sio sehemu yao maana hao ni victim.
 
Dada poa ni good girl ila walitakiwa wawakamate kimya kimya wengine wake za watu wa ndoa kabisa ila wapo umo ktk iyo biashara
 
Na ukimuweka jela malaya mmoja nyuma yake kuna watu watano wanaomtegemea nao utakuwa umewasababishia maisha magumu.
Uluchoongea kipo sahihi kazi ya umalaya mtu akishaianza baadae inageuka kuwa uraibu kama mtu anayetumia dawa za kulevya wanahitaji muda mrefu wa kupewa nasaha na kurudi kwenye hali ya kawaida.
Ni ngumu sana kumkamata changudoa/malaya kisha umlazimishe aende kufanya kazi kwa muhindi alipwe elfu 6 hawakubali hata kwa viboko maana wamezoea pesa nyingi za kupata kirahisi.
Fikiria Saudia pamoja na sheria kali kuhusu umalaya/kuzini na adhabu zao ni kali ambazo zinaweza kupelekea mtu kupoteza maisha lakini bado malaya wanaenda kufanya kazi ya kuuza miili yao kwa hiyo sio jambo jepesi kama anavyodhani huyo DC.
 
naunga mkono.
nawashangaa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa wanashangaaa tu. Safisheni biashara haramu ya ukahaba kwenye maeneo yenu.
biashara ya kuuza uchi ni kinyume na maadili yetu.
Huwezi kumfundisha mtu tabia nzuri.

Unajuaje kama Rais na yeye hajawahi kufanya ukahaba
 
Unajua kabla ya kuamua aina na njia za kutatua tatizo, ni lazima ufanye uchambuzi yakinifu wa tatizo (hasa the attributes) pamoja na ni kwa muda gani limekuwepo. Zaidi inabidi urudi kwenye ni hatua gani zilichukuliwa in the past kama ni chronic issues, ni hatua zipi zilifanikiwa, zipi zilifail na kwa nini. Hii itasaidia kutorudia makosa,kwa mfano approaches ya kuwakamata machagudoa ilianza zamani enzi za Mh Baba ya waziri wa mambo ya nje, ikaendelea kwa wakuu wa mikoa wengine lakini hawakuweza kufanikiwa. Leo mkuu wa wilaya kurudia the same approaches using the same people (POLICE) It wont work at all and will never work. Kuna hitaji la kurudi kwenye drawing board kabla ya kukurupuka na mihemuko.

Ila lazima tujue kuna problems ambazo root cause zake ni mtambuka na ni ngumu sana kuziaddress hasa ukiwa na viongozi wa aina ya tulionao, some emaciate from level of education, socio-economic status, community social norms and perception about that behavior or things. Sasa Ku address hizi construct sio mchezo, zinahitaji long term commitment.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…