benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu imeandika historia mkoani Kigoma ambapo
imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 567 kwa ajili ya miradi tisa ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 420 kwa kiwango cha lami mkoani humo.
Ujenzi wa barabara hizo zitawezesha mkoa huo kuunganishwa kwa barabara za kiwango cha lami na mikoa ya Tabora, Katavi na Rukwa pamoja na nchi za jirani za Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Burundi na hivyo kurahisisha shughul za usafiri na usafirishaji na hivyo kukuza uchumi wa mkoa huo na nchi kwa ujumla.
Meneja wa Wakala ya Barabara (TANROADS) mkoani Kigoma, Narcis Choma ameeleza hayo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya miradi inayotekelezwa na wakala hiyo kwa wanahabari waliofanya ziara mkoani humo ili kuona maendeleo ya miradi inayotekelezwa na serikali hususani ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja.
Choma alieleza kuwa hadi sasa zaidi ya kilometa 100 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na nyingine zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake.
Alitaka miradi hiyo ukiwemo wa ujenzi wa barabara ya Kazilambwa (Tabora) - Chagu (Kigoma) (km 36) umefikia zaidi ya asilimia 80, Malagarasi-Ilunde Uvinza (km 51.1) umefikia asilimia 31 na ujenzi wa barabara ya Kibondo-Mabamba mpakani mwa Burundi (km 47.93).
Barabara nyingine ni Manyovu -Kasulu-Kibondo-Kabingo (Km 260.6) ambayo imegawanyika katika sehemu nne nazo ni Kasulu-Manyovu na viunganishi vyake (km 68.25) umefikia asilimia 47.12, Kanyani-Mvugwe (km 70.5) umefikia asilimia 54, Mvugwe-Njiapanda (km 59.36) umefikia asilimia 66.3, Nduta-Kabingo (km62.5) umefikia asilimia 78.5
pia Tanroads inatekeleza ujenzi wa barabara sehemu ya Njiapanda ya Nduta Kibondo Mjini (km 25.9) ambayo umefikia asilimia 57.3. Aidha, aliieleza kuwa miradi hiyo imeweza kutoa fursa za ajira zaidi ya vijana wazawa 1,500 wanatoka katika wilaya zinazopita mradi huo mkoani humo.
Kuhusu manufaa mengine ya miradi hiyo kwa jamii inayozunguka, Choma aliongeza kuwa katika mra 47.12, Kanyani - Mvugwe (km 70.5) umefikia asilimia 54, Mvugwe - Njiapanda (km 59.36) umefikia asilimia 66.3, Nduta - Kabingo (km
62.5) umefikia asilimia 78.5 pia Tanroads inatekeleza ujenzi wa barabara sehemu ya Njiapanda ya Nduta Kibondo Mjini (km 25.9) ambao umefikia asilimia 57.3. Aidha, aliieleza kuwa miradi hiyo imeweza kutoa fursa za ajira zaidi ya vijana wazawa 1,500 wanatoka ka-tika wilaya zinazopita mradi huo mkoani humo.
Kuhusu manufaa mengine ya miradi hiyo kwa jamii inayozunguka, Choma aliongeza kuwa katika mradi huo kumepatikana utoaji huduma za kijamii na zaidi ya Sh bilioni 21 zitatumika katika miradi ya nyongeza katika wilaya za Buhigwe, Kasulu na Kibondo.
"Miradi hii itanufaisha jamii kwani itahusisha na ujenzi wa Shule ya Bweni ya Buhigwe, Soko jipya la Manyovu, Stendi ya Mabasi ya Manyovu, Ujenzi wa Shule ya Msingi Busunzu, Kituo cha Afya Busunzu, Stendi ya Mabasi ya Kibondo, Ukarabati wa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu na Kibondo, Ujenzi wa miundombinu ya maji safi na majitaka, pamoja na miundombinu ya zimamoto wilayani Kasulu na Manyovu," alisema.