Rais Samia anavyojenga Diplomasia ya uchumi kwa weledi mkubwa

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
20260504_140336.jpg

Na África J&L, Dar es Salaam

Wakati Rais William Ruto atakapohutubia Bunge la Tanzania Mei 5, 2026, akiwa kiongozi wa kwanza wa Kenya kufanya hivyo, wengi wataona tukio la kihistoria. Lakini kimsingi, hili ni zaidi ya historia. Ni ushahidi wa jitihada za utekelezaji wa diplomasia ya uchumi lengo likiwa moja tu ajira, biashara, na nafasi imara ya kiuchumi katika Afrika Mashariki.
Hili si suala la kisiasa bali akili kubwa inayojenga uchumi endelevu.

NAMBA HAZIDANGANYI

Biashara kati ya Tanzania na Kenya sasa imevuka dola za Marekani bilioni 1, Mwaka 2024 pekee:

  • Tanzania iliuza bidhaa zenye thamani ya takribani $320.87 milioni kwenda Kenya
  • Kenya iliuza zaidi ya $500 milioni kwenda Tanzania
  • Mzunguko wa biashara unaendelea kuongezeka huku changamoto zikipatiwa ufumbuzi.
  • Tanzania na Kenya ni washirika muhimu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Uwekezaji: ajira kwa Watanzania, ukuaji kwa uchumi

  • Kampuni zaidi ya 529 za Kenya zinafanya kazi Tanzania
  • Zimewekeza takribani $1.7 bilioni
  • Zimezalisha ajira zaidi ya 56,000 kwa Watanzania
  • Kuanzia benki hadi mawasiliano na usafirishaji, uwekezaji huu unachochea sekta muhimu za uchumi.
  • Hivi karibuni tumeona mwelekeo mpya ambapo kampuni za Tanzania zinfanya uwekezaji nchini Kenya.
  • Zaidi ya Shilingi bilioni 9.3 za Kenya zimewekezwa katika sekta kama ujenzi, nishati, viwanda, na vyombo vya habari, ni wazi kuwa Tanzania si soko tu, ni mwekezaji anayekua na mwenye ushawishi.

Miradi mikubwa, dira kubwa zaidi Diplomasia ya Rais Samia pia inafungua milango ya miradi ya kimkakati

  • Mfano mkubwa ni mpango wa kiwanda cha kusafisha mafuta Tanga, unaohusisha nchi kadhaa za Afrika Mashariki na Kati.
  • Mradi huu unaweza:
  • Kupunguza utegemezi wa mafuta kutoka nje
  • Kushusha gharama za nishati
Kuweka Tanzania kama kitovu cha usindikaji wa nishati.

Kinachomtofautisha Rais Samia Suluhu Hassan ni namna yake ya uongozi, si kelele, bali matokeo, ameweka kipaumbele katika uhusiano thabiti na kuchagiza diplomasia ya uchumi akipunguza misuguano ya kibiashara na kujenga mazingira rafiki kwa wawekezaji.

Ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania sasa inaonekana kama mshirika anayetabirika na anayeaminika.

Uhusiano huu pia unaimarisha usalama wa kikanda. Tanzania na Kenya zinaendelea kushirikiana katika masuala ya ulinzi, kupambana na ugaidi, na usimamizi wa mipaka. Diplomasia inapofanywa vizuri, haileti picha nzuri tu, inaleta maendeleo halisi. Na kwa Tanzania, maendeleo hayo tayari yanaonekana. #WananchiNaUkweli

#TumeYaUchunguziReport
Uwajibikaji Wa Haki
 
View attachment 3583747

Na Africa J&L, Dar es salaam

Nimeisoma hoja yako, lakini kuna mambo muhimu yanahitaji kuwekwa sawa ili tusichanganye takwimu na tafsiri ya mafanikio.

Kwanza, ni kweli biashara kati ya Tanzania na Kenya imeongezeka, lakini ukiangalia hizo namba zako mwenyewe:
Kenya inauza zaidi kwetu kuliko sisi tunavyouza kwao.

Hii ina maana gani?
Kuna trade imbalance, na sio lazima iwe ishara ya ushindi wa kiuchumi kwa upande wetu.

Pili, uwekezaji wa kampuni za Kenya Tanzania:
Ndiyo, ajira zipo
Lakini swali la msingi ni;
Ajira za aina gani? (low-skilled au high-value?) Faida nyingi zinabaki Tanzania au zinarejea Kenya?
Bila kujibu hayo, kusema ajira sawa sawa na mafanikio ni oversimplification.

Tatu, kuhusu diplomasia ya uchumi: Diplomasia nzuri haipimwi kwa mikutano au hotuba tu, bali kwa kuimarika kwa viwanda vya ndani Kupungua kwa utegemezi wa bidhaa za nje
Kuongezeka kwa exports zenye thamani kubwa, hapo bado tuna safari ndefu kidogo, tusijifanye tumefika.

Nne, suala la miradi mikubwa kama refinery ya Tanga, Hii ni potential, sio matokeo bado. Tunahitaji kuona utekelezaji wake, sio mipango tu.

Mwisho kabisa, Ni sawa kupongeza juhudi za serikali, lakini pia ni muhimu kuwa na uchambuzi huru badala ya kugeuza kila kitu kuwa mafanikio makubwa.

Diplomasia ya uchumi ni nzuri, lakini: Matokeo yake lazima yaonekane kwenye maisha ya wananchi wa kawaida sio kwenye takwimu pekee.
 
Back
Top Bottom