Rais Samia anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T na SG kwa TZS 6.55T?

Rais Samia anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T na SG kwa TZS 6.55T?

..WOW!!

..hold on!!

..bilioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu dodoma.

..trillion 2 kwa ajili ya ununuzi wa ndege toka kwa mabeberu.

..bajeti ya kilimo na huenda isipatikane yote ni billion 294.

..vipaumbele vyetu haviko sawasawa.

cc Chige, Richard
Maelekezo kwa Katibu Mkuu hazina ni kwamba lazima ahakikishe kila wizara inapata angalau asilimia 50% ya bajeti ya maendeleo kwa hiyo kuwa mpole ndio kwanza hata robo ya kwanza ya mwaka bado
 
Akitaka kutengeneza legacy yake kama Mwendazake zake alipoua bandari ya Bagamoyo, ina maana miradi yote aliyoanzisha JPM itakufa kibudu. Reli itaishia Dodoma na nyie wasukuma itakula kwenu,haitofika Mwanza.

Legacy sio majengo na zege.
Maza ataikamilidha na mawe ya uzinduzi yatasoma jina lake na historia itasomeka hivyo
 
Ndo maana nasema hizo ni jitihada za kufanya spinning.

Dodoma haipaswi kujengwa kwa fedha hizo.

RC wa Dodoma lazima tafahamu hii kwanini ienezwe kwa mtindo huu?

Hatuwezi kuambiwa tunaongezewa tozo na hapohapo zipo fedha za kugharamia miradi kama ujenzi wa Dodoma.

Narudia kusisita kwa mama aangalie sana ushauri wa wapambe wenye nia tofauti kabisa na serikali ilopita ambayo iliweza kukusanya kodi na kulipia mahitaji ya wananchi bila kuhangaika.

Tuelezwe serikali ilopita ilifanyaje kuhakikisha fedha zinaenda kwenye elimu, walimu wanalipwa mishahara na watumishi wanaliowa mishahara yao ifikapo mwisho wa mwezi.
Tushaamua kuhamia Dom hakuna namna lazima Jiji lijengwe maana pia inasaidia kuwa na Jiji jingine kubwa kwa ajili ya soko siko kutegemea Dar tuu.

Saizi ukipita barabara ya Iringa Dom ikejaa malori ya mizigo hasa mbao kwa sababu Dom kumekucha
 
Unasemaje juu ya ongezeko la bei ya mbolea? Kuna kicheko kwa wakulima?
Sasa kwani kuna kodi iliongezwa huko? Tatizo ni global supply imeshuka vs demand .

Ili mbolea ishuke lazima serikali itoe pesa ya ruzuku kitu ambacho ni mzigo mkubwa Sana
 
Hii nchi ngumu sana,

Mimi nimeandika mambo halisi yaliyofanywa na Rais wa nchi tena kwa muda mchache sana,Wewe unatukana tu

Mnaotukana bila kukanusha wala kukubali nilichoandika mnaani gani?

Sema sio kweli SGR haijengwi,

Sema sio kweli SG haijengwi,

Sema sio kweli hajatoa ajira,

Sema sio kweli watu wamepandishwa madaraja,

Sema sio kweli daraja la Busisi na Nyerere halijengwi,

Sema sio kweli tozo 232 zimefutwa,

Sema sio kweli VRF ya 6% bado ipo,

Sema PAYE sio 8%

Sema sio kweli wanafunzi 10,000 wamelamba mikopo,

Sema sio kweli SGR Isaka -Mwanza Km 341 haijaanza kwa 3.02trl ,

Sema sio kweli SGR Dar-Moro Km 300 iko 77% na wakandarasi wamelipwa Cash 2.7trl,

Sema sio kweli kipande cha Moro-Dodoma km 442 kiko kwenye 30% na watu wanalipwa cash Tshs 4.4trl,

Sema sio kweli SG mama kashindwa kutoa US$2.8BL ,

Sema sio kweli Nyasi za bandia VAT yake imefutwa,

Sema sio kweli kurasimisha ardhi sasa ni 1% tu,

Sema sio kweli ndege hazinunuliwi,

Sema sio kweli meli hazinunuliwi,

Sema sio kweli Mama amemaliza mpango wa Hoima na vijana 10,000 watalamba ajira,

NJOONI NA HOJA SIO POROJO,

MAMA ANAVUNJA REKODI ZOTE ZILIZOWEKWA KAMA UNABISHA SEMA WAPI KAKWAMA.
Sasa wewe yote hayo ulitaka baba yako ndiye afanye? Hayo ni wajibu wa serikali tena wanatakiwa kufanya mara tano ya hayo!
 
Hivi kweli nyie mkipewa serikali,Mnaweza kuiongoza hata mwezi mmoja?

Swali lako lingekuwa more meaningful kama ungetuuliza kuhusu uwezo wa kuiongiza nchi kwa ufanisi.

Uongozi wa “bora liende” kila mtu anauweza. Hata comedians wa Dar wanaweza. Tena wakipata bahati ya kuwa na key players wanaojua wanachokifanya na wakawasikiliza, nchi inaweza kwenda vizuri mpaka utashangaa.

Tumeshawahi kuona matokeo ya uongozi wa “bora liende”. Mkapa aliipokea nchi ikiwa na mlima wa madeni and a broken economy (characterized by inflation that had gone through the roof)!
 
Maelekezo kwa Katibu Mkuu hazina ni kwamba lazima ahakikishe kila wizara inapata angalau asilimia 50% ya bajeti ya maendeleo kwa hiyo kuwa mpole ndio kwanza hata robo ya kwanza ya mwaka bado

..bajeti ya maendeleo ni 20% ya bajeti nzima.

..serikali inabidi ifunge mkanda kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

..kwa mfano, kuna watumishi ambao hawahitajiki kama wakuu wa wilaya.

..kazi za wakuu wa wilaya zinaweza kufanywa na DAS.

..kuna maeneo mengi serikali inapaswa kuyaangalia ili kubana matumizi.
 
Binafsi hapo hoja namba Mbili huyu mama ametenda vyema sana,hiki ndo kitu kinanifanya niendelee kumpenda huyu mama Samia
 
Wasalaam wanaJf,

Ukichukua gharama za miradi miwili tu mikubwa ya SGR na SG inayoendelea kwa sasa yaani Isaka -Mwanza 341km Tshs 3.02trl, Makutupora-Morogoro 422Km Tshs 4.4trl ,Morogoro -DSM 300Km Tshs 2.7trl na SG US$ 2.9BL Tshs 6.5trl Jumla yake ni Tshs 16.6trl achilia mbali miradi mingine yote ikiwemo mipya na ile iliyoachwa na Rais Magufuli yote mama anaziendeleza tena kwa BOQ zilezile,

Kinachonivutia zaidi ni hivi vicheko kwa haya makundi mbalimbali najiuliza Rais Samia amewezaje yote haya yaliyowashinda watangulizi wake wote? Mfano:,


1. Kicheko cha Rais Samia na wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Mpaka Rais Samia anaingia madarakani zaidi ya watoto wa masikini elfu 10 hawakupewa mikopo,Leo tayari ameongeza Tshs 106BL sawa na 23% yaani kutoka Tshs 464BL FY2020/21 hadi 570BL FY2021/22 na kufanya kila mtoto wa masikini aliyefaulu kwenda chuo kikuu kupatiwa mkopo bila kujali historia ya alikosomea huku akifuta kabisa ile 6% ya ada ya thamani ya mkopo ( Value Retention Fee-VRF ) kwenye mikopo hiyo na Sasa wanufaika watakatwa 9% ( single digits) FY2021/22 kutoka 15% ya FY2020/21,Kwa lugha rahisi take home za watu hawa zimepaa kwa 6% nivicheko kila kona ya nchi,
__________________________________

2. Kicheko cha Rais Samia na Wafanyakazi,Sote tunafahamu,kwa miaka mitano ( 5 ) mfululizo tumeshuhudia wafanyakazi wa Umma hawakupandishwa vyeo|madaraja,lakini ndani ya miezi hii michache mama ameshatoa Tshs 509BL,Yaani 449BL za madaraja|vyeo na 60BL za malimbikizo ya mishahara na tayari Pesa hizi zimeleta vicheko kwa wafanyakazi huku akipunguza kodi (PAYE) toka 9% FY2020/21 mpaka 8% hivi sasa,kwa lugha rahisi FY2021/22 ameongeza mishahara ya wafanyakazi wote wa Serikali na binafsi kwa 1% kwa kuwarudishia hiyo 1% ya mishahara yao, na kwakufanya hivyo serikali itatumia|itapoteza kiasi cha Tshs 14.1781BL fedha ambayo itarudishwa kwa wafanyakazi kama nyongeza,
__________________________________

3. Kicheko cha Rais Samia na wasio Ajiriwa,mwisho ilikuwa FY2015/16 wakati wa Mzee JK alipoachilia ajira mpya elfu 52 trh 01|05|2015,Leo miaka mitano baadae na nimiezi michache ya Mama Samia tunashuhudia tena ajira mpya za serikali elfu 40 kwa gharama ya Tshs 239BL na 120BL kwaajili ya kubadili muundo wa Utumishi,maajabu zaidi ya mama tayari amesajili miradi mikubwa mipya 93 yenye thamani ya US$ 1.6BL karibu Tshs 3.23trl ambayo nayo itaajiri watu 23,600 na kumfanya ndani ya hivi vimiezi vichache kutoa jumla ya nafasi 53,600 za ajira achilia mbali miradi mingine mingi ya sekta binafsi|Umma inayoendelea kutoa ajira lengo likiwa ni ajira 8M mwaka 2025.
__________________________________

4. Kicheko cha Rais Samia Majimboni,Bila kujali ukubwa wa jimbo ameshatoa Tsh 132BL sawa na Tshs 500M kila Jimbo kwa majimbo yote 264 kama fedha za maendeleo ya Jimbo mbali na fedha za mfuko wa Jimbo,fedha hizi zimerudisha tabasamu kwa Wabunge hasa wa Majimbo,Mama ametoa tena Tshs 322.158BL kama bajeti ya nyongeza kwaajili ya Ujenzi wa Vyumba 10,000 vya madarasa Zahanati 555,Vituo vya afya 121,hakuishia hapo TARURA nao bajeti yao ameiongeza kwa 254% yaani kutoka 273BL FY 2020/21 hadi 966.43BL FY2021/22 kumaliza kila barabara korofi Vijijini|Mitaani,Nimwendo wa vicheko Tu,
__________________________________

5. Kicheko cha Rais Samia na wafanyabiashara|Wawekezaji, Mhe Samia Ndio rais pekee aliyetangaza hadharani hahitaji kodi za Kishetani na akafuta jumla ya kodi|tozo zote kandamizi zipatazo 232 bila kujali hasara ya Tshs 55.49997BL ambayo serikali yake itapata kwa kuondoa tozo|kodi hizo nia yake aongeze idadi ya walipa kodi kutoka 2.7M waliopo na matokeo najua wote tumeyaona ,Nchi hii tangu tupate uhuru sijawahi kusikia tozo|kodi zaidi ya 230 zikifutwa kwa kwamkupuo Kama ambazo mama ameachilia kicheko hiki kwani hataki kabisa Tax economy ,pamoja na kukataa kodi za kishetani na kuondoa tozo kandamizi bado Miradi yote ya Watangulizi wake anaiendeleza sawasawa ikiwemo SGR US$ 4.64BL au Tsh 10.2trl,SG US$ 2.9BL au Tshs 6.5trl,ndege Mpya,barabara zote ujenzi unaendelea, madaraja yote,meli zote pamoja na haya yote kufanyika bado Wafanyakazi wetu ni vicheko,Wafanyabiashara|wawekezaji wetu ni vicheko,bodaboda wetu ni vicheko, machinga wetu ni vicheko,wanafunzi wetu hasa wa elimu ya juu ni vicheko, wafugaji wetu ni vicheko,wakulima wetu ni vicheko, Wapinzani nao ni vicheko hata wewe unayesoma naamini, Tayari nawewe unakicheko chako umecheka na Mama Samia ,


" Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama deserves better Wazalendo wote tumtie moyo, mpaka mwaka 2030 tutashuhudia maajabu, Tuombe uzima Tu"
Uli ntumbafu ghete
 
Huyu mama aishi milele,

Mke wangu kalamba 250,000 daraja jipya,

Ndio kwa mara ya kwanza Sal Slip imebadilika tangu 2015.

Mimi na familia yangu tunamtaka huyuhuyu 2025,

Mbona anafanya yote yaliyofanywa na Magufuli na bado anaachia pesa, hayati alikwama wapi?
Umeandika ushuzi tupu
 
..miradi haijakamilika hivyo sio sahihi kusema Raisi ameweza kujenga sgr, au sg.
 
Kwenye Heslb watumishi wamepigwa chenga ya Mwili kabisaa!!hakuna kitu!kwenye punguzo la kodi ya asilimia moja ndio usiseme!!!!
 
Kwenye Heslb watumishi wamepigwa chenga ya Mwili kabisaa!!hakuna kitu!kwenye punguzo la kodi ya asilimia moja ndio usiseme!!!!


Mkuu hii Bunge limeshapitisha kama wewe bado unakatwa hiyo 6% nenda bodi kalalamike, Watakuhudumia
 
Back
Top Bottom