Rais Samia anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T na SG kwa TZS 6.55T?

Maelekezo kwa Katibu Mkuu hazina ni kwamba lazima ahakikishe kila wizara inapata angalau asilimia 50% ya bajeti ya maendeleo kwa hiyo kuwa mpole ndio kwanza hata robo ya kwanza ya mwaka bado
 
Akitaka kutengeneza legacy yake kama Mwendazake zake alipoua bandari ya Bagamoyo, ina maana miradi yote aliyoanzisha JPM itakufa kibudu. Reli itaishia Dodoma na nyie wasukuma itakula kwenu,haitofika Mwanza.

Legacy sio majengo na zege.
Maza ataikamilidha na mawe ya uzinduzi yatasoma jina lake na historia itasomeka hivyo
 
Tushaamua kuhamia Dom hakuna namna lazima Jiji lijengwe maana pia inasaidia kuwa na Jiji jingine kubwa kwa ajili ya soko siko kutegemea Dar tuu.

Saizi ukipita barabara ya Iringa Dom ikejaa malori ya mizigo hasa mbao kwa sababu Dom kumekucha
 
Unasemaje juu ya ongezeko la bei ya mbolea? Kuna kicheko kwa wakulima?
Sasa kwani kuna kodi iliongezwa huko? Tatizo ni global supply imeshuka vs demand .

Ili mbolea ishuke lazima serikali itoe pesa ya ruzuku kitu ambacho ni mzigo mkubwa Sana
 
Sasa wewe yote hayo ulitaka baba yako ndiye afanye? Hayo ni wajibu wa serikali tena wanatakiwa kufanya mara tano ya hayo!
 
Hivi kweli nyie mkipewa serikali,Mnaweza kuiongoza hata mwezi mmoja?

Swali lako lingekuwa more meaningful kama ungetuuliza kuhusu uwezo wa kuiongiza nchi kwa ufanisi.

Uongozi wa “bora liende” kila mtu anauweza. Hata comedians wa Dar wanaweza. Tena wakipata bahati ya kuwa na key players wanaojua wanachokifanya na wakawasikiliza, nchi inaweza kwenda vizuri mpaka utashangaa.

Tumeshawahi kuona matokeo ya uongozi wa “bora liende”. Mkapa aliipokea nchi ikiwa na mlima wa madeni and a broken economy (characterized by inflation that had gone through the roof)!
 
Maelekezo kwa Katibu Mkuu hazina ni kwamba lazima ahakikishe kila wizara inapata angalau asilimia 50% ya bajeti ya maendeleo kwa hiyo kuwa mpole ndio kwanza hata robo ya kwanza ya mwaka bado

..bajeti ya maendeleo ni 20% ya bajeti nzima.

..serikali inabidi ifunge mkanda kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

..kwa mfano, kuna watumishi ambao hawahitajiki kama wakuu wa wilaya.

..kazi za wakuu wa wilaya zinaweza kufanywa na DAS.

..kuna maeneo mengi serikali inapaswa kuyaangalia ili kubana matumizi.
 
Binafsi hapo hoja namba Mbili huyu mama ametenda vyema sana,hiki ndo kitu kinanifanya niendelee kumpenda huyu mama Samia
 
Uli ntumbafu ghete
 
Umeandika ushuzi tupu
 
..miradi haijakamilika hivyo sio sahihi kusema Raisi ameweza kujenga sgr, au sg.
 
Kwenye Heslb watumishi wamepigwa chenga ya Mwili kabisaa!!hakuna kitu!kwenye punguzo la kodi ya asilimia moja ndio usiseme!!!!
 
Kwenye Heslb watumishi wamepigwa chenga ya Mwili kabisaa!!hakuna kitu!kwenye punguzo la kodi ya asilimia moja ndio usiseme!!!!


Mkuu hii Bunge limeshapitisha kama wewe bado unakatwa hiyo 6% nenda bodi kalalamike, Watakuhudumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…