Pre GE2025 Rais Samia anayo sifa ya kupiga kura Tanganyika?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Samia kutaka kuingia kwenye mambo ya kupiga kura Tanganyika wakati yeye ni Mzanzibari (Ana kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi) siyo uvunjivu wa Katiba?
Mkuu kwani wewe ulipoenda kujiandikidha kupiga kura umetumia kitambulisho cha Mtanganyika mkaazi?

Hivi akitokea mtu akakushangaa kwa hili atakuwa amekosea? Samahani nilikuwa natafakari tu kwani ndo kwanza natoka usingizini.

Wako;
Mzanzibari Mkaazi.
 
Rais Samia alipata nafasi ya kuwa mgombea mwenza wa Magufuli kwa sababu ni mzanzibari Serikali za Mitaa siyo miongoni mwa mambo ya Muungano. Akipiga kura huku Tanganyika atakuwa amekiuka sheria.
Mkuu atakuwa amekiuka sheria ipi na ya mwaka gani, chini ya kifungu gani?
 
Kila Mzanzibar ni Mtanzania na sio kila Mtanzania ni Mzanzibar.
 
Katiba ilikwisha eksipaya hivyo tunaishi kiholela ndiyo sababu Mzee Mwinyi alilazimishwa kuzikwa kwao kupya.
 
Kila Mzanzibar ni Mtanzania na sio kila Mtanzania ni Mzanzibar.
Hii kauli mbona haina maana? Sawa na kusema kila mchagga ni mtanzania Ila sio kila mtanzania ni mchagga

Mwingine atasema kila mgogo ni mtanzania Ila sio kila mtanzania ni mgogo.

Mwingine atasema kila msambaa ni mtanzania Ila sio kila mtanzania ni msambaa

Etc.....
 
Kwani ni uongo ndugu zangu?
 
Ungeleta ibara inayosema unayosema tungekua sehemu salama. Mwisho nchi hii inaongozwa na Rais Mtanzania nasio raia wa nchi nyingine.
 
Rais Samia alipata nafasi ya kuwa mgombea mwenza wa Magufuli kwa sababu ni mzanzibari Serikali za Mitaa siyo miongoni mwa mambo ya Muungano. Akipiga kura huku Tanganyika atakuwa amekiuka sheria.
Mbona aibu hii kwakweli? Hivi tulisema atokee upande mmoja wa Tanzania maana yake ni mtu wa kutoka Taifa jingine?
 
Tuna wajinga wengi!! Hivi uraia huwa unapatikana kwa kujenga? Mrundi akija Tanzania akajenga nyumba, tayari anakuwa Mtanzania?
Ukisema wajinga wengi nawe usijondoe katika ili. Je,kuna raia wa Zanzibar?
 
Wewe ni fala tu. Hivi huko Chadema hakuna wenye akili kabisa?
Kuzindua ni kupiga kura au ni kuruhusu zoezi liendelee?
Akili zenu hazina akili kwa kweli
 
maswali mengine waulizeni waliomuweka pale, wenye hekima waliona mbali wakapinga asiwe raisi wao wakatumia mabavu eti wanalinda katiba nadhan wanafurahi sasa kwa haya yanayoendelea
 
Mbna mambo ya utanganyika Nyerere alishayamaliza au unamaanisha anataka kupigwa kura katika Halmashauri ya Tanganyika huko Katavi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…