mbikagani
JF-Expert Member
- Dec 5, 2014
- 3,107
- 1,782
RAIS Samia. Morogoro tunashida hizi;
KIWANDA CHA MAZAVA KUFUNGWA
Kiwanda hiki kilikuwa kinatengeneza nguo(jezi), kiliajiri zaidi ya watu elfu kumi(10000)
Kwa sasa kimefungwa kwa kile kinachoelezwa kuwa kutokuelewana na serikali ya awamu ya tano katika suala la ulipaji kodi.
Kimsingi hakuna anayependa mtu au taasisi isiyolipa kodi, lakini inasemekana mashariti ya ulipaji kodi yalikuwa kandamizi sana na ndiyo sababu ya hiki kiwanda kufunga uzalishaji.
Rais tupia jicho hapa ili kama kuna haja ya kuzungumza na wawekezaji hawa uwaruhusu wafungue kiwanda hiki maana wananchi wengi wamepoteza ajira zao.
2. KIWANDA CHA SUKARI CHA MBIGIRI CHASABABISHA UMASIKINI KWA WAKULIMA
Kiwanda hiki kimeleta umasikini mkubwa kwa wakulima wadogo wadogo wa miwa wilaya ya kilosa.
Mpaka sasa miwa yao imefikia kuvunwa na kiwanda bado hakijakamilika mpaka wanaamua kwenda kuuza kiwanda cha Mtibwa.
Mbaya zaidi benki ya AZANIA imewaongezea riba kwa kuchelewa kurudisha mikopo yao.
Kama haitoshi wakandarasi wamewashitaki wakulima kwa sababu benki ya AZANIA wamekataa kuwapa mkopo ambao kimsingi benki ilisaini mkataba wa kuwapa mkopo.
3. KIWANDA CHA TUMBAKU KUFUNGWA
Kiwanda hiki kiliajiri wananchi zaidi ya elfu kumi(10000), kwa sasa kimefungwa kwa kile kinachoelezwa ni kutoelewana na serikali ya awamu ya tano kwenye ulipaji kodi.
Si vema kutolipa kodi lakini inasemakana mpaka wameamua kufunga kiwanda, kodi ilikuwa kandamizi sana.
Angalia na hapa Mama kama mtaelewana waruhusu warejee ili wananchi wapate ajira maana kwa sasa wapo mitaani tu wanaangaika.