Rais Samia, angalia viwanda hivi vilivyofungwa hapa Morogoro

Rais Samia, angalia viwanda hivi vilivyofungwa hapa Morogoro

Aisee ila Tz kuna mazingira magumu sana ya kibiashara mikodi ya kutosha na ukifungua tu kuanzia Mwenyekiti wa CCM mpaka RPC itabid wawe kwenye mfuko wako wa posho la sivyo utapata tabu sana
Nchi ngumu sana hii.
 
Alliance one ni kidogo sana. Kile cha mjini (TTPL) ndio kilikuwa bonge la kiwanda tena kilikuwa na nyota tano kwa ufanisi na ubora. Msimu wa Tumbaku ukianza, mitambo haizimwi kwa miezi mitatu. Wanapisha wafanyakazi tu kwa shift tatu (kuna wanaoingia asubuhi, kuna wa mchana na wengine usiku). Na kila shift ina wafanyakazi zaidi ya 6,000.

Mbali ya Serekali kupoteza mapato, pia Vijana wengi wamekosa kazi na kusababisha wizi uanze kurudi huku mtaani. Kuna haja ya kufanya kitu ili hivi viwanda viendelee kuwepo.
Wadada wengi kutoka sehem kama Chamwino, Kiwanja cha ndege na Mazimbu wamepoteza ajira zao.
 
Back
Top Bottom