Alliance one ni kidogo sana. Kile cha mjini (TTPL) ndio kilikuwa bonge la kiwanda tena kilikuwa na nyota tano kwa ufanisi na ubora. Msimu wa Tumbaku ukianza, mitambo haizimwi kwa miezi mitatu. Wanapisha wafanyakazi tu kwa shift tatu (kuna wanaoingia asubuhi, kuna wa mchana na wengine usiku). Na kila shift ina wafanyakazi zaidi ya 6,000.
Mbali ya Serekali kupoteza mapato, pia Vijana wengi wamekosa kazi na kusababisha wizi uanze kurudi huku mtaani. Kuna haja ya kufanya kitu ili hivi viwanda viendelee kuwepo.