Asantehene
Member
- Nov 18, 2025
- 8
- 11
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres anatarajiwa kumaliza muda wake kama Katibu Mkuu wa tisa aliyeliongoza Shirika la Umoja wa Mataifa kwa miongo miwili, hadi hapo Desemba 31 mwaka huu. Kama kawaida, siasa za chinichini zimekwishaanza za kumpata mrithi wake, huku mataifa kadhaa yakiwa tayari yameshapendekeza watu wao (potential candidates).
Kwa haraka haraka, nilianza kuiwaza Tanzania kama tuna mtu yeyote anayeweza kuchukua nafasi hiyo. Kiufupi, nchi kama Argentina imempendekeza Rafael Mariano Grossi (miaka 65), kisha kuna mwanamama Rebecca Grynspan (miaka 70), ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Costa Rica, na mwanamama mwingine Michelle Bachelet (miaka 74), ambaye pia alikuwa Rais wa taifa la Chile, na wote hawa ukiwatazama wana sifa za kutosha kuongoza shirika hilo.
Kwa Afrika, mtu anayetazamwa kwa sasa ni Macky Sall (miaka 64), aliyekuwa Rais wa Senegal kwa mihula miwili hadi mwaka 2024, na anaweza kupata uungwaji mkono wa nchi nyingi tu za Afrika.
Nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni miaka 5, ikimaanisha kwamba kufikia mwaka 2031, uchaguzi mwingine ungeweza kufanyika. Afrika ina historia nzuri ya kuwa na makatibu wakuu wa umoja wa mataifa, akiwemo Koffi Annan aliyeongoza kati ya mwaka 1997 hadi 2006.
Namtazama Rais Samia kwa jicho la wivu, namuona kama fursa iliyopotea, kwasababu angekuwa na sifa zote za kumwezesha kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa, iwe mwaka 2031 au mwaka 2036.
Ni wazi kuwa Tanzania, ambayo iliwahi kuwa kimbilio hasa wakati wa ukombozi wa nchi za Afrika na mfano wa kuigwa katika siasa za kimataifa, imepoteza hadhi yake kimataifa, na kama kulikuwa na matumaini yoyote ya kushika nafasi za uongozi kimataifa, ni wakati wa kuzika matumaini hayo kwa sasa.
Nawasilisha.

- Umri: Hadi kufikia mwaka 2031, Rais Samia atakuwa na umri wa takriban miaka 71. Ingawa ni kama umri mkubwa, lakini huu ni umri mzuri sana wa kuwepo kwenye siasa za kimataifa.
- Jinsia na Jiografia: Rais Samia pia angekuwa na nafasi inayombeba kama mgombea mwanamke wa nafasi hiyo nyeti duniani. Tangu kuanzishwa kwake, nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa haijawahi kumwangukia mwanamke. Nani ajuaye, pengine hii ingekuwa fursa ya Tanzania kuweka rekodi ya kwanza kuwa mwanamke wa kwanza kutokea barani Afrika kushika nafasi hiyo.
- Mrengo wa Siasa: Rais Samia alianza nafasi yake ya urais akiwa na pointi za bure kabisa za kisiasa kwa kufanya upatanishi katika taifa ambalo tayari lilikuwa na migongano na migawanyiko ya kisiasa kutoka kwa mtangulizi wake, pamoja na uwezo wake wa kuzungumza na kila pande. Laiti angeendelea na falsafa zake za 4R, au angeendelea kujenga picha ya upatanishi kama "mama," angekuwa na nafasi nzuri ya kujipatia uungwaji mkono kimataifa kwa kigezo cha "sifa ya uongozi nyumbani" inayozingatiwa sana kumpata mgombea wa nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.