Rais Samia aongeza Saa 24 kwenye uokoaji Kariakoo

Rais Samia aongeza Saa 24 kwenye uokoaji Kariakoo

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Wajuvi wa masuala haya, kwahivyo, bila kujali hali ilivyo muda wa uokoaji ikitokea janga kama hili huwa ni masaa 72 pekee?

Kwa jinsi ile ajali ilivyotokea watakauwa waokoaji watakuwa wamefika maeneo yote? Naona kama kuna watu wataachwa huko wajifie!

=====

Screenshot_2024_11_19_09_47_30_072_com_instagram_android_edit.jpg
Screenshot_2024_11_19_09_47_47_502_com_instagram_android_edit.jpg



Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo.

Rais Dkt. Samia ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Mhe. Majaliwa kuhusiana na zoezi la uokoaji na kusema:

"Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninatambua utaratibu wa uokoaji una muda maalum wa saa 72 mpaka kusitisha zoezi hilo. Binafsi nina matumaini kuwa Mwenyezi Mungu anaweza akatenda miujiza yake na kuweza kuwanusuru ndugu zetu wengine ambao bado wamenasa kwenye jengo hilo. Ninakupa maelekezo ya kutositisha zoezi la uokoaji na kuongeza muda wa saa 24 zaidi ili kuwapambania ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai."

Aidha, Rais Dkt. Samia pia ameongeza kusema kuwa: "Kwa vikosi vyetu vyote na wananchi wote wanaopambana kuokoa maisha ya ndugu zetu katika zoezi hilo ninaomba ufikishe salamu zangu na uwaeleze kuwa natambua na nina wathamini sana. Wameonyesha utu, uzalendo mkubwa na uchapakazi wa hali ya juu sana. Hivyo nawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kuwapambania ndugu zetu kwani ninyi ni mashujaa wa taifa letu"

Rais Dkt. Samia anawaombea kwa Mungu awalinde na kuwapa nguvu muda wote wakiwa wanateleleza jukumu hilo kubwa na la kizalendo.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Samia amewasihi wananchi, ndugu na jamaa kuendelea kuwa na subira na kama taifa tuendelee kuwaombea ndugu zetu na wapiganaji wetu ili tufanikishe zoezi hili kwa mafanikio makubwa.

Mwenyezi Mungu tunakuomba utufanyie wepesi kwenye zoezi hili. Amin
Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
 
Wakuu,

Wajuvi wa masuala haya, kwahivyo, bila kujali hali ilivyo muda wa uokoaji ikitokea janga kama hili huwa ni masaa 72 pekee?

Kwa jinsi ile ajali ilivyotokea watakauwa waokoaji watakuwa wamefika maeneo yote? Naona kama kuna watu wataachwa huko wajifie!

=====

View attachment 3155882View attachment 3155883
Je kama hao walio naswa humo ndani bado wamo tena wako hai, na hayo masaa 24 yamekwisha
 
Tanzania nchi yangu.....
Kuna wakati nadhani sijui ni Magomeni quarters au wapi NHC walikuwa wanatoa watu kwa nguvu ili wavunje nyumba. Mzee MMOJA mstaafu na mkazi wa hapo akamwita mwandishi wa ITV karibu akamwambia najuta sana kuwa Tanzania, nilipata nafasi ya kuhamia nje nikakataa ila Sasa najuta......... Muda sana umepita....

Sasa kweli hii ni kitu hata ya kutoa tamko..... Jengo lisachiwe watu waokolewe wote. Na Leo asubuhi nimesikia hao waokoaji wamesikia sauti zinaomba msaada humo. Kwahiyo yakiisha hayo 24 waachwe wachanganywe na kifusi?????

Hivi mshawahi sikia sera ya USA kuwa no man will be left behind??.... Yaani iwe vitani au Hawa tourists au hata Hawa expatriate iwe amekufa iwe Yuko hai atarudishwa nyumbani....

Huko Chile mnakumbuka miners walikwama zaidi ya miezi miwili na waliokolewa...... Siku 69 mwaka 2010... Sasa sisi tuna law of limitation kwenye suala kama hili.
 
Badala ya kupunguza yale maloba na mizigo ambayo ilikuwa aina shida yeyote.......kazi kuongeza uzito tu.........lakini wenye vidigirii ndio wanajiona wanajua wakati yale maloba yanazidi kuongeza uzito............PUNGUZENI MALOBA HAYO NA MIZIGO MINGINE GHOROFA LIWE JEPESI MFANYEKAZI CHAP CHAP........ujuaji mwiiiiiingiiiii kisa nina digirii .........digirii inaongeza damu kwani
 
Back
Top Bottom