Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwenyezi Mungu awatetee...daahKunadugu bado wako chini kabisa ila hawaongeibsbb hawana nguvu,,serikali injitahidi kupekua Kila kitu kiwaokoa
Kuna kitu sielewi, ina maana ukishapita muda huo ulioagizwa na Rais ni kwamba jengo litaporomoshwa lote kwa kuamini kwamba ambao bado wapo chini ya kifusi watakuwa wamekwisha fariki?
Pongezi Kwa Rais Samia
Amewajali wahanga
Ameonyesha utu wake
Mama ishi sana Rais wetu
Sheria za uchaguzi zinakanyagwa kwa manufaa yao Leo wanajifanya sheria za uokozi ndio wanazifuata kwa makiniWao wakifa wanataka tuwazungushe Tanzania nzima mwezi mzima, leo wapendwa wetu wanapewa masaa ya kuokolewa?Kweli inawezekana sisi ni zaidi ya maiti, mimi sikujua kama kunasheria ya kigaidi kama hii
Bila shaka wanamaanisha uokoaji wa walio hai.Kwahiyo kumbe uokoaji una muda maalum kwamba ukipita tunaondoka eneo la tukio kuwe na Watu ama Lah?
Masaa 24 ni madogo kuwaokoa Watu bado wapo Wangeongeza Masaa 72 mengine tena aka siku 3 au mpaka jumapili ingelikuwa ni vizuri sana. Kuliko kuweka masaa 24 ni madogo sana kuwaokoa watu kazi yake sio ndogo jamani kuna watu bado wapo ndani wanasubiri kuokolewa Rais anatoa Masaa 24 kuwaokoa watu? Duhhhhhh Majangaa kweli.Wakuu,
Wajuvi wa masuala haya, kwahivyo, bila kujali hali ilivyo muda wa uokoaji ikitokea janga kama hili huwa ni masaa 72 pekee?
Kwa jinsi ile ajali ilivyotokea watakauwa waokoaji watakuwa wamefika maeneo yote? Naona kama kuna watu wataachwa huko wajifie!
=====
View attachment 3155882View attachment 3155883Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo.
View attachment 3155951
Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo
Rais Dkt. Samia ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Mhe. Majaliwa kuhusiana na zoezi la uokoaji na kusema:
"Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninatambua utaratibu wa uokoaji una muda maalum wa saa 72 mpaka kusitisha zoezi hilo. Binafsi nina matumaini kuwa Mwenyezi Mungu anaweza akatenda miujiza yake na kuweza kuwanusuru ndugu zetu wengine ambao bado wamenasa kwenye jengo hilo. Ninakupa maelekezo ya kutositisha zoezi la uokoaji na kuongeza muda wa saa 24 zaidi ili kuwapambania ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai."
Aidha, Rais Dkt. Samia pia ameongeza kusema kuwa: "Kwa vikosi vyetu vyote na wananchi wote wanaopambana kuokoa maisha ya ndugu zetu katika zoezi hilo ninaomba ufikishe salamu zangu na uwaeleze kuwa natambua na nina wathamini sana. Wameonyesha utu, uzalendo mkubwa na uchapakazi wa hali ya juu sana. Hivyo nawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kuwapambania ndugu zetu kwani ninyi ni mashujaa wa taifa letu"
Rais Dkt. Samia anawaombea kwa Mungu awalinde na kuwapa nguvu muda wote wakiwa wanateleleza jukumu hilo kubwa na la kizalendo.
Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Samia amewasihi wananchi, ndugu na jamaa kuendelea kuwa na subira na kama taifa tuendelee kuwaombea ndugu zetu na wapiganaji wetu ili tufanikishe zoezi hili kwa mafanikio makubwa.
Mwenyezi Mungu tunakuomba utufanyie wepesi kwenye zoezi hili. Amin
Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Kwanini waongeze saa 24?Bila shaka wanamaanisha uokoaji wa walio hai.
Baada ya hapo zoezi litabadilika na kuwa na kuopoa miili ya wafu.
Baada ya hapo zoezi litakuwa na kuhamisha vifusi.
Kila hatua hapo kuna taratibu zake! Nawasilisha!
Nadhani ni saa 24 za uokoaji kuwapata watu wakiwa wazima.Kwanini waongeze saa 24?
Kumbe zoezi linaendelea