Rais Samia aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

Rais Samia aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kilichokutana Jijini Dar es Salaam leo tarehe 29 Juni 2024.


#CCMImara
#VitendoVinaSauti
#TunaendeleaNaMama
#KaziIendelee
ukiangalia picha tu unapata matuamaini makubwa na ya uhakika moyoni, kwamba nchi iko salama, Imara na uelekeo wa Taifa ni mzuri sana...

kila la kheri comrade Dr.Samia Suluhu Hassan na wajumbe wote wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya ccm Taifa:KasugaYeah::KasugaYeah::ClapHD::ClapHD:
 
Watumishi wana hasira na kutopanda vyeo/madaraja mwezi June alijue hilo.
Wamekuwa ni ma GEN Z bado tu kuingia barabarani
 
RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kilichokutana Jijini Dar es Salaam leo tarehe 29 Juni 2024.


#CCMImara
#VitendoVinaSauti
#TunaendeleaNaMama
#KaziIendelee
Kikao cha kitapeli
 
Acha matusi ya kijinga wewe!

Huyo FaizaFoxy, ifuatilie michango yake. Mtu mjinga na mnafiki atawezaje kuuacha ujinga? Si ndivyo alivyo? Kusubiria hekima na weledi kutoka kwa FaizaFoxy,.ni kusubiria embe chini ya mchongoma.
 
Waje na jibu la muungano ,La lisu

Mana ,kinana aliamua luwaambia uwongo makatibu tawi nchizima pale dodoma
 
Ndugu zangu Watanzania,

Yaani hata ukitazama tu kwa picha na namna wajumbe walivyokaa unaona dhahiri kabisa kuwa hiki ni chama kilichobeba matumaini ya watanzania, unaona ni chama chenye kutoa muelekeo wa nchi, unaona ni chama kilicho imara na mfumo thabiti, unaona ni chama chenye Dira na muelekeo unaoeleweka na maono yenye kulipeleka mbele Taifa letu kimaendeleo.

Unaona namna kilivyosheheni watu wazito, wenye akili, upeo, maarifa, utulivu, uwezo wa kiuongozi na wanaostahili kuwa hapo walipo, unaona ni chama kinachojuwa nini watanzania wanataka, nini kiu ya wengi, unaona ni chama chenye majibu na majawabu ya maswali ya watu, unaona kimebeba na kuunganisha watu wenye mawazo na maono makubwa kwa mstakabali wa Taifa letu, unaona ni watu wenye vibali na Karama za uongozi na kibali mbele za Mungu.

Sasa nenda upande wa pili kule kwa CHADEMA, utacheka mpaka upasuke, kwanza wanaingia vikaoni kila mtu akiwa hana matumaini wala mawazo ya kukijenga chama wala kukipa uhai wala dira na muelekeo unaoeleweka, ni chama ambacho ni kama mkusanyiko wa watu mnadani ambapo wengine huenda tu kwa ajili ya kutembea na kuzurura tu na kupoteza Muda.

Itachukua miaka mingi sana zaidi ya Millenium kadhaa kwa vyama vya upinzani kufikia hata robo tu ya nguvu ya CCM. Vyama vya upinzani ni vyama vinavyostahili kuendelea kuongozwa tu. CCM itaendelea kuwa chama kiongozi kwa muda wote.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

View attachment 3029083

Pia soma: Rais Samia kuongoza Vikao vya Kamati kuu na Halmshauri kuu ya CCM Taifa June 29-30
Chawa anacheka kishetani. Acha uchawa dogo .
 
Back
Top Bottom