benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelionya jeshi la Polisi nchini kutotumia wadhamini kufanya vikao kazi na badala yake Jeshi hilo lijitegemee na vikao vyake vifanyika kwa gharama za Jeshi.
Amesema kuwatumia wadhamini katika kuwezesha kuendesha vikao hivyo, kutawafanya washindwe kuwaadhibu pale wanapofanya makosa.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo leo Jumanne Agost 30, 2022, wakati akifungua kikao cha maofisa wa polisi makao makuu, makamanda wa mikoa na vikosi, kinachofanyika katika Shule ya Polisi Tanzania, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Amesema kikao kinachofanyika leo kimedhaminiwa na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za serikali ambazo nazo zina binadamu na wanaweza kufanya makosa na wakashindwa kuwashughulikia.
"Leo tumekuja tuna wadhamini kama watano sita wametudhamini, lakini kama jeshi la polisi kikao kama hiki tunatakiwa tukifanye wenyewe, tujipange wenyewe,” amesema Rais Samia na kuongeza; "Waliodhamini leo ni taasisi mbalimbali za serikali na ambazo si za kiserikali, zina wanadamu wanaweza wakafanya makosa mkashindwa kuwashughulikia, kwa sababu wamewadhamini, mkutano kama huu mfanye kwa uwezo wenu wa Jeshi la Polisi, mjipekue mifukoni mfanye kikao."