benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa jumla ya shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kuwezesha na kukuza shughuli za ufugaji wa Samaki kwa njia ya vizimba miongoni mwa vijana ili wanufaike na uchumi wa buluu uliopo kwenye ukanda wa Ziwa Viktoria.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na vijana ambao wamepata mafunzo ya ufugaji samaki katika vizimba akiwa katika ziara yake aliyoifanya Wilayani Buchosa, Mkoani Mwanza amesema fedha zilizotolewa ni fursa kubwa kwa vijana kujipatia ajira na kuondokana na kutegemea uvuvi wa asili ambao uzalishaji wake ni mdogo
Mradi huo wa vizimba vya Samaki utazalisha tani elfu Arobaini (40,000) za samaki ambazo zitaongeza uzalishaji kwa sababu mahitaji ya samaki ni makubwa sana.
Katika hatua nyingine, Waziri Ulega alisema mwaka huu pia Serikali itawakopesha wavuvi nchini kote boti za kisasa zaidi ya 150 ili waweze kuboresha shughuli zao na kuongeza uzalishaji wa samaki. Boti hizo zitafungamanishwa na teknolojia za kisasa zitakazomsaidia mvuvi kurahisisha shughuli za uvuvi.