Rais Samia apeleka bil 20 kukuza uvuvi ziwa Victoria

Uandishi wa habari tangu awamu ya tano iingie, ni shida sana. Pesa hizi ni kodi zetu wananchi inayokusanywa na serikali.
Andika Serikali imetoa.. Sio fulani ametoa.
 
Mama fukuza kazi Waziri wa Mifugo na Uvuvi pamoja na mkurugenzi wa TADB,hawa wanaenda kuvuruga mradi wa ufugaji samaki kwa kutumia vizimba. Sisi tulikwisha toa oda za vizimba vya kisasa nje ya nchi, wao wanalazimisha kutuuzia vya kwao.

Vizimba vyao havina ubora tunaotarajia lakini pia wameweka bei za juu sawa na hivyo tulivyopanga kuagiza nje ya nchi. Hasara ikitokea itakuwa ni yakwetu ama Serikali? Huu mradi hautakuwa na tija yeyote kama ilivyopangwa, tafadhali mama waweke pembeni wapiga dili hawa.

Kila wakati tumesisitiza vizimba tunavyohitaji kuwekeza kwenye ufugaji wa samaki picha zake ni hizi hapa chini, lakini hadi sasa Mama bado hatujalipwa hizo pesa na mwezi huu unaelekea mwisho sasa. Hiyo mwezi Juni mwakani wanataka waje na tathimini za kupika? Muda unazidi kwenda.

 
Wanapewa kina nanani! Asijekuwa kaanzisha biashara kama mtoto wa Mseveni Uganda nzima kaiteka kwa vifaa vya uvuvi usiponunua vifaa kwake ukiviweka majini havirudi.
Uko sahihi ndugu, haya mambo ndio yanataka kutukumba kwenye huu mradi. Watendaji wa serikali hawashikiki kabisa, kila mtu anataka kufanya biashara kupitia walengwa wa mradi huu.

Hali ni mbaya sana
 
Pesa imepelekwa lini? Wameisha anza kupatiwa hiyo pesa au hadi mwaka utamalizika wakizungushwa tu? CCM hopeless kabisa.
Tunapigwa danadana tu ndugu, bado Waziri na Mkurugenzi wa benki wanatafuta njia ya kuzipiga kwanza.
 
Umeongea vizuri mkuu,mama kawajaza wahuni na watoto wa Mjini ,pamoja na huyo waziri wa uvuvi ,wengine ni Hawa ambao wanatakiwa kuondoka KWENYE baraza la mawaziri

Mwigulu
Makamba
Nape
 
Umeongea vizuri mkuu,mama kawajaza wahuni na watoto wa Mjini ,pamoja na huyo waziri wa uvuvi ,wengine ni Hawa ambao wanatakiwa kuondoka KWENYE baraza la mawaziri

Mwigulu
Makamba
Nape
Mradi umeharibika kabla ya kuanza rasmi
 
Hivi bilioni ishirini tunazijua?. Imefikia wakati ambao serikali inabidi iwe inatoa mchanganuo wa jinsi ambavyo fedha hizi zinatumika.
 
Hivi bilioni ishirini tunazijua?. Imefikia wakati ambao serikali inabidi iwe inatoa mchanganuo wa jinsi ambavyo fedha hizi zinatumika.
Wamejipanga kuzipiga ndugu, kwa kifupi huu mradi wa ufugaji samaki kwa kutumia vizimba hauna tofauti na ule mradi wa mtoto wa Mseven kule Uganda. Tumepigwa na hatuna la kuwafanya
 
Ni kweli, Mama hadi leo hii ameshindwa kumfuta kazi Waziri Mashimba Ndaki kwa kuhujumu mikopo yetu ya ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba hapa Mwanza.
Tangu wadanganye kwa mabango makubwa kwamba Rais Samia ametoa bilioni 20 kwa wavuvi wa samaki, hadi leo hii hakuna chochote ndugu zanguni. Hakuna pesa yoyote ambayo imetufikia wavuvi na Mama amekuwa mzito kufanya maamuzi

 
Hatimaye nyinyi WABABAISHAJI mumetupwa nje, afadhali tupumue sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…