peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi ripoti iliyopita ilifanyiwa kazi au ipo kabatini kama zilizopita?Kuna usemi kwamba "Ya kale ni dhahabu. Model ya Magufuli itakumbukwa daima" Mama alipochukuwa nchi alisema hataki watu kuonewa akawaachia huru mafisadi waliowekwa ndani na serikali ya Magufuli (japo ela za Plea Bargaining zilizokuwa kwenye subira ya mchakato wa kisheria kuliwa nyuma ya Magufuli kufariki).
CAG Assad alipumzishwa kwa ripoti kama hizi hizi za CAG Kichere. Sijajuwa kama Kichere ataendelea kuvumiliwa hadi lini.
Mama hata kama hapendi mafisadi walio kwenye ripoti ya Kichere kushughulikiwa (kuonewa) lakini tayari CCM kimeshindwa kuvumilia na kuagiza serikali kuwachukulia hatua wahusika wote.
Pasina kujali udhaifu wa Mhimili wa Mahakama yetu lijapo suala la rushwa katika kufanya maamuzi ya mashauri, ni dhahiri kwamba mama sasa ana kigugumizi cha ni kwa vipi nilitoa mafisadi jela alafu leo tena niwarudishe jela ama wale wale au hata kama ni mafisadi wapya!
Huu ni mfupa mgumu kwa mama na huenda hata kwa CCM kilichompa maagizo kuwachukulia hatua za kisheria.
Dondoo chache kwenye ripoti ya CAG 2022 - 2023:
1. TTCL imekopesha watu wasiojulikana 21 bl.
2. Mkurugenzi Mkuu na maafisa wengine waandamizi wa TPA ambao wote waliondolewa kazini kwa utendaji mbovu bado wanaendelea kuidhinisha malipo kwenye mfumo wa TPA.
3. Takriban V8 mpya 40 za serikali zilizoagizwa zimeyeyuka bandarini.
4. CAG hakusaini (alirukwa) baadhi ya mikataba ya manunuzi makubwa ya kimkakati ughaibuni kama sheria inavyotaka.
Kwa ripoti hii ya CAG Kichere nchi inaenda wapi wakati wapigakura wanakula mlo mmoja? Mchele mbovu (chenga 3,100/)
Tujadili kwa ustaarabu kwa kujifunza kitu siyo kwa kushindana maana nchi ni yetu sote.View attachment 2579909
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] Wenje kabisaaa...Hata Chadema wameanza kuona maridhiano yao na ccm nchi inaelekea kusiko
Tena Chadema watalaumiwa kuridhiana na chama ambacho kinayafuga haya. Bora Chadema wajiondoe kwenye maridhiano kungali mapema.Hata Chadema wameanza kuona maridhiano yao na ccm nchi inaelekea kusiko
I like your reasoning.Hivi ripoti iliyopita ilifanyiwa kazi au ipo kabatini kama zilizopita?
Tunajadili nini kama haziwaumi watawwla wenye kuweza kuchukua hatua?
Tusubiri Mungu aimalize CCM kabisa ndo tutakuwa na mwanzo mpya
Chama cha kupigia pesa.CCM ni CHAMA Cha majizi sana.
Ripoti ya mwisho ya CAG ni ya ubadhirifu ambao viongozi (Menejimenti na Bodi; Wakurugenzi wa Halmashauri, Mawaziri na Makatibu Wakuu) walishindwa kutoa majibu. Halafu Rais anawapa nafasi ya ati kuchunguza wahusika? Wafutwe kazi na TAKUKURU/Polisi wafanye kazi yao ili wasitafute watu wa kuwatwisha uchafu huo au kuficha ukweli.Angalia walivyopiga pesa.ila kwakuwa watanzania hamjali hata Mimi nikipata nafasi nitapiga pesa[emoji23][emoji23]View attachment 2582662
Nasema ivi nasema ivi...IMEISHA HIYOO.Umeshaambiwa mtu anadai halafu hajui anayemdai mzee...!
IMEISHA HIYO.
Nasema ivi nasema ivi...IMEISHA HIYOO.