Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Najaribu kuwaza kwa Sauti kama sio Rais Samia Suluhu leo Tanzania tungekuwa wapi?Suluhisho ni bima ya afya kwa kila mtanzania hapo ndio ntaamini hangaya bado hajachoka anazipiga ndefu ndefu ...auze hata mabombadia ma tano tupate bima mzigo auweke nssf
Ungejua mpango umeanza lini wala usingekuwa unasifia tu kila kitu.Kwani yeye ndio wakwanza kutawala Tanzania?
Mbona hatukuwa na hizo dialysis machine?
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,
Majungu haya tu, Sijaandika muda sanaMwezetu CM 1774857 maisha yako mazuri sana.Unanyuzi zaidi ya tano wiki hii za kusifia wakati wezako tunawakiwa na jua.
Yuko wapi kada kichaa?Kada kichaa pamoja sana
WaooohRais Samia apunguza gharama za matibabu ya figo kwa 66% kutoka TZS 300K mpaka 100K || Tanzania kununua mashine 7,000 kwaajili ya dialysis
" Hakuna kama Samia "
Dialysis ni kitendo cha kuondoa Sumu,Uchafu na ziada ya maji kwenye damu ya binadamu baada ya figo kufeli kufanya kazi hiyo au simply ni kitendo cha kupitisha damu kwenye mashine ili isafishwe,
Rais mnyenyekevu Samia Suluhu Hassan ametangaza kushusha bei ya matibabu ya figo ( dialysis) kwa watoto wa masikini wa nchi kwa karibu 70% kutoka Tshs 300,000 ya Sasa mpaka chini ya Tshs 100,000,Mnaposikia tunasema Rais Samia anahuruma kwa watu wake huwa tunamaanisha mambo haya,
Rais Samia pia kupitia MSD ameahidi kununua zaidi ya mashine mpya 7,000 za dialysis kwaajili ya Vituo vya kutolea huduma elfu 7 na hii ni baada ya Rais Samia kuzia wizi na ubadhilifu kwenye manunuzi ndani ya MSD kwa karibu 50% ya gharama.
Rais Samai amegundua hivi,mashine iliyonunuliwa kwa Tshs 100M kabla ya Rais Samia sasa inanunuliwa kwa Tshs 55M tu |Fungua hiyo Video chini umsikilize vizuri Director General wa MSD Maj. Gen. Dr. Gabriel Sauli Mhidize|
Taarifa za shirika la afya duniani ( WHO ) za mwaka 2018 zinaonesha jumla ya vifo 2,636 sawa na 1% ya vifo vyote Tanzania vilitokana na matatizo ya figo hakika Rais Samia ubarikiwe,
View attachment 1951660
VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA