Rais Samia asema itungwe Sheria itakayotoa muongozo kuwashughulia viongozi wanaofanya majukumu ambayo sio yao

Nina uhakika hujasikiliza kilichosemwa
Ulitaka wakati nasikiliza na ww uwepo pembeni? Nasema hivi, hiyo ripoti ni upotevu wa rasilimali muda na fedha kwani hakuna kitakachotekelezwa. Hiyo sio tume ya Kwanza kuundwa, na huwa hatuoni utekelezaji wowote wa maana.
 
Yeye mwenyewe Samia kampa Waziri Mbarawa mamlaka ya kusaini mkataba wa DPW kwa niaba ya serikali ya Dubai, kitu ambacho si kazi yake Samia.

Waanze naye kwanza.
 
Binafsi, na kwa miaka mingi tu, nimekuwa nasisitiza kurejea Sheria zote za Kikoloni na ikibidi, ziondolewe kabisa, yaani kufumuliwa na kutungwa upya kwa kutumia lugha zetu(kiswahili) (za makabila)huku zikizingatia Mila na Desturi zetu-Filosofia ya Uafrika ya kujali Utu.
Tunaweza.

Tunalaumiana kwa sheria zilizowekwa mahsusi kwa ajili ya kututawala, huku tukiacha kwa makusudi kusema kuwa "tumerithi sheria za kikoloni, Mfano.mdogo ni ile ya sheria ya Mkusanyiko![Nakushauri utafute chanzo cha sheria hii upate kuridhia mantiki ya waasisi wa sheria hiyo ambayo tuliiacha itutawale] yaani tunaacha kwa makusudi, isitoshe kwa uoga kusema "tumekosea" kuwaachia wazungu watutawale kwa remoti kwa sheria zao za kale!



Waafrika, mifumo yetu ya Sheria, miuondo yetu ya Kiserikali have been documented, tuangalie huko nyuma, -historically- tulifanyaje?? Je , Tunaweza kukwapua misingi ya sheria tulizoziasi na kuacha kwa mtutu wa bunduki(maxim gun) na kuweka zile tunazozitaka?

Nafikiri itakuwa ni vyema kabisa, kutambua juhudi kubwa na pana katika harakati za kujikomboa(kwa maana zote), kutoka minyonyoro ya Ukoloni(Kifikra,Kisiasa,Kijamii,na Kiuchumi)vilevile kutambua na kutoa kongole kwa Tume hii iliyokuja wakati muafaka.

Nasita kusema tumejinajisi, nathubutu kusema no to Neo-Colonialism. Heko Watanzania.

Tuachane na sheria kandamizi, zilizojaa unyanyasaji na unyanyapaa.Tunaweza.
 

Rais Samia asema itungwe Sheria itakayotoa muongozo kuwashughulia viongozi wanaofanya majukumu ambayo sio yao​


Hakika! Wakati wanatafakari hilo, nawashauri Wabunge wetu waanza kufukiri ni Jinsi gani pia; tutakavyoweka ukomo wa Chama Tawala, kukoma kufanya maamuzi kamavile-Kuingia mkataba kama huu wa DPW ambao unaviiashiria vya Rushwa miaka miwili kabla ya Uchaguzi. Yaani iwe marufuku kwa Chama madarakani Kuwakaribisha wawekezaji, Kuwekeza katika miradi yeyote mikubwa inayozidi 1/3 ya Mapato yetu ya Miaka 10. Iwe marufuku kuanzisha Mradi wowote mkubwa utakao husisha Serikali kukopa kwa mahususi kwa mradi huo. Kwa lugha nyepesi Serikali isiingie au kufanya Mradi wowote mkubwa miaka miwili kabla ya Uchaguzi mkuu.
 
Wamefanyia kazi mapendekezo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…