SI KWELI PreGE2025 Rais Samia asema 'Siwezi kuahirisha kuchukua fomu ya kugombea urais kwa sababu ya msiba wa Ndugai'

SI KWELI PreGE2025 Rais Samia asema 'Siwezi kuahirisha kuchukua fomu ya kugombea urais kwa sababu ya msiba wa Ndugai'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
RAISSAMIA09AG2025.jpg
 
Tunachokijua
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Januari 19, 2025 ulimpitisha kuwa mgombea wa nafasi ya Urais huku Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mgombea Urais wa Zanzibar.

Agosti 8, 2025 Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Amos Makalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma aliweka bayana kuwa mgombea Urais kwa tiketi chama hicho Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea mwenza Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi watachukua fomu Agosti 9, 2025 katika ofisi za INEC.

“Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, na Mgombea Mwenza, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kesho Agosti 9, 2025 wataenda Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuchukua fomu kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025."

Awali Agosti 06, 2025 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kupitia taarifa kwa umma alitangaza kifo cha aliyekuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mbunge wa Kongwa, kilichotokea Agosti 06, 2025 jijini Dodoma na kueleza kuwa Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi.

Madai

Ipo Picha iliyochapishwa Facebook ikiwa na ujumbe unaoonekana kuchapishwa na Rais Samia katika mtandao wa X ambapo sehemu ya ujumbe huo unasema 'Siwezi kuahirisha kuchukua fomu ya kugombea urais kwa sababu ya msiba wa NDUGAI'

Je ni upi uhalisia wa ujumbe huo?


Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa ujumbe huo haujachapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Rais Samia kupitia mtandao wa X.

Ujumbe huo ni wa kutengenezwa na wapotoshaji kwani yapo mapungufu kadhaa, ambapo picha yenye ujumbe huo haiakisi uhalisia kama ilivyo katika mtandao wa X. Mfano kutumika kwa tiki ya bluu (blue checkmark) badala ya tiki yenye rangi ya kijivu (Grey checkmark) ambayo inatumiwa na Rais Samia.

Kukosekana kwa alama ya Grok, nukta tatu zilizopo upande wa juu kulia zina maumbo ya mraba badala ya duara. Umbo la picha katika sehemu zenye kona ni tofauti na machapisho kutoka mtandao wa X.

Hivyo, ujumbe huo si wa kweli bali ni wa kutengenezwa na wapotoshaji. JamiiCheck inakukumbusha kutokusambaza machapisho, picha au video ambazo unapata mashaka kuhusu uhalisia wake kabla ya kuthibitisha ili kuepusha upotoshaji.​
Back
Top Bottom