Rais Samia ashiriki hafla utiaji saini Mkataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe leo tarehe 30 Septemba, 2022

Rais Samia ashiriki hafla utiaji saini Mkataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe leo tarehe 30 Septemba, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki hafla utiaji saini Mkataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe leo tarehe 30 Septemba, katika Jengo la Kitega Uchumi jijini Dodoma



Ummy Mwalimu - Waziri wa Afya
Lishe bora ni msingi wa afya na uchumi wa mtu mmoja, familia na taifa kwa ujumla.

Utapiamlo unaleta madhara kiafya na kiuchumi, lishe bora ni muhimu.

Madaraja na miundombinu mingine inaweza kukarabatiwa baada ya kuharibika, ubongo wa mtoto hauwezi kukarabatika baada ya kuharibika.

Watoto milioni 3 Tanzania wamedumaa, hawafundishiki. Ubongo wao umedumaa, hawawezi kuwa wabunifu, hawawezi kujifunza mambo mapya.

Tunaanza kutoa kozi ya afisa lishe ngazi ya Astashahada kuanzia mwaka 2022/23 ili tupate wataalamu wengi wa kusimamia ajenda za lishe hadi sehemu ya chini kabisa.

Tuna tishio la ugonjwa wa Ebola ulio anzia Uganda. Tumetoa maelezo kwa wakuu wa mikoa, tuendelee kujipanga ili usiingie, na hata ukitokea umeingia tuweze kuudhibiti.

Innocent Bashungwa - Waziri TAMISEMI
Tumepokea pesa ya ujenzi wa madarasa 8000 nchi nzima. Zoezi hili tutalisimamia na kulitekeleza kwa ufanisi mkubwa.

Samia Suluhu Hassan - Rais
Nimezungumza na Waziri wa afya tusitishe kwanza ujenzi wa vituo vya afya, kwa sasa tuimarishe huduma kwanza pamoja na kuwekeza vifaa tiba ikiwemo pia kujenga nyumba za wahudumu.

Kasimamieni matunzo ya vifaa hivi vilivyo tolewa. Sitavumilia kusikia kifaa miezi 6 au mwaka mmoja kimeharibika. Aliyehusika atanieleza, na mtumiaji atanieleza.

Simamieni vizuri mkataba huu wa lishe ili matokeo tunayopanga yaweze kutimia.

Wajawazito wapewe lishe bora ili wazae watoto wenye afya bora, watoto hao nao wakizaliwa watunzwe vizuri ili baadae wawe watu wazima wenye afya bora.

Uchunguzi ufanyike kwanini vijana wetu wakifikia umri wa kuongeza jamii wanahangaika, ni mitindo ya maisha (kuwa slim lady) au utasikia supu ya pwenza….. tatizo kubwa hili, lipo kwenye lishe. Watafiti kachunguzeni.

Tukiacha mambo yaende hivi tutakuwa na taifa la watu goigoi, itafika mahali hatutajua mke ni nani na mme ni nani.

Tuna vitambi, udumavu na wengine wana uzito mdogo, vyotr hivi ni matokeo ya lishe mbaya.

Tuna changamoto ya uelewa mdogo kuanzia ngazi ya juu hadi kwa jamii ya chini kabisa, tujikague kwanza sisi watu wa juu, tunaelewa kweli haya mambo?

Hata huku juu tuna matatizo, unamuelekeza mtu jambo lilelile mara tano, bado haelewi. Unawaza, ni dharau, hataki au shida nini? Kumbe hujui historia yake (ya ukuaji)

Sekta ya kilimo iangaliwe upya, watu walime na wapate lishe ya kutosha. Ndiyo maana mwaka huu bajeti tumeiongeza zaidi.

Hatuna sababu yoyote ya kusingizia kwa nini tuna shida ya utapiamlo, tuna mito, ardhi nzuri, mvua n.k Twendeni kushughulikia haya mambo.

Fortification ya mazao na vyakula ifanyike kuanzia ngazi ya chini.

Swala la lishe linamgusa kila mtu, nataka nipate ripoti za lishe kila robo mwaka. Vijana wanakula sana chips, lakini mwisho wa siku vumbi la mkongo linahusika.

Wakuu wa wilaya hamfanyi kazi, mnasubiri mkeka. Sikusema nitawabadilisha leo au kesho, kwahiyo kama hamfanyi kazi hao ndiyo wangu.

Kutoa mkeka ni kazi yangu na nitautoa wakati muafaka, wakuu wa mkoa nataka ripoti za wakuu wenu wa wilaya.
 
Hebu anayefahamu atoe ufafanuzi kidogo juu ya hilo "shughuli za lishe"...maana wengine hatujui kama lina uhusiano na hawa kina Mama Lishe wetu au ni suala la Mabwana Lishe na Mabibi Lishe, au ni tofauti na hayo?.
 
Hili ni jambo jema sana!

Angeweka tozo ili kuboresha lishe ya watoto wetu mashuleni hapo ningemuelewa sana.

Lishe bora inajenga Taifa la watu wenye akili!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki hafla utiaji saini Mkataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe leo tarehe 30 Septemba, katika Jengo la Kitega Uchumi jijini Dodoma


huyu Mrisho Mpoto ana mbwembwe!
Mimi sionagi hata Cha maana anachoimba, ni kwakuwa ana connection tu ya kutumbuiza kwenye hafla za serikali
 
Kunywa sumu dada, ndio Rais wako huyo Hadi 2030 inshallah
Unaniletea taarabu yako unafikiri na mimi nimetokea Kojan eeh! Mimi niko Milimani huku Usambaani!! Huku sisi tunacheza mdumange! Ndiyo ngoma yetu kuu.

Halafu hiyo 2030 atafika kwa mkataba na Mungu, au shetani?
 
Unaniletea taarabu yako unafikiri na mimi nimetokea Kojan eeh! Mimi niko Milimani huku Usambaani!! Huku sisi tunacheza mdumange! Ndiyo ngoma yetu kuu.

Halafu hiyo 2030 atafika kwa mkataba na Mungu, au shetani?
Usipanic bibie, ndiomaana nikamalizia na neno 'insha'llah"
It means "Mungu akipenda"
 
Udumavu kwa watanzania upo kwa kiwango cha juu sana, kuna vijana wa kati ya miaka 25 hadi 30 walihudhuria usaili mahali fulani.....aisee nilishangaa karibia wote wana miili midogo midogo. Niliona hii si kawaida, lazima ni tatizo la udumavu kutokana na lishe duni. Chukulia kijana wa kizungu ambaye ni teenager (miaka 13-19) angalia umbo lake ulinganishe na kijana wa kitanzania anayekaribia miaka 30, utashangaa.

Swala la lishe kutoka umri wa mwaka mmoja hadi miaka 18 ni very critical kwa sababu ndo umri ukuaji unapofanyika kwa kiwango kikubwa, kwa hiyo lishe ikizingua hapa ndo inakuwa imetoka hiyo. Hivyo ni muhimu elimu itolewe na watu wawe na uwezo kuwapa lishe stahiki watoto wao wa hadi miaka 18. Vinginevyo watu waelimishwe kuzaa si kufyatua tu kama matofali wakati huna uwezo wa kutoa lishe stahiki kwa watoto.​
 
Usipanic bibie, ndiomaana nikamalizia na neno 'insha'llah"
It means "Mungu akipenda"
Unatafuta mume tu wewe bila shaka. Na kwa bahati mbaya sasa sina desturi ya kuokoteza makapi yaliyoachwa na wanasiasa.

Kutwa kazi kurembua macho tu. Sijui huwa mnakula urojo kupitiliza!!
 
Kwahiyo vumbi la mkongo lirudi lisirudi?
 
Hebu anayefahamu atoe ufafanuzi kidogo juu ya hilo "shughuli za lishe"...maana wengine hatujui kama lina uhusiano na hawa kina Mama Lishe wetu au ni suala la Mabwana Lishe na Mabibi Lishe, au ni tofauti na hayo?.
Mkuu hao ni wataalamu wa chakula( Nutritionists au Food scientists)
 
Udumavu kwa watanzania upo kwa kiwango cha juu sana, kuna vijana wa kati ya miaka 25 hadi 30 walihudhuria usaili mahali fulani.....aisee nilishangaa karibia wote wana miili midogo midogo. Niliona hii si kawaida, lazima ni tatizo la udumavu kutokana na lishe duni. Chukulia kijana wa kizungu ambaye ni teenager (miaka 13-19) angalia umbo lake ulinganishe na kijana wa kitanzania anayekaribia miaka 30, utashangaa. Swala la lishe kutoka umri wa mwaka mmoja hadi miaka 18 ni very critical kwa sababu ndo umri ukuaji unapofanyika kwa kiwango kikubwa, kwa hiyo lishe ikizingua hapa ndo inakuwa imetoka hiyo. Hivyo ni muhimu elimu itolewe na watu wawe na uwezo kuwapa lishe stahiki watoto wao wa hadi miaka 18. Vinginevyo watu waelimishwe kuzaa si kufyatua tu kama matofali wakati huna uwezo wa kutoa lishe stahiki kwa watoto.​
Nkuunga mkono mara kumi. Nchi yetu hata wachezaji wa mpira huwezi kujua kama ni wanamichezo. Choka mbaya kweli kweli. Ila rais yeye kaona athari za kudumaa kwenye nguvu za kufanya mapenzi na hakuona kwenye akili na mwili ambavyo ndivyo vinaathiri zaidi.
 
Back
Top Bottom