Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
- Serengeti Girls ni Mashujaa WetuLeo ni siku nyingine ya furaha sana, si kwangu binafsi bali kwa taifa zima, tunapokutana hapa Ikulu na mabinti zetu mashujaa - Serengeti Girls.
Hii ni rekodi mpya ambayo haijapata kutokea kwa miaka 62 ya Uhuru wetu. Serengeti Girls hongereni sana.
Pia nitoe pongezi kwa viongozi wenu waliosimamia mechi na benchi zima la ufundi. Leo Taifa linajivunia, haikuwa rahisi.
Ushindi wenu umekuwa wa kujivunia sana pale mlipowatandika Cameroon, nchi yenye sifa zote za mpira wa miguu kwa wanawake na wanaume. Lakini Mungu alisimaam nasi mkawapa matano yao na sisi wakatupatia zawadi ya moja wakasepa.
Lakini timu hii imefuzu kushiriki Kombe la Dunia si tu kwa mpira wa miguu wa Wanawake hapa Tanzania, bali hata kwa Wanaume hawajawahi kushiriki Kombe la Dunia la Mpira wa Miguu.
Nafahamu juhudi zenu zilipelekea kuzifunga timu kama Burundi (5-2), Botswana (11) kila mmoja mlimpa goli lake. Na Cameroon pamoja na visa vyao mliwaachia 5 zao. Kwakweli mmeliweka Taifa mahali pazuri.
- Clara Luvanga na Rejodi ya Kipekee
Pamoja na ushiriki wa timu nzima, nimtambue binti yangu Clara Luvanga. Clara amemaliza mashindano haya akiwa na rekodi ya kipekee ya kuwa mfungaji bora barani Afrika kwa michuano hii ya U-17 kwa kumaliza akiwa na magoli 10. Si Afrika tu, naambiwa umeweka rekodi duniani kwa kuwa mfungaji bora namba 2. Upo nyuma kwa magoli mawili tu kwa yule aliyechukuwa rekodi ya dunia.
Na yale mengine ya kukukagua yasikusumbue, wewe mtindo mmoja. Huko tunapokwenda ni hivyo hivyo, watu hawakuzoea kuona Tanzania tuna-perform. Hata mlipo-perform pale Nairobi, Kenya walisema mara tumewapa madawa.
- Sasa Watatutambua Tanzania ni Nani
Hawajazoea kuona Tanzania inakwenda hivyo, ila kuanzia sasa watatujua sisi ni nani. Kwa ujumla Serengeti Girls mmedhihirisha kuwa mnaweza na mmetupatia heshima kubwa sana.
Bunge lilikuwa sahihi kwa lile walilowafanyia; kwa kuwapa heshima maalum kwa kutengua kanuni kuwaruhusu kuingia ndani ya Bunge. Mlistahiki kupewa heshima ile. Na kwa hilo nimpongeze pia Spika wa Bunge kwa kuwatambua.
Timu yenu itabaki kwenye kurasa za historia ya nchi hii kwa kufika mlipofika.
- Wizara ya Michezo Inachemka
Wizara tangu mmeingia viongozi ninyi, inachemka na tunaona. Matamasha hayakauki, michezo inakwenda mbele. Mpaka Tanzanite kama daraja mmeuza duniani. Kwakweli kuna ubunifu mkubwa lakini siri ya hili ni mashirikiano baina ya viongozi ndani ya Wizara na mashirikisho mbalimbali ya michezo.
Na mkiendelea hivyo, basi mtaona Tanzania ikipiga hatua. Najua hini ya wizara kuna Bararaza la Michezo (BMT) na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wanaosimamia michezo hususani mpira wa miguu.
-Tutafakari Mafanikio Zaidi
Pamoja na haya tusiishie tu kufurahi, bali pia tutafakari. Tutafakari ni ipi misingi na siri nzito ya mafanikio haya ili tuweze kupata mafanikio mengi makubwa zaidi. Kwa maoni yangu, la kwanza nilishalisema – lile la ushirikiano. La pili nadhani mafanikio haya yametokana na uwekezaji ambao untakiwa kufanyika kwa serikali kuanza kuchanga fedha kidogo kidogo kwa ajili ya timu zetu. Kwnye mifuko hii tuweke fedha zitakazohudumia timu zetu hususani pale zitakapokwenda kwenye mashindano ya kimataifa.
Lingine ni hamasa ya michezo na ameisemea vizuri Katibu Mkuu. Kwamba watoto wetu hawa waliwekwa hamasa. Na naiomba Wizara iendelee kuwajenga watoto wetu, si tu Serengeti Girls, lakini hata timu nyingine.
Na tujenge sasa Jamhuri ya Wapambanaji. Huko kwenye mitandao kuna Jamhuri ya Twitter, na sisi tujenge Jamhuri ya Wapambanaji.
- Tutunishe Mfuko wa Maendeleo ya Michezo
Ili kuendelea kuimarisha mfuko wa maendeleo ya michezo, na tusiwe tukawa tunatafutana ili kutafuta pesa za dharura, naziagiza Wizara ya Fedha na Wizara ya Michezo make nakupitia upya. Wabunge mpo hapa muwasaidie kwakuwa matokeo yanaonekana, ingekuwa ile ya zamani ya pigapiga tu, hapana.
Jambo lingine, muwe wabunifu kuangalia vyanzo vingine vya fedha mbali na Serikali na ule mfuko wa michezo.
- Serengeti Girls Msiogope Wapinzani, Mpo Vizuri
Serengeti Girls mtaenda India, yale ni mataifa makubwa ukilinganisha na sisi. Lakini hata Cameroon wanawekwa kambini vizuri kuliko sisi lakini tukawashinda, kwahiyo tusiogope. Hawa ni wakubwa kwa majina lakini kwa uwezo wa nguvu za miguu na kasi ya kwenda mbio ndani ya uwanja, mtawafunga.
Kubwa ni mazoezi. Lakini, kwa viongozi mnaowasimamia, diet. Ile diet ya kimataifa inayotakiwa wachezaji hawa wale. Wapewe diet hiyo. Wapewe mazoezi ya kutosha. Wapewe moyo ili waweze kwenda kufanya vizuri.
- Miundombimu ya Michezo
Nafahamu miundombinu ya michezo bado ni tatizo kwahiyo hili nitakaa na Wizara ya Fedha tuone kama tunaweza tukatafuta fedha za haraka kukarabati au kujenga baadhi ya miundombinu ili kuruhusu michezo kuja kuchezwa nchini au wachezaji wetu wacheze kwenye viwanja vyenye hadhi kama vile wanavyokwenda kuchezea nje.
Kwahiyo hilo nalo tutaliangalia na juhudi zinafanywa kama alivyosema Waziri. Kuna viwanja vipwya vitajengwa, vizuri. Kwahiyo hilo nalo tunaliangalia.
- Dodoma na Tanganyika Packers
Jingini ni kujenga Sports Arena Dodoma. Najua mtatumia lile eneo la Nanenane, najua ni pazuri, pakubwa na panafikika. Kwa Dar es Salaam inawezekana kwa kujenga kule Uwanja wa Mkapa ni mbali lakini muone namna ya kushauriana vizuri na Wizara ya Ardhi namna ya kutumia eneo la Tanganyika Packers kama itawezekana kulitumia.
Najua emneo lile lina utata wa umiliki wake lakini tutaangalia Serikalini kama ule utata tunaweza kuuondosha na litumike kujenga hiyo Arena. Panafikika zaidi. Hii itakuwa ni distribution ya maeneo ya michezo ndani ya jiji letu la Dar es Salaam.
- Wadau jitokezeni kudhamini timu \ Harambee
Jambo lingine ni kwamba mafanikio haya ni kwa taifa lote, kwahiyo niwaombe wadau wajitokeze kuzidhamini timu hizi na matukio ya michezo kwa ujumla.
Nitamuagiza Waziri Mkuu ambaye ni mwanamichezo mwenzenu aniwakilishe katika Harambee kubwa itakayofanyika mwezi ujao ya kuwaleta pamoja wadau wote – sekta binafsi na taasisi za umma. Mimi mwenyewe pia nitachangia, sisemi ni kiasi gani lakini nitachangia kwa uzito kidogo.
- Michezo Itangaze Utalii
Jingine niseme kwamba michezo ni jambo kubwa la kuitangaza nchi na hivi karibuni tumetangaza kampeni kubwa ya kuitangaza nchi yetu kupitia Royal Tour.
Niagize Wizara na Mwenyekiti wa Royal Tour kwamba kwa kushirikiana na watu wa Utalii wachezaji wetu hawa na wengine wanapokwenda kushiriki michezo ya kimataifa wasiende kinyonge kabisa. Kwa kila wanachovaa na kwa kila kinachoruhusiwa wakaitangaze nchi na vivutio vyake mbalimbali.
Jezi zao wanazovaa lazima ziendane na alama zetu lakini zaidi ni ile meseji yetu. Kuna meseji tofauti: Tanzania Unforgettable, Visit Tanzania n.k. Kaeni muone mnaenda na meseji ipi. Kuwe na uniformity; timu zozote zitakazokwenda meseji iwe hiyohiyo moja na wasiwe wanyonge.