Kichaa ni wewe mkuu, fanya umuone daktari mapema iwezekanavyo.
Nchi kuwa na matatizo au wewe kuwa na shida haimaanishi kuwa hakuna watu wenye kufurahia maisha muda huu.
Ndio uendawazimu wenyewe huo, kudhani kuwa shida ni za wote, ni za kwako tu mkuu. Wenye akili hawasemi we have problems wanasema i have problems, matatizo ni ya kwako peke yako mkuu Kaka pembe.
Wewe unavyolia kuna watu wanaziona fursa muda huu na wanazitumia ipasavyo. Watu waliziona fursa wakati wa corona sembuse muda huu!!.
Usidhani kuwa huko Cameroon wanakofuzu kombe la dunia la wanaume kila mara kama hawana matatizo, yapo mengi tu lakini kila wanapopata nafasi ya kufuzu wanaifurahia. Kushangilia mpaka ushinde mechi moja huko ndio upunguani wenyewe kwani unashindwa kuelewa kuwa mpaka kufuzu wameweza kuwatoa washindani ambao ni timu za mataifa walizocheza nazo.
Makasiriko na masononeko yatakuuzesha mapema sana, kuwa mwangilifu sana.