Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma leo tarehe 01 Februari, 2023
PROF. EDWARD HOSEAH, RAIS WA TLS
Mh. Rais, dhana ya Suluhu kutatua migogoro na kukuza uchumi imekuja kwa wakati wake ikiwa ni dhana ya inayotutaka sisi sote kutatua migogoro ya aina mbalimbali kwa njia ya usuluhishi. Kwetu sisi kama akili wa kujitegemea ni dhana pan asana lakini inatekelezeka tukianza kubadili fikra zetu kwa kuelimishana na kuelimisha umma juu ya umuhimu wa usuluhishi wa migogoro nje ya mahakama.
- Suluhu katika migogoro kupalilia amani ya nchi
Mh. Rais, Wananchi wakielewa umuhimu wa suluhu katika migogoro mbalimbali hapa nchini itatimiza maono yako ya kuiweka nchi yetu katika amani na mshikamano. Falsafa yako ya Suluhu kama jina lako lilivyo, inasadifiana sana na Wiki ya Kilele cha Maadhimisho ya Sheria.
Sisi Tanganyika Law Society tunaamini katika suluhu katika kutatua migogoro mbalimbali ya kijamii. Mambo muhimu tumeyaanzisha na kuyatetea na mengine tunaupongeza mhimili wa mahakama chini ya Mh. Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma kwa maono aliyonayo na watumishi wote wa mahakama katika kutatua migogoro mbalimbali kwa njia ya suluhu – yaani alternative dispute resolution.
Pia tunakushukuru na kukupongeza sana Mh. Rais kwa hatua mbalimbali na Madhubuti unazozichukua za kuleta suluhu na viongozi wenzio katika tasnia ya siasa na kukuza demokrasia nchini, hususan uliporuhusu vyama vyote vya siasa kufanya mikutano yake ya hadhara nay a kiofisi kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
Tunakupongeza Mh. Rais kwa kuonesha ukomavu wa kuliongoza taifa letu na dhana yako ya suluhu kama lilivyo jina lako.
- Mawakili wa Kujitegemea watumike kwenye utatuzi wa migogoro
Kama nilivyokudokeza kwenye hotuba yangu yam waka 2022 katika siku kama ya leo, kwmba Mawakili wa Kujitegemea waanze kutumika ipasavyo kwa kutoa huduma hii ya utatuzi wa migogoro mbalimbali kwa suluhu kwani tunao wataalamu wa kutosha kuanza kuifanya kazi hii na kwa kushiriki kwetu kama TLS itasaidia sana kupunguza migogoro mbalimbali ya ardhi, mirathi, ndoa kudhulumiwa na mingine mingi na kuwapunguzia mzigo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wanaotumia muda mwingi kushughulikia migogoro mbalimbali.
- Ushiriki wa TLS utapunguza mlundikano wa migogoro
Kwa ushiriki wetu kama TLS itawapunguzia sana mlundikano wa migogoro ambayo wao wanaishughulikia. Sisi TLS tunaweza kuifanya kazi hii kwasababu tayari tuna chapter 21 nchi nzima. Hatua hii ikizingatiwa kwa umakini mubwa hata mashauri mengi yanayopelekwa mahakamani yatapungua kwa kiasi kikubwa.
Hivyo, ikikupendeza Mh. Rais, itengwe bajeti kila mwaka kupitia TAMISEMI na Wizara ya Katiba na Sheria kuanza mwaka ujao wa fedha 2023/2024 ili dhana ya kutatua migogoro kwa njia ya suluhu ipate kuwa na kasi kubwa na mwitikio wa wananchi kwa kuona matunda yake chanya.
DKT. ELIEZA MBUKI FELESHI, MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa mwaka huu wa 2023 Wiki na Siku ya Sheria inaongozwa na kaulimbiu isemayo: “ Umuhimu wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Usuluhishi Katika Kukuza Uchumi Endelevu – Wajibu wa Mahakama na Wadau”
- Migogoro inatumia gharama kubwa kuitatua
Mh. Rais, sisi sote tunajua na tu mashahidi kuwa serikali unayoiongoza imedhamiria kuona migogoro inayojitokeza nchini inatatuliwa na itaendelea kutatuliwa kwa njia zitakazowawezesha wadau kumaliza tofauti zao mapema na hivyo kujikita zaidi katika uzalishaji/shughuli za kiuchumi kwani migogoro si tu kwamba inatumia gharama kubwa katika utatuzi, bali inafanya mitaji ya uwekezaji kukaa bila uzalishaji uliotarajiwa na hivyo kukwamisha maendeleo yaliyokusudiwa na kuendeleza uadui miongoni mwao.
Mh. Rais, Dhamira ya serikali unayoiongoza inatekelezwa kupitia maboresho yanayoendelea katika sekta mbalimbali nchini yakiwemo yale yanayotekelezwa kwa viwango stahiki na Mahakama ya Tanzania chini ya uongozi wa Mh. Jaji Mkuu, Prof. IIbrahim Hamisi Juma. Maboresho hayo yapo katika nyanja za sheria na rasilimali wezeshi katika maeneo ya miundombini, fedha, watu pamoja na teknolojia.
-Utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala unahitaji kuwekewa mazingira rafiki
Msisitizo wa utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala na usikilizwaji wa mashauri kwa njia za kimahakama, kama ulivyowekewa msingi imara kwenye sheria zetu, unahitaji kuwekewa mazingira Rafiki, jambo ambalo limekuwa likihimizwa sehemu mbalimbali duniani.
Mh. Rais, Mh. Peter Sam Shivute, Jji Mkuu wa Mahakama ya Namibia aliwahi kuandaa wasilisho takribani kiaka tisa iliyopita ambalo alilitoa katika mji wa Livingstone nchini Zambia katika mkutano uliowajumisha waheshimiwa majaji wakuu kutoka kusini mwa bara la Afrika, mkutano ambao ulifanyika tarehe 2 na tarehe 3 Agosti mwaka 2013.
- Mahakama huru ni muhimu katika utawala bora
Tafsiri rahisi ya hotuba ya Mh. Jaji Shivute ilisema hivi: Katika jamii yoyote inayostawi utawala wa sheria unabaki kuwa nguzo katika kukua na kuendelea kwa taifa. Mahakama huru na thabiti ni muhimu katika utawala bora na maendeleo ya kiuchumi kwani tafasiri adili na kwa wakati pamoja na utekelezaji wa haki za kiuchumi vitasaidia kutengeneza mazingira stahiki yanayohitajika sana katika uwekezaji na ukuaji wa uchumi wetu.
Bila kuwa na utawala thabiti wa sheria wawekezaji wataona vigumu na hatarishi katika kuwekeza katika chumi zetu na hivyo kubaki pasipo ukuaji wa uchumi na maendeleo ambayo kanda yetu inahitaji. Mdororo katika kuaminika katika biashara kunahusiana kwa sehemu kubwa na matatizo ya msingi yanaoathiri mfumo wa kisheria kama vile uwepo wa vitendo vya rushwa na utekelezaji wa mikataba pamoja na kutoheshimu haki za kumiliki mali.
- Mfano wa Uholanzi
Uholanzi, kwa mfano, Mahakama inahimiza taratibu za usuluhishi na upatanishi katika kusaidia utatuzi wa migogoro pale inapotokea kutoelewana katika uwekezaji wa kibiashara. Wawekezaji wa kigeni wananufaika kwa sehemu kubwa kuokana na mifumo na vyombo vya utatuzi wa migogoro kama vile usuluhishi, upatanishi na majadiliano kwani pia vinaweza kutoa nafuu stahiki kwa wadau.
Vile vile, uwepo wa vyombo vya usuluhishi, upatanishi na majadiliano katika utatuzi wa migogoro umekuwa na hamasa chanya kwa mahakama pia. Kutokuwepo kwa kile kinachoweza kutafsiriwa kama hodhi ya mahakama katika utatuzi wa migogoro, kunamaanisha kuwa mahakama itapaswa kushindana na vyombo hivyo vingine kwa kudumisha na kuboresha ufanisi wake yenyewe katika kushughulikia mashauri kwa namna bora. Hivyo mahakama na wawekezaji wanapata hamasa kwa mtazamo chanya kutokana na utendaji mzuri wa utatuzi wa migogoro ndani ya nchi.
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Ndugu zangu nimefurahi sana kuungana nanyi kwenye maadhimisho haya hapa Dodoma.
Ni mara yangu ya pili kuja lakini niwe shahidi, nashuhudia mabadiliko makubwa ndani ya sekta hii. Kwahiyo kila ninapoitwa kuwa nanyi, sijisikii vibaya najisikia raha kuwa nanyi.
- Kauli mbiu ya kufurahisha
Mh. Jaji Mkuu na Wadau, niseme nimefurahishwa na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema: “Umuhimu wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Usuluhishi Katika Kukuza Uchumi Endelevu – Wajibu wa Mahakama na Wadau”
Kaulimbiu hii inatukumbusha sote wajibu wa kusaidia ustawi wa taifa letu kwa kuwa na mazingira mazuri ya utatuzi wa migogoro au maelewano. Kwani kama ilivyoelezwa inatilia mkazo maelewano, ambayo ni moja ya mambo tunayoyasimamia katika Nyanja zote katika kuendesha serikali hii.
Serikali imedhamiria kukuza uchumi kwa kukuza fursa za uwekezaji na biashara ambazo zina ushindani nchini na katika ushindani kuna mambo kadha mnajua yanayotokea ambayo mengi yanahitaji usuluhishi na nimefurahishwa sana na hatua iliyochukuliwa n a mipangoiliyopo ya kuleta usuluhishikatika sekta ya biashara.
- Ni muhimu kuimarisha mifumo ya utoaji wa haki
Tumefungua Tanzania kuwa kitovu cha biashara ndani ya ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki lakini hata Kusini mwa Afrika. Na tumekuwa tukivutia wawekezaji kila tunapokwenda nje ya nchi yetu. Na kwa bahati nzuri tumekuwa tukiitikiwa vyema. Sasa wote wanaokuja wanataka kuona haki ikitendeka wanapofanya biashara zao, wanapowekeza mitaji yao na wanapofanya mawasiliano na taasisi mbalimbali za nchi yetu.
Kwahiyo, ni muhimu kuimarisha mifumo ya utoaji wa haki ili iweze kutatua migogoro kwa haraka inapotokea na hapana shaka hili litawavutia wafanyabiashara na wawekezajikwani linalenga imani ya usalama wa mali zao.
- Kuna umuhimu wa kutatua migogoro kwa usuluhishi
Kama Jaji Mkuu alivyosema, kuna umuhimu mkubwa wa kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ambazo hazihitaji sana wahusika kuwa wajuzi wa sheria. Ametueleza vizuri historia yake na ninafahamu kwamba elimu ya usuluhishi imetolewa kwa wiki nzima. Hili ni jambo jema ambapo nataka nitoe wito liwe ni endelevu kutokana na umuhimu wake, hasa katika zama hizi za nadharia za usawa wa kijinsia, uchumi na ushindani.
Imeelezwa hapa kwamba usuluhishi hupunguza gharama za kifedha na hata muda kwa ufuatiliaji wa kesi zinapokuwa kwenye vyombo vya sheria. Na hii ni kutokana na taratibu zao ambazo hulalamikiwa sana na wananchi.
- Haki ikipotezwa amani inapotea
Panapotokea uvunjifu wa amani, haki inakuwa imepotezwa na haki ikipotezwa basi na amani inakuwa haipo. Kwahiyo tujitahidi sana kufanya haki ipatikane mapema ili amani ya nchi yetu iendelee kutunzwa na kuendelezwa. Sisi serikalini tunaendelea na jitihada za kufanya haki iendelee kwa kuipitia upya mifumo iliyopo.
Kama mnavyojua au mlivyoona kwamba jana tu nilizidua Tume ya kufuatilia mienendo ya taasisi za haki jinai itakayoongozwa au inayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Chande na Makamu wake Ndugu Sefue. Hii tume itafanya kazi kwa muda wa miezi minne kuangalia mifumo ya haki na utatuzi wa migogoro inaimarishwa – siyo tu kwa ajili ya kulinda amani na utengamano wa taifa, lakini pia kukuza uchumi kwa hatua za maendeleo.