Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Haya ni baadhi ya mambo yaliyogusiwa kwenye Maadhimisho haya ya Miaka 25 ya Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF);
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi WiLDAF - Monica Mhoja
- Sheria ni nyenzo muhimu katika kuleta mabadiliko hasa ikitumiwa vizuri.
Maombi ya Monica Mhoja kwa Rais Samia kufanyika maboresho kwenye baadhi ya sheria nchini:
- Kuharakisha marekebisho ya sheria ya ndoa 1971 inayodogosha haki ya mtoto wa kike kukosa haki zake kama elimu, kuolewa katika umri mdogo na kukumbana na ukatili wa kijinsia na mikiki ya ndoa ambayo si sawa na umri wao.
- kufutwa kwa sheria za kimila za mirathi ambayo zimekuwa mwiba kwa wanawake na watoto wakike kwa kuwanyima haki ya mali ambazo wanakuwa wamezitolea jasho, kwani pia sheria hizi zinahujumu jitihada za wanawake katika kujikomboa kiuchumi na kuongeza pia sheria hii haiathiri wanawake tu bali hata watoto wa kiume endapo mama zao watanyimwa haki kutokana na sheria hii vibaya sheria hiina hivyo kushindwa kuwahudumia.
- Mapitio ya maboresho sheria ya vyama vya siasa na sheria ya uchaguzi ya taifa. Sheria ya vyama vya siasa haijaweka takwa la kisheria kuvitaka vyama vya siasa kuzingatia usawa wa kijinsia pia sheria ya uchaguzi ya taifa haijaweka utaratibu fanani kuwapata wanawake wabunge na madiwani kwenye ngazi za viti maalum, hii inapelekea vyama vya siasa kutozingatia jinsia kipindi cha uchaguzi.
- Haja ya kutungwa kwa sheria mahsusi itakayoshughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Samia Suluhu Hassan
- Takwimu zinaonyesha asilimia kubwa wanaojishughulisha na kilimo ni wanawake, hivyo sheria ya ardhi ifanyiwe maboresho ili kuwanufaisha pia na wanawake.
- Serikali itayafanyia kazi mapendekezo mbalimbali ya maboresho ya sheria yaliyotolewa na WiLDAF pamoja nawadau wengine.
- Pamoja na sheria kuwepo bado mapungufu ni mengi, hivyo yatazamwe na kufanyiwa kazi.
- Sheria peke yake siyo suluhisho katika katua changamoto mbalimbali kwasababu sheria zipo na makosa bado yanafanywa. Elimu ya jamii kwa watanzania kujua kwa nini sheria zimetungwa na adhabu endapo utakuwa umekiuka sheria hizo inahitajika.
- Sheria zimetungwa na wadau lakini wananchi hawakushirikishwa kuzifahamu na kuzikubali, endapo na wananchi watashirikishwa hata seheria za kimila zitamezwa na mfumo huo. Endapo wananchi wakishirikishwa basi ni wa maeneo ya Dar, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, wengine wanaishia kusikia tu kwenye vyombo vya habari lakini hawazielewi wala kuzifatisha sheria hizo.
- Wakati wa kufanywa mabishano ya sheria jinsi ya kuboresha sheria upande wa sera usiachwe ukiwa unalegalega bali uangaliwe ili kuleta maboresho ambayo yatakuwa na faida kwa waathirika.
- Mtandao wa kinjinsia ndani ya jeshi la polisi upewe jukwaa ambalo wataweza kutoa maoni yao na kusikilizwa bila ya uoga mbele ya viongozi wao.
- Ufanyike utafiti kwenye sheria za kimila kwa sheria mbaya kuachwa na zile sheria nzuri ziongezewe nyama ili ziwe sheria kamili zinazotambulika.
- Kutumia mbinu ya kuwatumia viongozi wa kijamii, kidini na watu wanaokubalika katika jamii kuwaelewesha na kuwawezesha kuelezea sheria na sera kwa wananchi ambapo itasaidia kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na pamoja na kuachana na mila potofu.