Mtoto wa Shule
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 15,133
- 11,914
Tumsamehe tu.Katutia aibu sana huyu bi kigagula
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumsamehe tu.Katutia aibu sana huyu bi kigagula
Naomba nisikujibu.Akirudi ndio watafufuka au?
Weka sahihi uandishi wako! Unamaanisha Nini unapoandikaLeo tarehe 07 Nov. 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania alishiriki mkutano wa 27 wa kujadili mabadiliko ya tabia nchi.
Mkutano huo umefanyika kwenye mji wa Sharm El Sheikh. Rais Samia ameambatana na Waziri wa mambo ya nne na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Stergomena Tax.
---
Rais Samia awakutanisha marais 11 kujadili umeme
Ni katika mkutano wa COP 27 unaoendelea nchini Misri kuanzia Oktoba 31 mpaka Novemba 18.
Dar es Salaam. Kutokana na upungufu wa megawati zaidi ya 6,000 unaozikabili nchi za kusini mwa Afrika, Rais Samia Suluhu Hassan kesho ataongoza mjadala ya kuongeza uzalishaji wa umeme na usambazaji wake katika mkutano wa 27 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Tabianchi (COP 27) kutafuta suluhu ya kudumu.
Rais Samia amewaalika wakuu wenzake wa nchi 11, rais wa Benki ya Dunia na rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ili kufanikisha uzalishaji na usambazaji wa nishati ya kutosha kwa ajili ya viwanda vinavyoendelea kujengwa barani humu.
“Mara zote Tanzania ilikuwa mshiriki tu, hii ni mara ya kwanza tunaandaa mkutano wa pembeni unaowakutanisha wadau muhimu. Kwa sasa, kwa ujumla tuna upungufu wa megawati 6,000 lakini miaka mitano ijayo utafika megawati 10,000. Tunahitaji nguvu ya pamoja kuwekaza,” amesema Januari Makamba, Waziri wa Nishati.
Waziri Makamba amesema Afrika huzalisha umeme kwa ushirikiano wa mataifa kadhaa (power pools) na Tanzania ni mjumbe wa ushirika wa mataifa ya kusini (Southern Africa Power Pool) ulioanzishwa mwaka 1997 ukilenga kuimarisha uzalishaji na usambazaji ili Taifa litakalokuwa na ziada liliuzie lenye upungufu.
“Tangu SAPP ianzishwe hakujawahi kuwa na umeme wa kutosha hata miundombinu ya usambaji haikujengwa. Sasa hivi Tanzania tunakamilisha njia ya usambazaji kwenda Zambia na ile ya Kenya itakayokamilika Desemba. Kwa ukubwa wa soko letu, itakuwa rahisi kupata mkopo nafuu.
Rais (Samia) amewaita wadau ili kujadiliana vyanzo mbadala hasa umemejua na upepo vinavyoweza kuchangamkia na kampuni kubwa za nishati,” amesema Makamba.
Kwa sasa, waziri alisema Tanzania inavyo vyanzo vinavyoweza kuzalisha zaidi ya megawatu 2,000 za umemejua na upepo na tayari Serikali inatekeleza miradi ya kuzalisha megawati 300 akitolea mfano uliopo Kishapu mkoani Shinyanga na Singida.
Takwimu zilizopo zinaonyesha nchi wanachama wa SAPP zina vyanzo vya kuzalisha zaidi ya jigawati 10.3 vinavyoweza kuendelezwa ndani ya miaka 10 ijayo na kukidhi mahitaji iwapo zitajenga giridi ya kilomita 6,085 kuusambaza kwa wananchi wao.
“Tunahitaji uwekezaji wa dola 18 bilioni za Marekani kukidhi mahitaji yatakayoongezeka kwa miaka mitano ijayo katika mataifa yote 12 ya SAPP,” amesema Makamba.
Ajali ilivyokuwa inatokea yeye hakuwa Nchini, masuala mengine ni kuyapa muda tu kwa Sababu asingeweza kuvunjilia mbali ratiba ambayo tiyar alikuwa nayo toka Jamhuri ya China hadi Misri, tkumbuke pia waziri Mkuu alikuwa mstari wa mbele kuiwakilisha serikali katika ajali ile.Sijui viongozi wenzake walikuwa wanamwonaje hapo mkutanoni! Yaani watu wake wamefariki na dunia nzima inajua, yeye eti yuko mkutanoni!
SHAME!
Duh!Ajali ilivyokuwa inatokea yeye hakuwa Nchini, masuala mengine ni kuyapa muda tu kwa Sababu asingeweza kuvunjilia mbali ratiba ambayo tiyar alikuwa nayo toka Jamhuri ya China hadi Misri, tkumbuke pia waziri Mkuu alikuwa mstari wa mbele kuiwakilisha serikali katika ajali ile.