Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki uzinduzi wa album ya Harmonize leo tarehe 25 Mei, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City.
View: https://www.youtube.com/live/PafgRqkHmNo?si=oHJtx2WgTWFmEp9k
Rais Samia ameoneshwa kufurahishwa na ukuaji wa Harmonize kwani alivyo sasa ni tofauti na alivyokuwa miaka 8 nyuma.
Amesema mapito ya kimahusiano aliyopitia Harmonize huwapata vijana wengi, na ametaja baadhi kama Ray Vanny, Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz.
Amewapongeza wanawake wote waliolea na kukuza watoto hadi kuwafikisha kwenye mafanikio, wanawake na jeshi makini na jeshi imara.
Amesema amekuwa na kawaida ya kubeba wafanyabiashara kwenye ziara zake, sasa ataanza kwenda na wasanii ili kufungua zaidi nchi na kukuza tasnia hiyo.
Amewasaa wasanii wa muziki na filamu kuwekeza kwenye maisha yao kwani hawatafanya kazi hizo milele. Uwekezaji huo utawasaidia pindi watakapokuwa hawawezi tena kufanya kazi wanazofanya sasa.
View: https://www.youtube.com/live/PafgRqkHmNo?si=oHJtx2WgTWFmEp9k
ALICHOZUNGUMZA RAIS SAMIA
Amemshukuru Msanii Harmonize kwa kumualika kwenye hafla hii aliyoiita 'Usiku wa kuutukuza muziki wa Mama'Rais Samia ameoneshwa kufurahishwa na ukuaji wa Harmonize kwani alivyo sasa ni tofauti na alivyokuwa miaka 8 nyuma.