Rais Samia ashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa miradi mahsusi ya umeme. Vijiji vyote Bara kufikiwa umeme mwishoni mwa 2023

Rais Samia ashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa miradi mahsusi ya umeme. Vijiji vyote Bara kufikiwa umeme mwishoni mwa 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishudia Utiaji Saini wa Mikataba ya Utekelezaji wa Miradi Mahsusi ya Umeme leo tarehe 14 Februari, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam



Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini REA, Hassan Said anazungumza

Mikataba 14 ya Wakala wa Nishati Vijijini inatarajiwa kusainiwa leo Februari 14, 2023.

Miradi ya Ujazilili wenye thamani ya Tsh Bilioni 2 kwa ajili ya mikoa 7, utaunganisha umeme kwa wananchi 88,200 utasainikwa kwa wakandarasi wanne.

Mradi wa pili Migodi na Kilimo kwa ajili ya mikoa 25 katika maeneo 336, thamani yake ni Tsh. Bilioni 115, lengo ni kupunguza gharama za wachimbaji hasa wadogowadogo

Mradi wa 3, Mradi wa kupeleka umeme kwenye vituo vya afya, pambu za maji, maeneo 399 katika mikoa 25, thamani yake ni Tsh. Bilioni 35.6, ambapo kuna ushirikiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya, Utakuwa na parcage mbili.
Hassan Said: Vijiji vyote Tanzania Bara vitapata umeme kufikia Desemba 2023.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini REA, Hassan Said amesema mradi mkubwa unaoendelea wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili utapeleka huduma ya umeme katika vijijini 4,071.

Amesema “Mungu akitujalia vijiji vyote vya Tanzania Bara vitakuwa vimefikiwa na Huduma ya Umeme mwishoni mwa mwaka huu (2023), mradi huo unagharimu Tsh. Trilioni 1.2, hizo ni fedha za Serikali, kuna mchango wa Benki ya Dunia na Umoja wa Jumuia za Ulaya.”

Waziri Makamba azungumza. Asema umeme hautoshi
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema hayo wakati wa Utiaji Saini wa Mikataba ya Utekelezaji wa Miradi ya Umeme, Dar es Salaam.

Amesema “Tulipo kwenye umeme leo ndipo tulipokuwa kwenye barabara Mwaka 1990, umeme hautoshi, miundombinu haitoshi lakini tunafarijika sana na Rais Samia, kama aliyovyofanya Mzee mkapa Mwaka 1995 ndicho unachokifanya leo kwenye umeme ili shida ya umeme iishe.”

Ameongeza kuwa mahitaji ya Umeme kwa Watanzania ni mengi, kila Kijiji kitafikiwa itakapofika Desemba 2023 lakini kusambazwa ni jambo lingine kwa kuwa wanaweza kufika vijiji vyote lakini wasifike vitongoji vyote

Rais Samia anazungumza
Mniruhusu nami niingize sauti yangu katika kumshukuru Mungu kutukutanisha hapa katika tukio hili kubwa la kihistoria. Lakini pia nitumie fursa hii kumshukuru Waziri January Makamba Waziri wa Nisshati na timu yake. Mashirika mawili TANESCO na REA kwa kukamilisha mipango hii iliyosainiwa leo hapa na kwamba imewapendeza kunishirikisha mimi kutia saini kwenye mikataba hiyo.

Natumia fursa kuipongeza Wizara ya Nishati, Wakala wa nishati REA na TANESCO kuandaa miradi hii, ni miradi mizuri sana kama nilivyosema ni miradi muhimu sana kwa thamani na ukubwa itakayokuwa na manufaa kwa nchi na watu wake.

Kama anavyosema Wazii mwaka jana wakati tunatengeneza bajeti, Waziri alisema nimeingia ofisini lakini kua kilio kikubwa sana cha umeme. Akaja na bajeti yake akataka trilioni 11. Nikamtazama usoni nikamuuliza Waziri upo serious? Trilioni 11 nazipata wapi? Unajua kuna miradi mikubwa tunaifanya na pesa zinahitajika, nikamwambia arudi ajipange vizuri arudi na phases ya kutekeleza miradi unayoipendekeza.

Akaenda karudi akaniambia phase ya kwanza nahitaji trilioni 4, nikamuuliza kwa miaka mingapi akasema miaka minne. Nikamwambia hiyo naweza kubeba. Ntakupangia bilioni 500 kila mwaka ndani ya miaka minne tutakuwa tumetimiza. Kwa kuanzia tutatenga mradi wa bilioni 400 kwa mradi wa gridi imara, bilioni 400 za serikali lakini bilioni 400 tulipata kwa wenzetu wa IMF.

Leo hii tumesaini mikataba ya shilingi trilioni 1.9 kwa ujumla ambayo ni jumla ya mikataba 26 itakayokwenda kwa miaka hiyo niliyosema. Leo pia tumesini mikataba ya kupeleka umemee katika migodi midogo midogo, maeneo y kilimo, vituo vya afya na vyanzo vya maji, huku niko kujali wanyonge.

Tukipeleka umeme kwenye migodi midogo, kama mlivyoona hata mitambo na mashine zinazotumika zitabadilika kwa ajili ya vishimo vile wanavyotumbukia na grili mojamoja. Watakuwa na mitambo mizuri. Watachimba wakisalama.

Tunapeleka umeme kwenye vyanzo vya maji, miradi hii ina maana sana kwa watu wetu wa mikoni na kwenye wilaya mbalimbali na huko vijijini.

Miradi hii tuliyoisaini leo itapeleka umeme katika maeneo 336 ya uzalishaji mali nchini. Mategemeo yetu ni kwamba yataenda kutusaidia kujenga uchumi katika ngazi za chini au mico-economy tunakwenda kupeleka kunyanyua. Lakini wamesema vitongoji 1522 vinakwenda kupata umeme na vituo vya afya 63 na maeneo yenye vyanzo vya maji. Kwahiyo hii ni kazi kubwa kidogo inakwenda kufanyika.

Nchi yetu ni kubwa, tutamaliza mradi huu bado malalamiko yatakuwepo, lakini kama tulivyosema hii ni phase ya kwanza, tutakwenda phase ya pili mpaka tumalize.

"Kila nikiangalia mapesa yanayohitajika pale nasema Mungu wangu, Mungu saidia Samia ntapata wapi pesa hizi! Lakini kwenye nia kuna njia, leo SGR nna pesa mpaka lot ya 6 kufika Kigoma, sikutegemea"

Kwa ujumla miradi hii inakwenda pamoja kwani bila kuimarisha gridi ya taifa juhudi kubwa zinazofanyika kupeleka umeme vijijini hazitaweza kuzaa matunda.
 
Mradi wa kwanza ni Kuunganisha Ilala na Kurasini underground
Bilioni 13 kutumika
 
Haya mambo ya kutiliana saini kwenye camera za tv na radio zamani hayakuwepo kwani shughuli ya kawaida ya kiofisi. Ujio wa machawa ndio umeleta haya. Miradi yote ya nishati katika nchi zisizo za kidemokrasia huwa ni upigaji mtupu
 
Tabora Katavi

KVA 132

Vituo vya kupoza umeme
Transformer kubwa kufungwa
MVA 10,20,35
 
Viwanda Zegereni
KVA 220

Substation ya MVA 120
Bilioni 51 kutumika
 
Msigani Ubungo

Transformer 4 kuwekwa

Bilioni 2 kutumika
 
Miradi yote ikikamilika gharama za Umeme zitashuka Tanzania
 
Back
Top Bottom