Rais Samia: Askari mnalalamikiwa kushikilia leseni za madereva muda mrefu

Rais Samia: Askari mnalalamikiwa kushikilia leseni za madereva muda mrefu

Hivi Police huwa wanabadilika pamoja na haya maagizo? Ni kati ya Wafanyakazi wa Serikali ambao kwao Mulungula kwanza kuwajibika baadaye. Wewe jaribu uibiwe vitu Nyumbani kwako halafu ripoti Police, utadhani wewe ndio Mwizi mwenyewe kwa usumbufu.
 
Hivi Police huwa wanabadilika pamoja na haya maagizo? Ni kati ya Wafanyakazi wa Serikali ambao kwao Mulungula kwanza kuwajibika baadaye. Wewe jaribu uibiwe vitu Nyumbani kwako halafu ripoti Police, utadhani wewe ndio Mwizi mwenyewe kwa usumbufu.
hahhahahahahah sema hii kitu ni changamoto
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado Askari wanalalamikiwa kwa masuala kadhaa ikiwemo kushikilia Leseni za Madereva kwa muda mrefu au kuwalazimisha kulipa faini papo hapo ilihali Sheria inampa muda Dereva wa kuilipa.

Amesema, "Kingine ni kuna ukamataji mwingi wa Vyombo. Ukipita Vituo vya Polisi utakuta Pikipiki nyingi zimepangwa, na nyingine hazionekani kama zimekamatwa jana na leo"

Ameongeza, "Makosa yasikilizwe, kesi imalizike ahukumiwe kosa. Vyombo vinabaki muda mrefu unahisi vimetelekezwa. Iangaliwe kwa undani kero hizi zinasababishwa na nini"
Siku hizi askari anakushikia vipi leseni wakati hata nikumachia nina namba ambazo ndio muhimu na IDs zingine plus copy.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Suluhisho
  1. Kuwekwe vituo maalumu vya ukaguzi wa vyombo vya moto kwenye kila barabara
  2. Vituo hivyo vifungwe cctv cameras for transparency reasons
  3. Askari wasiruhusiwe kuwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye mifuko yao katika vituo hivyo vya ukaguzi
  4. Kuwepo dawati la malalamiko dhidi ya askari kwenye kila mji na wapokeaji wa malalamiko wasiwe askari ...labda PCCB
  5. Kwenye hilo dawati la malalamiko kuwepo mashine za kurekodi malalamiko husika
VInginevyo Rais utachakaa kero ni nyingi na huwezi kuzifuatilia zote, omba mashine zikusaidie ili haki unayoihubiri ipatikane bila uonevu
Yaani umeorodhesha mambo yote ya Muhimu, suala LA polisi kusimamisha magari hovyo hovyo huchochea sana rushwa na ajali!! Fikiria polisi anakupakazia makosa zaidi ya Mara tatu katika safari moja, utakuwa na amani ya safari!? Lazima uchanganyikiwe na ni chanzo kikubwa cha ajali
 
Labda malezi yamewafikisha hapo hivi Hawa jamaa wanalipwaje? Naona kama hawana security of tenure.

Tukianza kuwafundisha wazingatie haki basi hata ikifikia KUSIMAMIA uchaguzi watatenda haki.

Vetting ya kuwapata Viongozi na Askari wapya ikifanyika vizuri hali itakuwa tofauti.

Tukiacha upande mmoja wavuruge haki hata upande wa pili watavuruga.
 
Ilifikia kipindi JWTZ walipewa Kila sector nashauri hata barabarani wapewe mafunzo halafu wawekwe na wao tuangalie malalamiko yataendelea au raia watafurahia kuwepo wao?
 
Ilifikia kipindi JWTZ walipewa Kila sector nashauri hata barabarani wapewe mafunzo halafu wawekwe na wao tuangalie malalamiko yataendelea au raia watafurahia kuwepo wao?

unawaza kama mtoto anayefikiri baba yake anapiga watu wote.

ishu hapa ni rushwa,sio nani katoka wapi.
 
Hao upewa hesabu kwa siku kama daladala isipotimia upelekwa FFU akalinde bank hivyo lazima waende speed.
Hakuna mswahili ajitumae bure kwenye Kazi
 
Ilifikia kipindi JWTZ walipewa Kila sector nashauri hata barabarani wapewe mafunzo halafu wawekwe na wao tuangalie malalamiko yataendelea au raia watafurahia kuwepo wao?
Labda kama Wana matumbo ya chuma, Hakuna uzalendo kwenye njaa
 
Corruption haiwezi kuisha,ikitungwa kanuni kwa nia ya njema kuimarisha usalama barabarani kwa vyombo vya moto inageuka advantage kwa mla rushwa.
Hata fine za makosa ya traffic kila zikiongezwa inageuka advantage kwa mla rushwa.
 
Kuna mmoja alikamata leseni ya dereva wangu akamwambia niifuate nyumbani kwake Kurasini. Niliishia kununua resheni ya nyumbani kwake ya wiki nzima[emoji24]
Kaka una gari kweeli kama kuandika leseni tu inakuwia vigumu[emoji24][emoji24][emoji24]
Pic%20Layer_2021111311215721.jpg
 
Kwa sasa kufanya biashara ya usafirishaji TZ ni shida sana hasa kwa gari hiace, wanaomba leseni wakidai wanakagua ukimpa tuu kinachofata ni faini bila sababu za msingi, nchi yetu kama tutafika tuendako
Dawa ni kutompa kujifanya umeisahau tu unamtia sound! Maana ukimpa tu anarekodi zile namba za leseni kisha anakuuliza aidha una “Luteni” au akuandikie faini?

Kisingizio huwa ni kuvuka zebra tu😅
 
Back
Top Bottom