Rais Samia ataka uwekezaji wa sayansi, Teknolojia

Rais Samia ataka uwekezaji wa sayansi, Teknolojia

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Afrika wakiwekeza zaidi katika sayansi na teknolojia kwa vijana, wanaweza kuwa sehemu muhimu ya kustawisha uchumi kama ilivyo China.

Ametoa kauli hiyo Dar es Salaam leo, wakati akifungua Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika, ambao unawakutanisha viongozi na wadau mbalimbali kutoka Afrika.

Amesema ni muhimu wanawake na vijana wakajengewa uwezo kupitia elimu, ikiwa ni pamoja na kutumia sayansi na teknolojia itakayowawezesha kumiliki na kutumia rasilimali za Afrika, kujenga na kukuza Afrika ya viwanda na biashara kwa uchumi imara.

“Tutakapokwenda kutekeleza hili, tutaangalia lengo namba mbili ambalo linaangazia biashara Afrika, ambalo linasisitiza kuhusu kuwa na raia walioelimika, wenye maarifa ambao wanaweza kwenda sambamba na kasi ya sayansi na teknolojia,”amesema.

Rais Samia amesema kuwa: “Ninataka kutilia mkazo suala la elimu kwa vijana kuhusu sayansi na tekolojia, na mfano mzuri ni kwa nchi ya China, ambayo uchumi wake kupitia sayansi na teknolojia unajengwa na vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35, unaweza kukuta maprofesa wengi wa miaka 35, ambao wamebobea katika masuala ya sayansi na teknolojia na ndiyo wanaongoza makampuni mengi yanayozalisha sana kwenye nchi yao.
 
Sisi wananchi kazi yetu kusimuliwa tu.

Ila zinapotokea fursa.

Wale wale ndio wanazipata.
Uko sahihi Mkuu. Lakini nikuulize swali; Kwa nini akili huwa zinawarejea mkiwekwa pembeni? Siku zote tunawaambia hapa hawa viongozi wenu hawana jema zaidi ya kuwatumia nyie kama matambala ya deki!
 
Aiseee kuna 3D mpya wachina wamekuja nayo kwenye movie theater hatariii sanaaa. Sisi watanzania kwanza tunataka kilimo ili tushibe na akili zetu zijuwe nani anafaa kuwepo madarakani. Akili haifanyi kazi na njaa sasa hii technology tutaishia kulala mbele ya computer na minyao kibao.
 
Wazo lauheshimiwa rais Samia kalinasa hapa , hakuna Namna zaidi ya kutumia Mbinu hii kukuza sayansi na technologia, soma uzi huu haraka na kwa Kasi umfikie rais .Ili aangalie Namna na kulitendea kazi wazo hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya China chini ya chama bora CPC wameweka sheria kali kwa viongozi washenzi , mafisadi na wachelewesha maendeleo . China inaua ,ina nyonga na Ina funga viongozi wapumbavu . China hawachekee wapumbavu.

Ni upambavu kwa sisi kuwaza kuwa Kama China wakati tupo chini ya serikali chakavu na chini ya chama chakavu .

Kiongozi unapoitaja na kuizungumzia China unazungumzia taifa namba 2 kiuchumi duniani na namba 1 Kisayansi na kiteknolojia duniani.

Tuwape heshima yao chama cha kikomunisti cha China , Chama Cha mapinduzi [ CCM ] hakiwezi kufanya Kama China na kamwe hakiwezi kutufikisha mahali China walipo katika sekta yoyote ile .

N.B: TUACHE KUOTA NDOTO ZA MCHANA TUTA JIKOJOLEA.
 
Aiseee kuna 3D mpya wachina wamekuja nayo kwenye movie theater hatariii sanaaa. Sisi watanzania kwanza tunataka kilimo ili tushibe na akili zetu zijuwe nani anafaa kuwepo madarakani. Akili haifanyi kazi na njaa sasa hii technology tutaishia kulala mbele ya computer na minyao kibao.
Sisi computer isha tushinda ma IT wetu akili zimelala
 
Serikali ya China chini ya chama bora CPC wameweka sheria kali kwa viongozi washenzi , mafisadi na wachelewesha maendeleo . China inaua ,ina nyonga na Ina funga viongozi wapumbavu . China hawachekee wapumbavu.

Ni upambavu kwa sisi kuwaza kuwa Kama China wakati tupo chini ya serikali chakavu na chini ya chama chakavu .

Kiongozi unapoitaja na kuizungumzia China unaouzungumzia taifa namba 2 kiuchumi duniani na namba 1 Kisayansi na kiteknolojia duniani.

Tuwape heshima yao chama cha kikomunisti cha China , Chama Cha mapinduzi [ CCM ] hakiwezi kufanya Kama China na kamwe hakiwezi kutufikisha mahali China walipo katika sekta yoyote ile .

N.B: TUACHE KUOTA NDOTO ZA MCHANA TUTA JIKOJOLEA.
Wacha wivu. Kwa hiyo Ulitaka aseme Amerika au Europe.

Usituweke vita yenu na Wachina iwe ni vita yetu.

Amani
 
Uko sahihi Mkuu. Lakini nikuulize swali; Kwa nini akili huwa zinawarejea mkiwekwa pembeni? Siku zote tunawaambia hapa hawa viongozi wenu hawana jema zaidi ya kuwatumia nyie kama matambala ya deki!
Hilo nalo waende wakaliangalie
 
Wacha wivu. Kwa hiyo Ulitaka aseme Amerika au Europe.

Usituweke vita yenu na Wachina iwe ni vita yetu.

Amani
Nasema tena hatuwezi kufika mahali walipo China kwa huu utani wa CCM . Kasome CPC iliwa fanya nini wachina .kasome hawa watu Mao Zedong, Deng Xiaoping na Xi Jinping kipi waliwafanya na walifanyia wachina mpaka wakawa hapo walipo alafu njoo watazame viongozi wetu walio kwenye chama chakavu cha CCM . Kuna utofauti mkubwa Kati ya CPC na CCM ni Kama mbingu na ardhi na CPC ndio siri ya mafanikio ya China.

Tusidanganyane Kama watoto wakati ni vitu visivyo wezekana Chini ya CCM.
 
Mama ruhusu machinga barabarani hali tete utaua familia. Ndoa zilishasambaratika pesa hakuna nguvu ya kiume Hakuna shibe ndo tatizo
 
Uko sahihi Mkuu. Lakini nikuulize swali; Kwa nini akili huwa zinawarejea mkiwekwa pembeni? Siku zote tunawaambia hapa hawa viongozi wenu hawana jema zaidi ya kuwatumia nyie kama matambala ya deki!
Sina kisirani chochote mkuu natoa mawazo yangu tu ambayo kwa muda huu yametokea kuwa ya aina hiyo.
 
damedamn.png
 
Back
Top Bottom