Rais Samia ataka uwekezaji wa sayansi, Teknolojia

Kwa hiyo unasema Tutawaliwe tena? Manake mbadala siuoni. Hatahivyo vita baridi kati ya Wachina na Wazungu isiwekwe kwenye nyoyo zetu. Tunayetu mengi tu kama Kuondoka katika Jumuiya ya Madola. Total Rubbish to be in it.
 
Sisi wananchi kazi yetu kusimuliwa tu.

Ila zinapotokea fursa.

Wale wale ndio wanazipata.
Kiongozi wako huyo, anakupa maono yake na namna atakavyosimamia maono yake hayo ili nchi anayotawala iyafikie hayo aliyoyaona yeye.
Au nimeongeza chumvi, mkuu wangu 'stroke'?

Nchi yetu hii Tanzania itapiga hatua kubwa sana chini ya uongozi wa namna hii wa kupashana tu taarifa na siku zinasonga mbele.

Miaka inapita mbio, sisi tunapeana mipasho tu!
 
Hilo nalo waende wakaliangalie
Shamaliza kazi mwana mama; saa hii anawaza atasema jambo gani jingine kwenye ufunguzi mwingine.

Uongozi wa aina hii hauleti mabadiliko chanya; nchi inabaki hapo hapo tu ilipofikia au inarudi nyuma. Hakuna kwenda mbele.
 
Maneno meengi hamna kitu ndugu yangu.

Ila tunawaona watoto wao namna wanavyokula keki ya Taifa.
 
Huo ndiyo mwelekeo sahihi. Auzime mwenge wa uhuru, ni ushirikina vijana wanakimbiza moto badala ya kukaa laboratory kufanya vumbuzi.
 
Actions speaks louder than words

Tozo Juu (which translates kwenye bundles kuwa juu na digital miamala kuwa juu) TCRA kutumika kama nyundo badala ya nyenzo...

Yaani hawa watu bora wangeacha vitu bila kuingilia huenda tungefika mbali sana... (Anyway wamezoea kuvuna wasichopanda)
 
Ndivyo ilivyo. Mambo mengi yanaishia kwenye maneno. Hawamaanishi wanachosema.
Si unajua tena ukiwa kiongozi, ukifika mahali unahubiri tu kama uko madhabahuni, na vile hawaulizwi chochote zaidi ya kupigiwa makofi, basi wanahubiri tu.
 
23 September 2024
New York City

Mahojiano na rais Cyril Ramaphosa kuhusu jinsi 4R zilivyoiinua imani ya wananchi na wafanyabishara ndani ya nchi na wale wawekezaji kutoka nje


JINSI CYRIL RAMAPHOSA ANAVYOTUMIA 4R ZA UKWELI, KAMA ZANA YA KUVUTIA MAENDELEO


View: https://m.youtube.com/watch?v=4gF-YkcFMFQ Kwa kujivunia kutoka moyoni bila kuwa na ulaghai wa kutumia 4R kuwezesha chama chake pekee kuwa na wabunge 100% bunge la taifa na bunge la majimbo, Mheshimiwa Cyril Ramaphosa wa South Africa anajivunia jinsi ANC ilivyovuna 40 % ya kura huku chama kinachofuatia DA 21 % huku asilimia zilizobaki 39% zimegawana vyama vingine vidogo.

Kupitia 4R za ukweli nchi inaendelea kuwa na mihimili huru ya Bunge, Mahakama na vyombo vya habari.

Hali hiyo imewapa imani wawekezaji wa ndani wana imani kuwekeza zaidi ndani na pia hali hiyo inavutia wawekezaji zaidi kutoka nje.

Kutokana na kuwa na kuaminiana ndani, South Africa imekuwa mfano kwa mataifa dada jirani zilizo nchi za SADC na mbali zaidi.

4R za ukweli zisizo na hila ovu zimemuondolea rais wa South Africa kutokukosa usingizi na kuwaza kutumia majeshi ya usalama kama polisi na usalama wa taifa kuwatishia raia.

kutokana na mazingira mazuri yaliyoletwa na 4R kupitia serikali ya Umoja wa Kitaifa GNU, sana nchi ina nafasi ya kutumia viongozi wa vyama vingine vya kisiasa katika kulitumikia taifa ktk nafasi za kiuongozi na hivyo nchi kufaidika na kila raia aliye na upana wa maono bila kujali wametoka vyama vingine.

Tofauti na kama ingekuwa utawala wa kimabavu, kuzuia raia kufikia nafasi za kiuamuzi kupitia kura walizopata baada ya kuaminiwa na wapiga kura waliowacgagua katika uchaguzi ulio wazi, huru na wa haki kuanzia ngazi ya mchakato wa mikutano ya vyama vyao, kampeni hadi kutangazwa wameahinda.

Source: SABC News
 
Tujiulize je 4R za Tanzania zimeleta nini zaidi ya hadaa, ulaghai, matumizi mabaya ya mfumo wa haki jinai, kuteka, kupoteza na mauaji ya kisiasa.

4R za Tanzania badala ya kuwapa imani raia na wafanyabiashara, 4R imekuwa ni kiini macho chenye kutumia kuleta hofu, kuzuia chaguzi huru, kuzuia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwa kadri ambavyo wangeweza, nchi kupewa jina la nchi ya utawala wa kimabavu na mbaya zaidi kududimiza maendeleo na kuwanyima furaha raia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…