Rais Samia atangaza siku 5 za maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth aliyekuwa Mkuu wa Nchi ya Tanganyika

Tatizo huelewi kiitifaki, Malkia alikuwa nani kwa Tanganyika. Malkia, kabla ya uhuru alikuwa mkuu wa koloni la Tanzania kufuatia Azimio la Umoja wa Mataifa, ambapo Tanganyika iliwekwa chini ya usimamizi wa Uingereza mpaka itakapokuwa tayari kujitawala.

Tanganyika, baada ya mkoloni Mjerumani kuondolewa, mwingireza aliwekwa kama mlezi wa Tanganyika.

Hata baada ya uhuru, Tanganyika/Tanzania imekuwa nchi mwanachama wa Jumuia ya madola. Na mkuu wa jumuia ya madola ni Malkia/Mfalme wa Uingereza.

Kudai kuwa mbona uingereza haikutoa siku za maombolezo kufuatia kifo cha Magufuli, ni sawa leo hii Rais au Waziri mkuu afariki, zitolewe siku za maombolezo, halafu wewe useme kuwa mbona hawakutoa siku za maombolezo kufuatia msiba wa baba yako au mama yako.

Binadamu wote ni sawa lakini tunatofautiana. Samia ni mkuu wa nchi, Biden ni mkuu wa nchi, malkia ni mkuu wa nchi lakini kuna tofauti kubwa. Ukubwa wa mamlaka hupimwa katika idadi ya unaowaongoza/unawahudumia. Malkia alikuwa mkuu wa mataifa mangapi, linganisha na Magufuli alikuwa mkuu wa mataifa mangapi. Kufuatia kifo cha Magufuli, Uingereza ilitoa salamu za rambirambi, kwa nafasi ya Magufuli kama mkuu wa nchi ya Tanzania pekee, ilitosha.
 
Tanzania ilikuja mwaka 1964, Wakati huo Malkia hakuwa mtawala tena wa Tanganyika au Zanzibar.

Kama unaleta hoja kuwa Malkia alikuwa mkuu wa nchi ya Tanganyika, alipigiwa kura na mtanganyika gani mpaka akawa mkuu wa nchi yao?. Naona unatetea legacy ya ukoloni!
 
MNATAKIWA MJUE KUANZIA SASA NA KUENDELEA ,KIONGOZ YOYOTE MKUBWA HUANZIA ROHONI YANI UPANDE WA PILI, JUMUHIYA YA MADOLA SIO MNAVYO IJUA NINYI condoo wa mungu
 
Kabla ya uhuru Afrika iligawanyika katika tawala za kikabila, ndiyo maana ilikuwa rahisi kwa wakoloni kuzichukua tawala hizi, kuzigawanya walivyoona inafaa, na kuzifanya kuwa makoloni.

Tanganyika, Uganda, Kenya ilikuwa ni koloni koloni moja la Wajerumani, likijulikana German: Deutsch-Ostafrika) (GEA), na mjerumani alikuwa mtawala wake kwa utaratibu ambao hao wakoloni walikubaliana. Ni mifumo na migawanyo hiyo ya wakoloni, mpaka leo tunaendelea nayo. Wao ndio walituwekea mipaka ambayo mpaka leo tunaendelea kuheshimu kuwa ni mipaka ya nchi zetu, kama vile ilikuwepo kabla ya ukoloni, kumbe haikuwepo.

Ni baada ya Mjerumani kupoteza ushindi kwenye vita ya Dunia ndipo Tanganyika ikawekwa kwenye uangalizi wa Uingereza mpaka itakapokuwa tayari kujitawala. Wakati huo wote, kiongozi mkuu wa Uongereza ndiye alikuwa kiongozi pia mkuu wa Tanganyika na makoloni mengine yote yaliyokuwa chini ya Uingereza. Kwa wakati huo, hao wakoloni walikuwa ndiyo mamlaka halali za kiutawala mpaka pale mataifa mengi yaliyokuwa makoloni yalipogomea mfumo huo. Machifu ambao kabla ya ukoloni, walikuwa ndio viongozi wakuu wa tawala zao, wakafanywa kuwa viongozi wa chini katika mfumo wa nchi ulioacnzishwa na wakoloni.

Siyo kila utawala huwekwa kwa njia ya kura. Hivi hata kabla ya kuja kwa wakoloni, ni nchi gani ya Afrika ilikuwa inawapata viongozi wak kwa njia ya kura? Kwa sababu hakukuwa na upigaji kura, tuseme Afrika nzima haikuwahi kuwa na watawala?
 
Zilipotea Mkuu mambo ya UTAWALA BORA

Two years back...niliiipata ila kwa mbinde sana Mkuu kupitia hukohuko kwao SKOTISHI tena kwa heshima ya Julius upande wa Conservation
Duuu. Kweli hapa kazi tuu
 
Mapaka ya mbali yaliyokuwa yanafadhili utumwa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na huku Tanzania na kututesa sana kupitia ukoloni yafe halafu tuomboleze?!Haya ni mambo ya aibu na ya ajabu kabisa kutoka Serikali dhaifu na mfu ya CCMπŸ’πŸ’πŸ’
 
Kuna mahala Mwafrica anapaswa kuonyesha hasira zake dhidi ya ukoloni ule na huu uliopo sasa ambao umeendelea zaidi kwa kutumia ndugu zetu kama vibaraka na mkoloni kupandikiza mifumo inayoendelea kutokoloni.
 
Nakuuliza tuliwatuma wafanye hivyo vitu?? Nani kawaleta huku kama sio ujangili wao?

Hakuna njia yoyote ya kumtetea mkoloni atabaki kuwa shetani tu daima.
Ni shetani kwako ambaye hupendi lakini kwa wengine ni binadamu tu kama binadamu wengine na ni chanzo cha maendeleo Afrika na duniani kote.
 
Malawi na Rwanda ni siku 10 πŸ˜†πŸ˜†

Cheki hii πŸ‘‡
 

Attachments

  • Screenshot_20220911-205531.png
    39.8 KB · Views: 3
Malawi na Rwanda ni siku 10 [emoji38][emoji38]

Cheki hii [emoji116]
Ukiwa mjinga unaweza kuamini kuwa una uwezo wa kujitenga na mzungu, na ukaishi.

Leo hii hao wazungu ndio wanaofanya tuwe na mawasiliano ya haraka kuanzia kusafiri mpaka simu, television, mitambo mbalimbali, n.k.

Mchina pamoja na kupifa hatua katika kuiga teknolojia mbalimbali za wazungu, bado ameshikamana na wazungu kiasi cha kuwa mvutiaji no.1 wa wawekezaji toka Ulaya na America. Mjinga asiteweza kutengeneza hata baiskeli, anaamini anaweza kuishi kwa kujitenga na mataifa ya wazungu.

Wametutangulia, tufanye kazi kwa bidii, tushirikiane nao, huenda siku moja tutawakaribia, au pengine vizazi vyetu vya huko mbeleni vitawafikia. Lakini kwa fikra duni za baadhi ya watu kuwachukia wazungu, ndiyo tutazidi kuwa duni zaidi.

Ni nini ulicho nacho mtu mweusi ambacho kina thamani bila ya hao wazungu?

Tuna mbuga za wanyama, lakini watalii tunaowategemea kwa idadi kubwa ni hao wazungu.

Tuna dhahabu, almasi, tanzanite, wanunuzi wakubwa tunaowategemea ni hao wazungu.

Hata huko Uarabuni, kwenye mafuta mengi, makampuni ya uchimbaji, na soko kubwa la hayo mafuta, ni wazungu.

Hata chanjo za watoto wetu na akina mama wajawazito, bado tunamtegemea mzungu atulipie.

Wazungu wana mabaya yao, lakini matatizo mengi yanayompata mtu mweusi, mhusika mkubwa ni mtu mweusi mwenyewe.
 
mimi kabisa nimsifie huyo alibino alietesa babu zangu ngoja likapugwe mirungu huko
πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…