Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Tatizo huelewi kiitifaki, Malkia alikuwa nani kwa Tanganyika. Malkia, kabla ya uhuru alikuwa mkuu wa koloni la Tanzania kufuatia Azimio la Umoja wa Mataifa, ambapo Tanganyika iliwekwa chini ya usimamizi wa Uingereza mpaka itakapokuwa tayari kujitawala.Sasa hii ni shobo!
Sisi Rais wetu Magufuli alipofariki Waingereza walitangaza siku ngapi za maombolezo?.
Sisi tumeshafiwa na viongozi wetu wakubwa tu akiwemo Mzee Kawawa , hatujawahi kutangaza siku tano za maombolezo , Huyu Malkia kwetu ni nani haswa hadi tumpe siku zote hizo?
Huu ni utumwa wa Fikra!
Halafu hii serikali mbona inatoa taarifa kwa Umma usiku wa manane, imekuwa serikali ya kichawi?
Tanganyika, baada ya mkoloni Mjerumani kuondolewa, mwingireza aliwekwa kama mlezi wa Tanganyika.
Hata baada ya uhuru, Tanganyika/Tanzania imekuwa nchi mwanachama wa Jumuia ya madola. Na mkuu wa jumuia ya madola ni Malkia/Mfalme wa Uingereza.
Kudai kuwa mbona uingereza haikutoa siku za maombolezo kufuatia kifo cha Magufuli, ni sawa leo hii Rais au Waziri mkuu afariki, zitolewe siku za maombolezo, halafu wewe useme kuwa mbona hawakutoa siku za maombolezo kufuatia msiba wa baba yako au mama yako.
Binadamu wote ni sawa lakini tunatofautiana. Samia ni mkuu wa nchi, Biden ni mkuu wa nchi, malkia ni mkuu wa nchi lakini kuna tofauti kubwa. Ukubwa wa mamlaka hupimwa katika idadi ya unaowaongoza/unawahudumia. Malkia alikuwa mkuu wa mataifa mangapi, linganisha na Magufuli alikuwa mkuu wa mataifa mangapi. Kufuatia kifo cha Magufuli, Uingereza ilitoa salamu za rambirambi, kwa nafasi ya Magufuli kama mkuu wa nchi ya Tanzania pekee, ilitosha.