Rais Samia atangazwa tena mshindi wa tuzo mbili za kimataifa

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan ametangazwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Watetezi na Amani kuwa mshindi wa tuzo mbili za kimataifa ikiwemo ya amani duniani 2022.

Tuzo nyingine aliyotangazwa kuwa mshindi ni Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kuipata ni tuzo ya Rais wa Dhahabu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Gaudencia Kabaka amesema Rais Samia alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hizo wiki iliyopita na atakabidhiwa tuzo hiyo Oktoba 24, mwaka huu.

Akizungumza leo Jumamosi Oktoba Mosi, Kabaka amesema miongoni mwa mambo yaliyomfanya Rais Samia kupata tuzo hizo ni uboreshaji wa miundombinu ya afya na elimu ndani ya kipindi kifupi cha uongozi, utetezi wa masuala ya amani ikiwemo uhuru wa kuabudu na amani.

Mengine ni kujali masuala ya kijinsia kwa kuteua wanawake wengi katika uongozi, ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari na msingi na utoaji wa elimu bila malipo.

“Sisi UWT na wanawake wote wa Tanzania tumeona fahari sana kwa kuwa na Rais mwanamke ambaye ni Mheshimiwa Samia. Rais wa kwanza Afrika mwanamke kushinda tuzo mbili na kuandika historia ya kipekee nchini,” amesema.

Maraisi waliowahi kupata tuzo hizo kwa Afrika ambazo Rais Samia atakabidhiwa Oktoba 24, mwaka huu kwa Afrika ni Rais wa Liberia, George Weah na Rais wa Botswana Ian Tseretse Khama.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Samia kupokea tuzo akiwa madarakani baada ya Mei 22, 2022 alipokea tuzo ya Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) ikiwa ni kutambua jitihada anazozifanya katika ujenzi wa miundombinu nchini.
 
Najua wafuasi wa Magufuli na wale wa Upinzani ambao wamesahau tulipotoka watabeza na kukejeli tuzo hizi

Ila kwa sisi tunaokumbuka hii nchi ilivyokuwa kabla ya tarehe 17/3/2021 hakika tutaendelea kusheherekea mafanikio ya Rais Samia na kumtakia mema zaidi
 
Hii habari ni pigo kubwa kwa chawa na viroboto vya mlamba asali.

Sasa hivi wanakuja kutapika maana ugali wa usiku haupiti kooni.
 
Sema nini!!Maendeleo hayana chama, tupige kazi kwa pamoja.
 
Huo Ni mwanzo tu au mvua za rasha rasha tu maana atabeba kila tuzo mnayoifahamu nyie, Rais Samia ni kiongozi kwelii kwelii,Ndio maana nilipendekeza humu kuwa Apewe Udaktari wa Heshima katika uongozi na mahusiano ya kimataifa, Rais Samia Ni chuo Cha uongozi na mfano wa kuigwa katika Bara la Afrika na Dunia yote kwa ujumla, Huko mbele ya Safari Atatumika Kama Rejea ya kiongozi Bora kuwahi kutokea katika Bara la Afrika, kiukweli anatuheshimisha Sana watanzania kwa Sasa
 
Najua wafuasi wa Magufuli na wale wa Upinzani ambao wamesahau tulipotoka watabeza na kukejeli tuzo hizi

Ila kwa sisi tunaokumbuka hii nchi ilivyokuwa kabla ya tarehe 17/3/2021 hakika tutaendelea kusheherekea mafanikio ya Rais Samia na kumtakia mema zaidi

Kwahiyo unamsifia Samia kwa sababu ya ubora, au kwakuwa unampimia kwa ulevi wa madaraka wa Magufuli? Sio kwakuwa magufuli alikuwa kiongozi fedhuli, basi automatically mama Samia ni bora.
 
Huo Ni mwanzo tu au mvua za rasha rasha tu maana atabeba kila tuzo mnayoifahamu nyie, Rais Samia ni kiongozi kwelii kwelii,Ndio maana nilipendekeza humu kuwa Apewe Udaktari wa Heshima katika uongozi na mahusiano ya kimataifa, Rais Samia Ni chuo Cha uongozi na mfano wa kuigwa katika Bara la Afrika na Dunia yote kwa ujumla, Huko mbele ya Safari Atatumika Kama Rejea ya kiongozi Bora kuwahi kutokea katika Bara la Afrika, kiukweli anatuheshimisha Sana watanzania kwa Sasa

Mimi na mke wangu na familia yangu yote usituweke kwenye hao watanzania wanaoheshimishwa na mama Samia.
 
Kwani wewe Ni msomalia Tindo, mh Rais wetu kwa kazi kubwa aliyoifanya katika nchi hii na namna alivyo imarisha diplomasia yetu hakika kwa Sasa Tanzania imekuwa chaguo la kila mtu kujaribu kukanyaga Aridhi ya Tanzania, ndio sababu ya kuona mafuriko ya watalii wakimiminika hapa nchini
 
Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan ametangazwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Watetezi na Amani kuwa mshindi wa tuzo mbili za kimataifa ikiwemo ya amani duniani 2022.

Tuzo nyingine aliyotangazwa kuwa mshindi ni Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kuipata ni tuzo ya Rais wa Dhahabu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Gaudencia Kabaka amesema Rais Samia alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hizo wiki iliyopita na atakabidhiwa tuzo hiyo Oktoba 24, mwaka huu.

Akizungumza leo Jumamosi Oktoba Mosi, Kabaka amesema miongoni mwa mambo yaliyomfanya Rais Samia kupata tuzo hizo ni uboreshaji wa miundombinu ya afya na elimu ndani ya kipindi kifupi cha uongozi, utetezi wa masuala ya amani ikiwemo uhuru wa kuabudu na amani.

Mengine ni kujali masuala ya kijinsia kwa kuteua wanawake wengi katika uongozi, ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari na msingi na utoaji wa elimu bila malipo.

“Sisi UWT na wanawake wote wa Tanzania tumeona fahari sana kwa kuwa na Rais mwanamke ambaye ni Mheshimiwa Samia. Rais wa kwanza Afrika mwanamke kushinda tuzo mbili na kuandika historia ya kipekee nchini,” amesema.

Maraisi waliowahi kupata tuzo hizo kwa Afrika ambazo Rais Samia atakabidhiwa Oktoba 24, mwaka huu kwa Afrika ni Rais wa Liberia, George Weah na Rais wa Botswana Ian Tseretse Khama.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Samia kupokea tuzo akiwa madarakani baada ya Mei 22, 2022 alipokea tuzo ya Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) ikiwa ni kutambua jitihada anazozifanya katika ujenzi wa miundombinu nchini.
Tuzo uchwara hizo.....!!
 
Kwani wewe Ni msomalia Tindo, mh Rais wetu kwa kazi kubwa aliyoifanya katika nchi hii na namna alivyo imarisha diplomasia yetu hakika kwa Sasa Tanzania imekuwa chaguo la kila mtu kujaribu kukanyaga Aridhi ya Tanzania, ndio sababu ya kuona mafuriko ya watalii wakimiminika hapa nchini

Hamna mtalii kaja nchi hii kwa ajili ya mama Samia, labda ukawahadae watu wasiojua lolote huko vijijini.
 
Lini uliona mafuriko ya watalii kuja hapa Tanzania Kama kipindi hiki baada ya Royal Tour iliyofanywa na mh Rais ya kuvitanngaza vivutio vyetu vya utalii
 
Najua wafuasi wa Magufuli na wale wa Upinzani ambao wamesahau tulipotoka watabeza na kukejeli tuzo hizi

Ila kwa sisi tunaokumbuka hii nchi ilivyokuwa kabla ya tarehe 17/3/2021 hakika tutaendelea kusheherekea mafanikio ya Rais Samia na kumtakia mema zaidi
Ilikuwa lazima umtaje magufuli, maana bila hivyo mimba yake aliyokuachia ingejisikia vibaya sana
 
Hakuna link yoyote ya kudhibitisha haya uliyoyaandika...
 
Lini uliona mafuriko ya watalii kuja hapa Tanzania Kama kipindi hiki baada ya Royal Tour iliyofanywa na mh Rais ya kuvitanngaza vivutio vyetu vya utalii

Lini uliona cancelation kubwa ya watalii kuja nchini zaidi ya muda ya kipindi cha Covid? Kwasasa wageni waliokuwa wamesitisha safari zao kutokana na Covid, ndio wameamua kuja,na sio hizo porojo zenu za roho tua.
 
AWAMU YA 6 KAZINI
OKTOBA 01, 2022

HONGERA: MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN ametangazwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Watetezi na Amani kuwa mshindi wa Tuzo mbili za Kimataifa.

Ikiwemo ya Amani Duniani 2022 na nyingine ni Rais wa kwanza mwanamke Barani Afrika kuipata ni Tuzo ya Rais wa Dhahabu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.

#AwamuYaSitaKazini
#TunajengaTaifaLetu
#VijanaGreenMarathon
#KaziIendelee
IMG-20221001-WA0351.jpg
 
Back
Top Bottom