Rais Samia atangazwa tena mshindi wa tuzo mbili za kimataifa

Rais Samia atangazwa tena mshindi wa tuzo mbili za kimataifa

Huo Ni mwanzo tu au mvua za rasha rasha tu maana atabeba kila tuzo mnayoifahamu nyie, Rais Samia ni kiongozi kwelii kwelii,Ndio maana nilipendekeza humu kuwa Apewe Udaktari wa Heshima katika uongozi na mahusiano ya kimataifa, Rais Samia Ni chuo Cha uongozi na mfano wa kuigwa katika Bara la Afrika na Dunia yote kwa ujumla, Huko mbele ya Safari Atatumika Kama Rejea ya kiongozi Bora kuwahi kutokea katika Bara la Afrika, kiukweli anatuheshimisha Sana watanzania kwa Sasa
Mkakati wa wachawi wenzake kumlinda ili asisombwe na mafuriko ya team Magufuli.

Hayo yanayitajwa yote yalishakuwepo. Hakuna kipya. Vituo vya afya, madarsa, elimu bure na miundombinu, vilikuwepo.

Alistahili tuzo ya kuuza nchi na kuanzisha tozo kali kwa wananchi.
 
Najua wafuasi wa Magufuli na wale wa Upinzani ambao wamesahau tulipotoka watabeza na kukejeli tuzo hizi

Ila kwa sisi tunaokumbuka hii nchi ilivyokuwa kabla ya tarehe 17/3/2021 hakika tutaendelea kusheherekea mafanikio ya Rais Samia na kumtakia mema zaidi
Lakini wafuasi wa Magufuli nao ni Ccm !!
 
Mimi na mke wangu na familia yangu yote usituweke kwenye hao watanzania wanaoheshimishwa na mama Samia.
Nkeo atakubaliana na msimamo wako huu pale mtakapokuwa ndani shuka Moja tu. Pakikucha ataungana na watanzania wengine kumpongeza mama Kwa ushindi huu. Mkuu Tindo wewe ni mkongwe humu. Ifike kipindi uwe unakubali tu ukweli ktk baadhi ya mambo yanayofanywa na Rais Samia ni makubwa na sio Kwa kulinganisha na mtangulizi wake Bali ni karama aliyopewa na Mungu
 
Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan ametangazwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Watetezi na Amani kuwa mshindi wa tuzo mbili za kimataifa ikiwemo ya amani duniani 2022.

Tuzo nyingine aliyotangazwa kuwa mshindi ni Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kuipata ni tuzo ya Rais wa Dhahabu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Gaudencia Kabaka amesema Rais Samia alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hizo wiki iliyopita na atakabidhiwa tuzo hiyo Oktoba 24, mwaka huu.

Akizungumza leo Jumamosi Oktoba Mosi, Kabaka amesema miongoni mwa mambo yaliyomfanya Rais Samia kupata tuzo hizo ni uboreshaji wa miundombinu ya afya na elimu ndani ya kipindi kifupi cha uongozi, utetezi wa masuala ya amani ikiwemo uhuru wa kuabudu na amani.

Mengine ni kujali masuala ya kijinsia kwa kuteua wanawake wengi katika uongozi, ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari na msingi na utoaji wa elimu bila malipo.

“Sisi UWT na wanawake wote wa Tanzania tumeona fahari sana kwa kuwa na Rais mwanamke ambaye ni Mheshimiwa Samia. Rais wa kwanza Afrika mwanamke kushinda tuzo mbili na kuandika historia ya kipekee nchini,” amesema.

Maraisi waliowahi kupata tuzo hizo kwa Afrika ambazo Rais Samia atakabidhiwa Oktoba 24, mwaka huu kwa Afrika ni Rais wa Liberia, George Weah na Rais wa Botswana Ian Tseretse Khama.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Samia kupokea tuzo akiwa madarakani baada ya Mei 22, 2022 alipokea tuzo ya Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) ikiwa ni kutambua jitihada anazozifanya katika ujenzi wa miundombinu nchini.
Safi Sana na nyingi zaidi zinasubiria.
 
Mkakati wa wachawi wenzake kumlinda ili asisombwe na mafuriko ya team Magufuli.

Hayo yanayitajwa yote yalishakuwepo. Hakuna kipya. Vituo vya afya, madarsa, elimu bure na miundombinu, vilikuwepo.

Alistahili tuzo ya kuuza nchi na kuanzisha tozo kali kwa wananchi.
Utakufa na chuki zako kwa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kipenzi Cha watanzania, kubali au ukatae Ni kuwa mh Rais Samia anakubalika Sana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
 
Najua wafuasi wa Magufuli na wale wa Upinzani ambao wamesahau tulipotoka watabeza na kukejeli tuzo hizi

Ila kwa sisi tunaokumbuka hii nchi ilivyokuwa kabla ya tarehe 17/3/2021 hakika tutaendelea kusheherekea mafanikio ya Rais Samia na kumtakia mema zaidi
Hivi Magufuli alimto...mba mama yako?,kulikoni kupambana hivyo na Marehemu?
 
Tuzo ya Amani?kwani aliikuta nchi iko vitani au kulikuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Ila Wazungu wakikuona hamnazo,wanajua kupamba sana.
 
Tunzo ya Amani duniani...mmmmm Noble peace awards!,kuanzia kwa Tutu, Luthuli, de kleck, madiba na sasa our own president!!!
 
Back
Top Bottom