Tetesi: Rais Samia atavunja Barara la Mawaziri, Biteko atakuwa Waziri Mkuu na Mpina atapewa uwaziri ila mambo yatakuwa ni yale yale

Tetesi: Rais Samia atavunja Barara la Mawaziri, Biteko atakuwa Waziri Mkuu na Mpina atapewa uwaziri ila mambo yatakuwa ni yale yale

Adolf Mkenda labda
Najua ni mchumi ila Mimi sio muumini wa academician Kwa sababu theya are too mechanical Kwa hiyo hapana.

Kimei hajui kuongea hawezi jibu hoja Kwa lugha rahisi ambayo watu ambao sio wachumi wakamwelewa.
 
Kasimu Majaliwa bado yupo sana, Na akiondolewa kwa sasa sioni wa kuvaa viatu vyake, Biteko hata ndala hazimtoshi.
Majaliwa yupo sana tuuuu......Biteko bado sana....adubiri 2026 huko sasa badooo ajifunze sana kwa Majaliwa
 
nishakosa imani kabisa na hawa CCM, maana tunakokwenda sipajui kwa kweli, labda nyie wenzangu.
 
Kwa mtazamo wangu kulingana na hali ya mambo na yanayoendelea Bungeni, hiki ndio kinakwenda kutokea siku si nyingi na mabadiliko haya yatakuwa ni ya kisiasa tu.

Mwigulu na Mbarawa, wanaweza kuondolewa kwa muda halafu baadae wakarudishwa au kubadilishiwa wizara, huku Biteko akipewa uwaziri mkuu na Mpina kupewa uwaziri na Majaliwa kupumzishwa.

In this country, it only needs to be an adult to predict what our politicians are going to do or behave under certain circumstances.
Hakuna kitu kama hicho
 
Ndio alivyodanganywa kuwa Kanda ya Ziwa shida yao ni Wazir Mkuu tena Biteko? Kama ndio mnaamini hivyo miambieni huko Kanda hawana shida na Wazir Mkuu wana shida na Rais mwenye maumuzi magumu dhidi ya ufisadi wa hadharani achilia ule wa siri.
Biteko sio kitu Kanda ya Ziwa dhidi ya Majaliwa, Biteko ni kipenzi cha CCM na sio Wasukuma. Ukiwaambia wamchangue nani wao Wataenda na Majaliwa na sio Biteko kwani wanazo kumbukumbu za Magufuli na Majaliwa na Sio Samia na Biteko.
Muambieni Mama kabisa tena hadharani kuwa yeye sio kipenzi cha Wantanzania na washamstukia mapema mno hata abadili katiba bado haisaidii kitu.
 
Mnaomuwaza Mwigulu na Mbarawa mnapoteza muda na kujipa uchungu bure!

Hawa watu ktk baraza Samia anawahitaji wao 'binafsi' si kingine.

Watu wa aina hii wanaohitajika binafsi na watawala huwepo almost ktk serikali zote duniani na huwa hawagusiki wala kupimwa utendaji wao.
Kwanini anawahitaji wao binafsi...Wana nini Cha ziada kuzidi wengine...?
 
Nimeona Samia ana tabia ya kumteua anayeonekana kuwasumbua mawaziri waliopo, akisema njoo nawe ufanye yale uliyokuwa ukiyasema bungeni, ajabu kwa Mpina hamgusi, sijui anaogopa kitu gani, au anasubiri nini.

- Labda Mpina anaweza kuteuliwa after 2025 election kama atafanikiwa kurudi bungeni, lakini kwa sasa sioni atateuliwa awekwe wapi, hasa nikiona anavyodili zaidi na mambo ya wizara ya fedha, ambapo "mtoto wa mama" kwa sasa anaonekana hagusiki.

Kuhusu Majaliwa kupumzika, hiyo inaweza kutokea after 2025, ambapo Samia ataamua kwenda na Biteko kama PM wake baada ya kumpa experience kwa cheo cha Naibu WM alichonacho sasa, ila sidhani kama itakuwa before 2025.
Majaliwa haondoki kabla ya 2025 kwa sababu kisheria 2025 anamalliza kipindi chake 10 yes na anastaafu rasmi wala baada ya 2025 hawezi kuendelea kuwa Waziri Mkuu Never
 
Majaliwa Lazima avunje Record ya Sumaye. kukaa miaka 14 kama waziri mkuu
Nauliza tu, hivi kwa nini anaandamwa sana.

Maana kwa hali ilivyo anashida. Kwanza alipelekewa biteko, leo makonda anakuja na kumuamrisha. Ningekuwa majaliwa ningeomba kujiuzuru.
 
Back
Top Bottom