Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mpaka sasa Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa awamu ya nne anashikilia rekodi ya kupata kura nyingi na kwa asilimia kubwa katika awamu yake ya kwanza tu katika kutafuta nafasi ya kuingia ikulu tangia mfumo wa vyama vingi uanze.
Napenda kuwakumbusheni na kusisitiza kuwa hoja yangu ipo katika uchaguzi wa kwanza wa mgombea husika. Yaani namaanisha kuwa asilimia alizozipata Hayati Benjamini Mkapa mwaka 1995 alipokuwa anagombea Urais kwa Mara ya kwanza na asilimia alizozipata Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Magufuli Mwaka 2015 alipokuwa anagombea Urais kwa Mara ya kwanza .
Hakuna kati yao aliyefanikisha kupata kura na asilimia alizozipata Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete.kwa sababu Hayati Benjamini Mkapa alipata Asilimia 61 na hata Hayati Dkt Magufuli hakufikia kura na asilimia hizo katika awamu yake ya kwanza ya kuomba Urais alipopambana na Hayati Edward lowassa.
Wakati Mheshimiwa Dkt Kikwete yeye alipata kura takribani asilimia 80 ya kura zote. Na huyu ndiye mgombea wa CCM ambaye alikuwa anakubalika sana hapa nchini kuwahi kutokea tangia mfumo wa vyama vingi uanze katika awamu yake ya kwanza ya kuutafuta Urais. Ni mgombea ambaye alikuwa na mvuto mkubwa sana wa kisiasa na alikubalika na watu wa vyama vyote.
Soma Pia: Tukumbuke: Komredi Polepole ameweka rekodi ya kuipa CCM Ushindi wa 84% kwa Rais wa JMT na 98% kwa Wabunge wa Kuchaguliwa 2020!
Lakini katika awamu yake ya pili yaani 2010 kura zake katika sanduku la kura zilishuka na hata asilimia za kura zake zilishuka ,wakati Hayati Benjamini Mkapa pamoja na Hayati Dkt John Magufuli wao asilimia zao zilipanda sana katika awamu zao za pili katika kutafuta na kutetea nafasi zao. Hapa napo pana mjadala ambao ulipelekea Rais Dkt Jakaya Mrisho kushuka .ambapo siwezi kujadili hapa maana inahitaji andiko la peke yake kuweza kuwachambulia vizuri sana na kwa undani.
Sasa nikiangalia hali ya kisiasa ilivyo hapa Nchini kwa sasa,hasa kukubalika na umaarufu wa Rais Samia kwa watanzania na namna anavyopendwa na kuungwa mkono na watu wa makundi mbalimbali na wa vyama vyote .naona Jemedari wetu Daktari Mama Samia akienda kuivunja Rekodi hiyo inayoshikiliwa na Daktari Jakaya Kikwete kwa kupata kura nyingi za kishindo hapo Mwakani katika Historia ya Taifa letu.
Naona akienda kuvuna mamilioni kwa mamilioni ya kura za ndio katika sanduku la kura na kupata asilimia kubwa zitakazoweka rekodi itakayodumu kwa muda mrefu. Hii ni kwa kuwa ndani ya muda mfupi amefanikiwa sana na kwa kiasi kikubwa sana kugusa Maisha ya mamilioni ya watanzania,kuinua maisha ya watu,kuleta unafuu wa kimaisha ,kujenga matumaini kwa watu,kuwawezesha vijana ambalo ndilo kundi kubwa hapa Nchini. Ambapo sasa vijana wanamkubali sana Rais Samia.lakini kubwa kuliko ni kuwa ameleta maendeleo makubwa sana katika kila secta ambayo siwezi kumaliza kuyaorodhesha hapa jukwaani.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.