Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Yes, tukubali tu kwamba tumeshindwa tumpe mwekezaji aendeshe ili sisi atulipe kodi yetu. Kuna muda Kagame aliomba tumpatie ili awe anatupatia kwa mwezi Trillion 1, tukagoma. 🙂
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Ndgu. Eric Hamisi. Nafasi yake inachukuliwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ndgu. Plasduce Mkeli Mbossa.

Kwahiyo, nikivurunda ninatenguliwa mchezo kwisha. Tena ninatafutiwa nafasi nyingine .Maisha yanaendelea. Saaaafi sana.
 
Walimuondoa yule wa waliyemkuta Kwa figisu wakamuweka huyu wa kwao..
Waendelee hadi kule walimpotoa kalemani sasa kumeoza kabisa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Yule aliye chukua nafasi ya Kalemani,wale ni wenye nchi aka mshikaji wake Kigogo. Yule pamoja na kuharibu hatolewi mpaka 2025.Anakula asali tu kama alivyosema baba yake.
 
Hivi nchi za Ulaya bandari zao nazo zina shida kama hizi zetu? Kama hawana wao wamewezaje kudhibiti? tunashindwa nini kujifunza mifumo ya udhibiti toka kwao?

Maana pale TPA ukichaguliwa ni lazima utatenda dhambi hata kama ulikuwa hutaki kumuudhi muumba wako, maana hela inakufuata yenyewe sasa uikatae sheikh ?
 
Akiwa Oman aligusia uwezekano wa kurahisisha usafirishaji wa viumbe hai kupitia mlango wa bahari. Juzi kati Kuna taasisi ilijiapiza kuzuia mpango wowote wa kusafirisha wanyama hai kutoka eneo hili la Afrika ya Mashariki. Hizi ndimi mbili hizi nilijiuliza sana kwa nini zinakinzana? 😳 🤔
 
Yule aliye chukua nafasi ya Kalemani,wale ni wenye nchi aka mshikaji wake Kigogo. Yule pamoja na kuharibu hatolewi mpaka 2025.Anakula asali tu kama alivyosema baba yake.
Tena nikwambie hakuna sehemu saiz haivuji watu wanatafuna sana! Mfano pale TRA ndo usiseme! Ila machawa walivyo vichwa maji eti mama anaupiga mwingi! Kamishina mkuu wa TRA ni shida jipu linalosubiria kutumbuka! Makamba yeye yuko njiani maana anachokifanya hakieleweki! Sema pia shida ni mama mwenyewe kukubali kudangavywa na wapigaji!
 
Hivi nchi za Ulaya bandari zao nazo zina shinda kama hizi? Kama hawana wao wamewezaje kudhibiti? tunashindwa nini kujifunza mifumo ya udhibiti toka kwao?

Maana pale TPA ukichaguliwa ni lazima utatenda dhambi hata kama ulikuwa hutaki kumuudhi muumba wako, maana hela inakufuata yenyewe sasa uikatae sheikh ?
🤣🤣🤣tunaambiwa pale pamejaa maafisa sasa wanakazi gani
 
Yes, tukubali tu kwamba tumeshindwa tumpe mwekezaji aendeshe ili sisi atulipe kodi yetu. Kuna muda Kagame aliomba tumpatie ili awe anatupatia kwa mwezi Trillion 1, tukagoma. 🙂
TICS wenyewe hawatupi hio Tirioni 4...wanalipa bilioni 14 kwa mwaka, tena baanda ya heka heka za mwendazake b4 walikua wanalipa bilioni7...muwekezaji mwingine ndo kabisaa hatutapata kitu.
 
Back
Top Bottom